Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  27 Dhu al-Qi'dah 1443 Na: 1443 H / 24
M.  Jumapili, 26 Juni 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Huku Watu Walioathiriwa na Mafuriko Wakililia Chakula na Makaazi, Serikali ya Hasina Yawalazimisha Watu Kusherehekea Uzinduzi wa Mradi wake wa Uporaji Mkubwa wa Daraja la Padma - Ikifichua ‘Muujiza wa Maendeleo’ wa Mfumo Mbovu wa Utawala wa Kirasilimali

(Imetafsiriwa)

Takriban nusu ya Bangladesh sasa iko katika mshiko wa mafuriko mabaya zaidi kuwahi kutokea kutokana na kuteremka kwa maji mengi sana ya mvua masika kutoka kwenye vilima vinavyozunguka eneo la Meghalaya nchini India. Takriban watu milioni sita wa maeneo ya kaskazini na kaskazini-mashariki mwa Bangladesh wamekwama au wamekimbia makaazi yao katika maeneo ya nyanda za chini kaskazini-mashariki mwa nchi. Watu wengi wamekufa na wengine wako katika hali mbaya ya kibinadamu huku watu waliokwama wakihangaika kutafuta makaazi, kupata maji na milo kwa siku saba zilizopita. Msaada wa serikali upo kwenye karatasi na umefungika katika utoaji muhtasari wa kila siku pekee wa maafisa lakini kiuhalisia mamilioni ya watu wangali wanalilia bidhaa chache za misaada. Hasa wananchi wa kawaida wanajitolea elimu, ujuzi, rasilimali na fedha zao katika shughuli za misaada na uokoaji huku serikali ya Hasina ikiwa na shughuli nyingi kusherehekea uzinduzi wa Daraja la Padma. Ili kusherehekea uporaji wao mkubwa, serikali imetenga sehemu kubwa ya fedha, kwa mfano, Taka milioni 90 zilitengwa kwa ajili ya vyoo tisiini vya umma vinavyojengwa kwa ajili ya mikusanyiko ya watu siku hiyo ya uzinduzi. Ambapo ni Taka 6.55 pekee na chini ya nusu kilo ya mchele kwa kila kichwa ndiyo imetengwa kwa ajili ya watu milioni 4 wa maeneo yaliyokumbwa na mafuriko (The Daily Star, Juni 22, 2022)! Wamekuwa wakatili na waovu ilioje watawala hawa wa kisekula kwamba sasa wanadhihaki mateso ya watu. Baada ya ‘kukagua’ masaibu yasiyoelezeka ya watu katika maeneo yaliyokumbwa na mafuriko kutoka juu ya helikopta, Hasina aliyaelezea mafuriko ya sasa kuwa “hakuna jipya” na pia akasema kwamba “(mafuriko) yana mambo chanya vilevile”! Hakutaka kujisumbua kukutana na wahasiriwa wa hata nyumba moja wakati wa ile inayoitwa ziara yake ya ukaguzi. Badala ya kufikiria kusuluhisha masaibu ya wahasiriwa, serikali ya Hasina ina shughuli nyingi kulazimisha 'maendeleo' yao kwa watu. Ili kuficha ufisadi wao mkubwa na uporaji katika ujenzi wa Daraja la Padma, wanataka watu wawe katika hali ya sherehe. Kwa hivyo, mtihani wa SSC uliakhirishwa na masomo ya chuo kikuu yalighairiwa kwa sababu ya kuzinduliwa kwa Daraja la Padma!

Enyi Watu! Hii ndio sura mbaya ya sera za Kirasilimali zinazotekelezwa na Benki ya Dunia au tabaka tawala la Mabepari ambapo ‘maendeleo’ yanakusudiwa tu kwa watawala wa kisekula, mabepari wakubwa na wakoloni, na hakuna nafasi ya watu wengi ndani yake. Inajulikana kuwa serikali ya Hasina ilipora mamilioni ya dolari kutoka kwa mradi huu kwa kuongeza gharama ya mradi wake karibu mara tatu zaidi ya makadirio ya awali. India ilitoa ruzuku kamili ya dolari milioni 200 kwa serikali ya Hasina kwa mradi huu kwani unatumika kama njia yake ya usafiri baina ya Kolkata hadi Agartola kupitia Dhaka na maslahi ya muda mrefu ya kijiografia na muunganisho ("India inatoa ruzuku kamili ya $200 milioni ambayo ilikuwa imeahidi kwa Daraja la Padma", bdnews24. com, 16 Julai 2015). China pia ilifurahishwa na kutunukiwa tuzo ya ujenzi wa daraja hilo kwani itapata maslahi yake ya kiuchumi. Kwa kuwafurahisha wadau wote wakuu na kupora pesa za watu, serikali ya Hasina imeweka mizigo yote ya gharama kwenye bega la watu; imependekeza ushuru wa juu wa madaraja ambapo maisha ya watu na riziki zao zitatatizika. Upinzani wa kisekula umefichua sura zao halisi kwa kujitia upofu kuhusu maslahi ya Dola ya Kishirika na sera ya Kirasilimali kana kwamba mradi huu ungekuwa bora zaidi kama ungefanywa na taasisi ya kirasilimali – benki dunia.

Iwapo maendeleo chini ya utawala wa kisekula yangekuwa yanalenga watu kweli, basi sehemu ndogo kutoka kwa mradi huu wa daraja la Padma ingeweza kuelekezwa katika kujenga matuta yenye ubora katika maeneo ya Haor (ardhi nyevu) ili kulinda riziki, mazao na rasilimali. Suluhu zinazofaa za uchimbaji na miamba zingekuwepo kufikia sasa kulinda maeneo ya chini, yanayokabiliwa na mafuriko ya masika kila mwaka. Uzembe wa watawala hawa wa kisekula kwa watu umefikia kiwango cha juu kiasi kwamba timu za operesheni za uokoaji za kijeshi zinatumia ‘viroba vya migomba’ kuokoa watu wanaohangaika kuhama kutokana na uhaba wa boti katika maeneo hayo. Ni tabia ya kimataifa kwamba raia wa kawaida kamwe sio kipaumbele katika mfumo wa utawala wa Kirasilimali. Kwa mfano, Misri, Uturuki na Pakistan zinaendesha miradi mingi mikubwa kulingana na sera za ukoloni mamboleo kwa kuzifadhili kupitia madeni na mikopo ya kigeni kutoka Benki ya Dunia na IMF; matokeo yake, licha ya ukuaji wao mzuri wa Pato la Taifa katika nchi hizi, kwa upande mmoja wanalemewa na madeni makubwa ya kigeni, na kwa upande mwingine kuyumba kwa uchumi, umaskini na ukosefu wa usawa wa mapato unaongezeka kila mwaka.

Enyi Waislamu! Historia ni shahidi kwamba ni mfumo wa utawala wa Khilafah pekee ndio uliowajali wanadamu bila kuzingatia tabaka, rangi na dini. Chini ya Khilafah, maendeleo yalikuwa yakizingatia watu kikweli na hakujawahi kuwepo kipote chochote cha wachache kutumia miradi mikubwa kwa manufaa yao. Khalifa wa pili Umar (ra) pia alitekeleza miradi mikubwa ya kuboresha maisha ya watu. Alimuamuru gavana wa Misri Amr ibn al-As (ra) kujenga mkondo unaounganisha Mto Nile na Bahari Nyekundu ili kutokatiza usambazaji wa chakula kwa raia wa Madina wakati wa baa la njaa. Chini ya uongozi wa Umar (ra), Mkondo huu wa Amir al-Mu’minin wenye urefu wa kilomita 138 (maili 85.7) ulijengwa ndani ya miezi sita tu. Bahari hizo mbili ziliunganishwa ambayo ilikuwa ndoto kubwa ya wafalme wa awali wa Uajemi na Warumi ambayo haikuwa imetimia. Pia, wakati mji wa Basra wa Iraq ulipoanzishwa wakati wa utawala wa Umar, yeye (ra) alianza kujenga mkondo wa maili tisa kutoka Tigris hadi mji huo mpya kwa ajili ya umwagiliaji maji mimea na maji ya kunywa.

Enyi Waislamu! Mumewavumilia watawala hawa wasaliti wa kisekula kwa muda wa kutosha na sasa ni wakati mwafaka muwaondoe na mfumo wa utawala wa kirasilimali unaowazalisha. Munaweza kupinga na kuwakosoa watawala, kupanga mikutano na makongamano kuhusu usimamizi wa maafa ya mafuriko. Lakini kufikia sasa mulipaswa kutambua kwamba taabu yenu haitakwisha hadi mfumo huu wote wa utawala wa kisekula uondolewa. Majanga ya kimaumbile sio tatizo lisiloweza kudhibitiwa lenyewe, bali mfumo mbovu na potofu wa kisekula wa kirasilimali wenyewe ni janga kwa wanadamu wote kote ulimwenguni, ambao kamwe haujali ustawi wa raia wa kawaida. Isipokuwa muchukue hitaji la mara moja la Khilafah Rashida kwa njia ya Utume na kung'oa mfumo wa kirasilimali, siku zinazofuata zitakuwa mbaya zaidi kuliko ilivyo sasa. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

]وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكًا وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Surah Taha: 124].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu