Tusipozisukuma Dola za Kikafiri Katika Mwelekeo Sahihi, Zitatusukuma Katika Mwelekeo wa Makosa!
- Imepeperushwa katika Afghanistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Katika mkutano na waandishi wa habari mnamo Septemba 14, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Ned Price alisema: “Tumeeleza waziwazi kwamba hatuangalii kutambuliwa. Tunaangalia ni wapi - yalipo maslahi yetu, ushirikiano wa kivitendo pekee, ushirikiano wa kivitendo ambao tunatumai utaisukuma Taliban katika mwelekeo sahihi, na tutaendelea kushirikiana nao kwa msingi huo hadi tuone maboresho katika maeneo ambayo tunajali zaidi kuyahusu.”