Jumapili, 24 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/30
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Amerika

H.  16 Sha'aban 1445 Na: 02 / 1445 H
M.  Jumatatu, 26 Februari 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Agubikwa na Moto

(Imetafsiriwa)

Katika hali ya kusikitisha ya kujichoma moto kwa watawa wa Kibudha wakati wa Vita vya Vietnam, mwanachama anayehudumu wa Jeshi la Wanahewa la Marekani mnamo Februari 26, 2024, alijichoma moto mbele ya ubalozi wa 'Israel' jijini Washington D.C., akitangaza, "Sitakuwa mshiriki tena katika mauaji ya halaiki.” Huku akiwa amegubikwa na moto, alirudia mara kwa mara kupiga kelele, “Iacheni Huru Palestina,” kilio cha kufadhaisha na kutapatapa cha haki ambacho kinaambatana na uchungu mkubwa wa kimaadili juu ya ushiriki wa Marekani katika mauaji ya halaiki yanayoendelea huko Gaza. Kitendo hiki cha kujiua, ni mithili ya watawa ambao, mnamo 1963, walichagua kujiunguza moto hadi kufa kwa kupinga vita na mateso, sio tu ni kulaani dhidi ya vita; ni kauli ya kina dhidi ya kushiriki katika ukatili ambao askari hakuweza tena kuvumilia ushiriki wake katika mauaji ya halaiki yanayoendelea Gaza.

Kuhusika kwa Jeshi la Wanahewa la Marekani katika kulisaidia jeshi la 'Israel' kunathibitishwa vyema. Ripoti kutoka ‘The Intercept’ zinafichua kuwa Marekani imekuwa na mchango mkubwa katika kubainisha malengo ya kampeni za ulipuaji wa mabomu ambayo yamesababisha idadi kubwa ya vifo kuzidi watu 30,000. Mwanajeshi wa anga aliyejichoma moto alifahamu kwa undani kuhusika moja kwa moja kwa jeshi la Marekani katika mauaji ya halaiki yanayoendelea. Kitendo chake cha kujichoma moto mbele ya ubalozi wa umbile la Kizayuni ilikuwa ni kauli ya kuuonyesha ulimwengu mzima ukatili walioufanya na muhimu zaidi kuungwa mkono na serikali yake inayochochea mauaji ya halaiki kwa fedha na silaha.

Dori ya Marekani katika mzozo huo inaenea zaidi ya msaada wa kijeshi tu. Marekani inaendelea kutuma mabomu na zana za kivita kwa umbile la Kizayuni, ikifahamu fika kwamba silaha hizo zinatumiwa kuwalenga raia kama sehemu ya mkakati wa pamoja wa adhabu ya umbile hilo la Kizayuni. Ushirikiano huu katika kulenga maisha ya watu wasio na hatia unaangazia jinsi nchi za Magharibi zinavyoendelea kuwaona Waislamu kama mali ya bei nafuu ambayo inaweza kutupwa kama "uharibifu mkubwa." Utangazaji wa vyombo vikuu vya habari, au kukosa kutangaza kwake, wa matukio haya unahusu vile vile. Kimya cha vyombo vikuu vya habari kuhusu kujiua kwa mwanahewa huyo na muktadha mpana wa ushiriki wa Marekani katika mauaji ya halaiki unaonyesha ushirikiano kamili na sera za Ikulu ya White House. Ukosefu wa uangaziaji hutumika kuficha ukweli wa hali kutoka kwa wananchi wa Marekani, ambao wengi wao wanapinga kwa kiasi kikubwa mauaji ya halaiki yanayofanywa. Licha ya upinzani wa umma, utawala wa Biden unaendelea kulipatia jeshi la umbile la Kizayuni silaha na kulinda vitendo vyake kwenye jukwaa la kimataifa.

Kimya kutoka kwa majeshi ya ulimwengu wa Kiislamu kinatia uziwi masikio. Msimamo wa kijasiri ulioonyeshwa na mwanajeshi huyu asiyekuwa Muislamu, ambaye alichukua msimamo dhidi ya kushiriki katika mauaji ya halaiki, unakinzana kabisa na kutochukua hatua kwa viongozi wa kijeshi wa Kiislamu. Mwanajeshi huyu, asiyefungamana na dini ya Kiislamu wala kubeba itikadi ya jihad inayopaswa kuwatia moyo askari wa Kiislamu, ameonyesha kiwango cha ushujaa na uthabiti wa kimaadili unaowaaibisha viongozi wa majeshi ya Kiislamu. Matendo yake yanaonyesha kufeli kwa kiasi kikubwa: kutokuwepo kwa ujasiri kati ya wale ambao wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuwatetea wanyonge. Ni kwa uongozi wa kisiasa wa Khilafah pekee ndipo majeshi yanaweza kutumika kulinda heshima ya Waislamu badala ya kuwatumia kuwakandamiza Waislamu.

Kisha swali linazuka: inakuwaje mwanajeshi kutoka nchi ya kigeni, asiye na wajibu wa moja kwa moja wa kidini kwa watu wa Palestina, aonyeshe aina ya ujasiri na uadilifu wa kimaadili unaopita ule wa viongozi wa majeshi ya Kiislamu? Tofauti hii sio tu kufeli kwa ushiriki wa kijeshi bali ni kufeli kwa uongozi wa jeshi la Waislamu. Kimya na kutochukua hatua kwa viongozi hawa mbele ya mauaji ya halaiki yanayoendelea sio tu usaliti kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw) bali pia unahujumu kiini hasa cha ushujaa wa wanaume ambao ungepaswa kuwa na sifa ya askari wa Kiislamu. Ulimwengu unaweza kutambua ujasiri wa mwanahewa huyu wa Marekani kama kioo kinachoakisi mapungufu yetu wenyewe. Wakati umewadia kwa viongozi wa majeshi ya Kiislamu kuwasilisha ari ya kweli ya kujitahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu (swt), kuwatetea wanaodhulumiwa, na kusimama dhidi ya dhulma.

[وَمَا لَكُمْ لاَ تُقَاتِلُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَالْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاء وَالْوِلْدَانِ الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا أَخْرِجْنَا مِنْ هَـذِهِ الْقَرْيَةِ الظَّالِمِ أَهْلُهَا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّا وَاجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا]

Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako [4:75]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Amerika

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Amerika
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu