Ijumaa, 11 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/03
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Australia

H.  1 Rabi' II 1447 Na: 03 / 1447 H
M.  Jumanne, 23 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kutoka Uingereza hadi Australia: Utambuzi wa Uongo Unafungua Njia ya Uhalalishaji Mpana zaidi wa Mahusiano

(Imetafsiriwa)

Miaka miwili baada ya mauaji ya halaiki yaliyofanywa na umbile la Kizayuni katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, likiungwa mkono kikamilifu na Marekani, NATO, na washirika wao makruseda, Umoja wa Mataifa na dola zenye nguvu duniani wamejibu kwa kulituza umbile hilo. Utambuzi wa “Dola ya Palestina” unakuja huku Gaza ikivuja damu, na baada ya dola 150+ tayari kutoa utambuzi sawia.

Uingereza, ambayo iliunda umbile hilo mwaka 1948 kwenye ardhi iliyokoloniwa, sasa inataka kuosha mikono yake kutokana na jukumu huku ikiendeleza sera dhidi ya Umma wa Kiislamu na kuzuia kurudi kwake chini ya Khilafah inayotawala kwa sheria ya Mwenyezi Mungu. Australia, Canada, na Ureno zilifuata Uingereza. Waziri Mkuu wa Albanese alitangaza: “Australia inatambua rasmi Dola huru ya Palestina.”

Hata hivyo hakuna hata mmoja wa viongozi hawa anayeweza kubainisha mipaka ya hiyo inayoitwa dola, kwa kuwa umbile la Kizayuni linadhibiti karibu Palestina yote na hata kutaka upanuzi wake kati ya Mto Nile na Furat. Utambuzi huu si chochote ila ni kifuniko cha kisiasa: jaribio la kuziondolea hatia serikali za Magharibi kutokana na kushiriki katika mauaji. Unatumikia umbile hilo pekee, sio watu wa Palestina, ambao wamekabiliwa na kifo na mateso kwa zaidi ya miaka 70, haswa katika miaka hii miwili iliyopita.

Hatua hizi pia zafungua njia ya kuhalalisha mahusiano. Tawala za khiyana katika ulimwengu wa Kiislamu zitafuata, zikilipa umbile hilo “uhalali” sio tu kutoka kwa Umoja wa Mataifa unaoongozwa na Marekani, bali kutoka kwa dola ambazo zinapaswa kuwa zinautetea Umma.

Hata umbile la Kizayuni lilikataa ishara hiyo. Netanyahu aliapa kuwa kamwe hakutakuwa na dola ya Palestina, akiahidi kuendeleza kampeni kuelekea “azimio la mwisho”, akimaanisha, mauaji zaidi na uhamisho. Ili kulihakikishia umbile hilo, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer alidai utambuzi “utafufua matumaini ya amani,” akijiunga na nchi 150+, na akaiweka kama sehemu ya msukumo wa suluhisho la dola mbili linaloanza na kusitishwa kwa mapigano na kuachiliwa huru kwa wafungwa. Kiuhalisia, hili linatoa tu ulinzi na usalama kwa dhalimu ambaye amekiuka desturi zote za kibinadamu na za kimungu.

Umma wa Kiislamu lazima utimize wajibu wake: uwanusuru watu wake wa Palestina na ufanye kazi ya kukomboa ardhi yote inayokaliwa kwa mabavu kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume kwa kufuata mfano wa Umar al-Faruq katika kuifungua Bayt al-Maqdis na Salah al-Din katika kuikomboa kutoka kwa Mkruseda.

Jihadharini na wanafiki wanaojifanya kuunga mkono lakini wanakula njama dhidi ya Ummah, hasa Umoja wa Mataifa na wanachama wake wa kudumu, ambao wapo ili kuzuia umoja wa Waislamu chini ya sheria ya Mwenyezi Mungu na ulinzi kwa wanaodhulumiwa.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[قُلْ يَا قَوْمِ اعْمَلُواْ عَلَى مَكَانَتِكُمْ إِنِّي عَامِلٌ فَسَوْفَ تَعْلَمُونَ مَن تَكُونُ لَهُ عَاقِبَةُ الدِّارِ إِنَّهُ لاَ يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ]

“Sema: Enyi watu wangu! Fanyeni muwezayo, na hakika mimi nafanya. Mtakuja jua nani atakuwa na makaazi mema mwishoni. Hakika madhaalimu hawatafanikiwa.’” [Al-An‘am: 135].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Australia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Australia
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu