Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  28 Rajab 1441 Na: 1441 H / 014
M.  Jumatatu, 23 Machi 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Katika Janga hili, Lazima tumtegemee Mwenyezi Mungu (swt), Tutafute rehma zake (swt), na Tukimbilie Kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (swt)

Bangladesh inakaribiwa kukabiliwa na janga kwani kuzuka kwa virusi vya korona, kumeanza kuleta uzito, watu wanamaliza siku zao kwa wasiwasi na kutokuwa na hakika. Wataalamu wa afya na wananchi wanaofahamu wamekasirika sana kuona serikali kutojitayarisha kamwe na hatua za kudhibiti mkurupuko huo hata ingawa walikuwa na muda zaidi ya miezi miwili mkononi wakati virusi hivyo viligunduliwa kwa mara ya kwanza huko Wuhan, Uchina mnamo Disemba 2019. Badala yake serikali hii ya wajinga ilikuwa imejishughulisha kusherehekea Maadhimisho ya Mujib wakati ikihatarisha watu kutokana na janga la “virusi vipya vya korona”. Pamoja na vituo vibaya vya afya, uhaba wa mavazi ya kujikinga kwa wafanyikazi wa huduma ya afya, kutokuwepo kwa vifaa vya upimaji, na ufuatiliaji usiofaa wa mawasiliano na utaratibu wa kutoa taarifa, serikali hii bado inacheza siasa na kiwango na ukali wa mkurupuko wa virusi vya korona nchini Bangladesh, na kukandamiza kutofaulu kwao, wanakandamiza kikamilifu habari yoyote ya idadi ya walioathirika na vifo kupitia vitisho. Wakati matayarisho ya serikali ni duni kupambana na janga hili hatari, Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh inataka kulingania uangalifu wa watu wetu kwa ushauri kadhaa na miongozo ya dhati:

Kwanza, hatupaswi kushtuka na kuogopa katika wakati mgumu kama huu, na badala yake kukumbuka kuwa mkurupuko huu watoka kwa Mwenyezi Mungu Azza Wa Jal ambao twahitajika kukabiliana nao kwa uvumilivu na kuzidisha kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Kama kipenzi chetu Mtume Muhammad (saw) alivyosema:

«عَجَبًا لِأَمْرِ الْمُؤْمِنِ إِنَّ أَمْرَهُ كُلَّهُ خَيْرٌ، وَلَيْسَ ذَاكَ لِأَحَدٍ إِلَّا لِلْمُؤْمِنِ، إِنْ أَصَابَتْهُ سَرَّاءُ شَكَرَ فَكَانَ خَيْرًا لَهُ، وَإِنْ أَصَابَتْهُ ضَرَّاءُ صَبَرَ فَكَانَ خَيْرًا لَهُ»

“Ni ajabu ilioje kwa jambo la Muumini; hakika kila jambo lake kuna kheri na hili si kwa yeyote isipokuwa muumini. Likimpata yeye jambo zuri, anamshukuru Mwenyezi Mungu na hilo ni kheri kwake; na likimpata yeye jambo baya, anasubiri na hilo ni kheri kwake.” [Muslim].

Pia kuzuka kwa virusi hivi ni ukumbusho kwetu sote, ikiwemo Wamagharibi kuwa jinsi gani tuko dhaifu mbele ya Mwenyezi Mungu (subḥānahu wa taʿala) bila kujali nafasi yetu ya kifedha au maendeleo ya kiteknolojia/matibabu.  Kwa hivyo, sasa ndio wakati wakuwa karibu zaidi na Mwenyezi Mungu (swt), kutaka msamaha kwa makosa yetu na kukimbilia kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (swt).

Pili, hatupaswi kutenda kama Makafiri-Washirikina. Tunapaswa kujiweka mbali na kuzuia bidhaa na hivyo kuzua majanga ya mahitaji ya kila siku. Hatupaswi kuwa wabinafsi, wachoyo na kutojali wengine, lakini badala yake tunapaswa kuwajibika na kusaidiana. Usisahau kuwa, sisi ni Waislamu, tumeinuliwa kama mfano kwa wanadamu. Mwenyezi mungu (swt) asema,

[وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا]

“Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Ummah wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu” [Surah Al-Baqarah: 143].

Tatu, Tunapaswa kumtegemea Mwenyezi Mungu (swt) na kuendelea kusubiri, badala ya kuipa nafasi hofu. Lazima tukumbuke kuwa Ajali-Kifo-Riziki ziko mikononi mwa Mwenyezi Mungu (swt). Yeye (swt) asema:

[وَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَنْ تَمُوتَ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّهِ كِتَابًا مُؤَجَّلًا]

“Na haiwezi nafsi kuwa ife ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu kama ilivyo andikwa ajali yake” [Surah Al-i-Imran: 145];

[وَمَا مِنْ دَابَّةٍ فِي الْأَرْضِ إِلَّا عَلَى اللَّهِ رِزْقُهَا وَيَعْلَمُ مُسْتَقَرَّهَا وَمُسْتَوْدَعَهَا كُلٌّ فِي كِتَابٍ مُبِينٍ]

“Na hakuna mnyama yeyote katika ardhi ila riziki yake iko kwa Mwenyezi Mungu” [Surah Hud: 6]; na “Hakika Mwenyezi Mungu ndiye mwenye kuruzuku, Mwenye nguvu, Madhubuti” [Surah Adh-Dhariyat: 58]. Mwenyezi Mungu (swt) pia anasema:

[قُلْ لَنْ يُصِيبَنَا إِلَّا مَا كَتَبَ اللَّهُ لَنَا هُوَ مَوْلَانَا وَعَلَى اللَّهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ]

“Sema: Halitusibu ila alilotuandikia Mwenyezi Mungu. Yeye ndiye Mola wetu Mlinzi. Na Waumini wamtegemee Mwenyezi Mungu tu!” [Surah At-Tawba: 51].

Nne, kama maeneo kadhaa nchini Bangladesh tayari yameripotiwa kuwa na wagonjwa wa “virusi vilivyozuka vya korona”, tunapaswa kuwa waangalifu katika kutembelea maeneo hayo. Na iwapo virusi vitaanza kuenea huko, hatupaswi kuenda huko kama sehemu ya wajibu wa Sheria kama Al-Bukhari alivyopokea: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alisema:

«الطَّاعُونُ رِجْزٌ أُرْسِلَ عَلَى طَائِفَةٍ مِنْ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَوْ عَلَى مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ فَإِذَا سَمِعْتُمْ بِهِ بِأَرْضٍ فَلَا تَدْخُلُوا عَلَيْهِ وَإِذَا وَقَعَ بِأَرْضٍ وَأَنْتُمْ بِهَا فَلَا تَخْرُجُوا فِرَارًا مِنْهُ»

“Tauni ni janga (au adhabu) iliyotumwa kwa Wana wa Israeli, au kwa wale waliokuwa kabla yenu. Mutakaposikia habari zake katika ardhi fulani, Musiende huko, na ikizuka katika ardhi uliyokuwamo, usiondoke, kuikimbia.

Mwishowe, Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[ظَهَرَ الْفَسَادُ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ بِمَا كَسَبَتْ أَيْدِي النَّاسِ لِيُذِيقَهُمْ بَعْضَ الَّذِي عَمِلُوا لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ]

“Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyoyafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu.” [Surah Ar-Rum: 41]. Kutokea siku ambayo tumepoteza Khilafah yetu tumekuwa chini ya nidhamu zilizoundwa na mwanadamu, na tukapoteza rehema ya Mwenyezi Mungu (swt). Chini ya Mfumo huu ulioundwa na mwanadamu, sio tu tunakandamizwa, lakini badala yake majanga ya kutengenezwa moja baada ya jingine yanatuangukia sisi. Kwa hivyo, lazima tujumuishe juhudi zetu zote kuirudisha Khilafah ili kuweka rehema katika dunia hii, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) asema:

«السُّلْطَانُ ظِلُّ اللَّهِ فِي الْأَرْضِ»

“Sultani (Khalifah) ni kivuli (rehema) cha Mwenyezi Mungu ardhini.” [Al-Daraqutni].

Sera za huduma za afya za Dola ya Khilafa zitafungua mlango wa maabara za kisayansi na utafiti kwa raia wake wote sio kwa ajili ya kupata faida, lakini kama jukumu la Dola kutimiza mahitaji ya umma kwa afya na ustawi. “Wanajamii wote wana haki ya kuanzisha maabara za kisayansi kuhusiana na mambo ya maisha, na serikali yenyewe inapaswa kuanzisha maabara kama hizo.” [Kielelezo cha Katiba ya Dola ya Khilafah cha Hizb ut Tahrir] Hesabu za uvumbuzi wa “virusi vya korona” vifaa vya kupimia katika sekta ya kibinafsi, uzalishaji wa viosha mkono vya bei ya chini, nk tayari umeonyesha kuwa Umman nchini Bangadesh umejaa vipaji na talanta; Khilafah ya Uongofu pekee ndiyo inayohitajika sasa kuhakikisha kuwa mfumo tofauti wa huduma za afya kama rehema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa wanadamu wote. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنْ السَّمَاءِ وَالأَرْضِ وَلَكِنْ كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ]

“Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamungu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma.” [Surah Al-A'raf: 96]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu