Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  10 Dhu al-Hijjah 1443 Na: 1443 H / 039
M.  Jumamosi, 09 Julai 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Pongezi kutoka Hizb ut Tahrir kwa Mnasaba wa Idd Al-Adha Iliyobarikiwa ya Mwaka 1443 H

(Imetafsiriwa)

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La Ilaha illa Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Wa lillahi Alhamd

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa walimwengu wote, Muweza wa yote, Mwenye nguvu, Aliyetukuka, Mkuu. Yeye aliye na funguo za utukufu unaotarajiwa, kwazo huwanusuru wale wanaomnusuru. Yeye ni Muweza juu ya yote. Na rehema na amani zimshukie Mtume Mtukufu (saw) aliyelingania Uislamu, akaifikisha Qur’an, akawapanga Maswahaba juu ya Wahyi, akasimamisha dola na akaumakinisha mfumo wa Uislamu, bwana wa viumbe, bwana wetu Muhammad, na kwa familia yake yote na maswahaba.

Machozi ya matamanio yanaangaza kwenye nyuso za Mahujaji wanapoiaga Al-Kaaba tukufu, na ukaribu wa nyoyo za Waislamu unatia manukato viwanja vya Swala za Idd kwa bashasha na furaha, na furaha ya watoto wa Kiislamu wanaocheza kama ndege wenye nishati, iliyopambwa kwa nguo za Eid... Ni Eid Al-Adha; siku za furaha ambazo zinapaswa kuenea katika ardhi za Waislamu. Eid Mubarak kwenu.

Kwa mnasaba huu, Hizb ut Tahrir inatoa pongezi na baraka zake nyingi kwa Ummah mzima wa Kiislamu, ikimwomba Mwenyezi Mungu (swt) aumiminie siku za raha, furaha na utulivu, na kuujaza Ummah kwa baraka Zake.

Vile vile napenda kutoa pongezi zangu na za Mkuu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na ndugu na dada wote wanaofanya kazi katika idara na vitengo vyake kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, Mwenyezi Mungu amhifadhi, nikimuomba Mwenyezi Mungu (swt) aukirimu Ummah wa Kiislamu kwa ushindi na tamkini kupitia mikono yake.

Idd inakuja wakati Ummah unakabiliwa na ongezeko kubwa la mashambulizi dhidi ya kile kilichosalia cha mafungamano na Uislamu. Baada ya miongo kadhaa ya uharibifu wa vita vya moja kwa moja na vya wakala ambapo nchi za Magharibi zilijaribu kupata udhibiti wa rasilimali na miji mikuu ya Umma wa Kiislamu, Amerika na wale waliokuwa pamoja nayo kutoka nchi za Kiislamu walitoka kijeshi na kuwakabidhi vibaraka wao ambao walikuwa wamezama kwenye giza na uhalifu nyoyoni mwao, ili kuuhujumu zaidi kijamii. Hivyo basi, Magharibi ilitabanni "sera ya nguvu" katika kufungua milango ya jumuiya za nchi za Kiislamu kwa maovu ya jamii ya Kimagharibi.

Magharibi mkolono kafiri tayari imefufua katika nchi yake mila za watu wa mataifa ya kale ambazo zilikemewa na Qur’an, hivyo maradhi mbalimbali ya kijamii yalizuka huko. Kwa kuongezeka kwa magonjwa haya katika nchi za Magharibi, leo hii imefikia hatua ya ugonjwa hatari; kuanzia matendo ya watu wa Lut (ushoga), hadi yale aliyoyafanya Firauni katika kuua watoto, hadi upagani wa wale waliokuja baada ya kuangamizwa kwa watu wa Nuhu. Leo, Magharibi imekwama katika hali mbaya ya uasherati, uvumbuzi wa suala la jinsia, na kuzidisha kwake ukosefu wa kujistiri kimwili, hadi katika suala la kuhalalisha mauaji ya vijusi, mpaka kwa wazo la uasi dhidi ya sheria kutoka kwa Muumba, hadi kuenea kwa kutofuata dini, na kuzidisha ukafiri, ikiwemo janga la unyogovu na matumizi ya dawa za kulevya, ambayo ni ncha tu ya mlima wa theluji kwa bomu linaloendelea kuhesabu madakika kulipuka kwake la mujtamaa wa Kimagharibi.

Na kwa sababu Magharibi inafahamu uzito wa matukio yanayotokana na machukizo hayo, inataka kuyaeneza katika ardhi zetu ili kuzilemaza hadi itakapomaliza mgogoro wake na Urusi na China, kisha ikamilishe ukoloni wake.

Kwa hivyo, Magharibi leo imekuwa shimo jeusi, inayotishia kuwameza wanadamu kwenye giza linalojulikana na Mwenyezi Mungu pekee.

Enyi Waislamu:

Hamtaregea kuwa Umma bora uliotolewa kwa wanadamu mpaka muinuke, na muwaamrishe kufanya mema mliyoyabeba na muwakataze maovu ambayo wamezama ndani yake. Hakuna wa kukuongozeni kwenye hayo isipokuwa Mtawala atakayekurudishieni Khilafah kwa njia ya Utume, akifuata mfano wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kama Makhalifa waongofu, Mwenyezi Mungu awe radhi nao walivyokuwa. Kwa hivyo, mtaenea katika ardhi kama washindi, ili kusimamisha sheria ya Mwenyezi Mungu, na kuwatoa wanadamu kutoka kwenye giza la mifumo iliyotungwa na wanadamu kuwapeleka kwenye nuru ya wazi ya Uislamu. Mwenyezi Mungu asema: ﴾كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ﴿ “Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu” [Aali-Imran: 110]. Mwenyezi Mungu (swt) pia asema: ﴾الر كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ لِتُخْرِجَ النَّاسَ مِنَ الظُّلُمَاتِ إِلَى النُّورِ بِإِذْنِ رَبِّهِمْ إِلَى صِرَاطِ الْعَزِيزِ الْحَمِيدِ﴿ “Alif Lam Ra. (A.L.R.) Hichi ni Kitabu tulicho kiteremsha kwako ili uwatowe watu kwenye giza uwapeleke kwenye muwangaza, kwa idhini ya Mola wao Mlezi, uwafikishe kwenye Njia ya Mwenye nguvu, Msifiwa” [Ibrahim: 1].

Kwa kila mtu binafsi katika watu wenye nguvu na ulinzi:

Watawala wa Waislamu wamemfanyia khiyana Mwenyezi Mungu, Mtume Wake na Waislamu, na umedhihiri uovu na dharau kutoka kwao ambayo haitoki tena machoni mwao na kuona huko hakuwezi tena kuepukika. Enyi watu wa Nusra, mpaka lini mtawasaidia wasaliti hawa?! Na mpaka lini mtaupa kisogo Umma wa bwana wenu Muhammad (saw)?! Mumeona jinsi Magharibi ilivyo tayari kumtupa mmoja wenu chini ya magurudumu ya watu kwa mpepeso wa macho ili kuisimamisha treni ya mabadiliko. Huku Waislamu wakiwainua juu ya mabega yao wale wanaowaunga mkono na kuandika majina yao kwa wino wa nuru. Je, mnasimama na timu gani kati ya hizo mbili, enyi watu wa Nusra? Mwenyezi Mungu asema ﴾مَّن كَانَ يُرِيدُ الْعَاجِلَةَ عَجَّلْنَا لَهُ فِيهَا مَا نَشَاء لِمَن نُّرِيدُ ثُمَّ جَعَلْنَا لَهُ جَهَنَّمَ يَصْلاهَا مَذْمُوماً مَّدْحُوراً * وَمَنْ أَرَادَ الآخِرَةَ وَسَعَى لَهَا سَعْيَهَا وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَئِكَ كَانَ سَعْيُهُم مَّشْكُوراً﴿ “Anaye taka yapitayo upesi upesi, tutafanya haraka kumletea hapa hapa tunayo yataka kwa tumtakaye. Kisha tumemwekea Jahannamu; ataingia humo hali ya kuwa ni mwenye kulaumiwa na kufurushwa * Na anaye itaka Akhera, na akazifanyia juhudi a'mali zake, naye ni Muumini, basi hao juhudi yao itakuwa ni ya kushukuriwa” [Al-Isra’: 18-19].

Kwa kutamatisha, tunawakumbusha Waislamu kusherehekea Idd hii kwa namna inayomridhisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kueneza furaha katika nyumba zao, mitaa na miji yao na kufurahia siku zijazo, na kushiriki katika kazi yenye malengo na jitihada za dhati pamoja na Hizb. ut Tahrir kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.

Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar, La illaha illa Allah, Allahu Akbar, Allahu Akbar, Allahu Akbar Wa Lillahil Hamd

Idd Mubarak.

Mhandisi Salah Eddine Adada

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari

ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu