Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan

H.  27 Dhu al-Hijjah 1443 Na: Afg. 1443 H / 15
M.  Jumanne, 26 Julai 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir ni Mwiba Machoni mwa Masekula na Susu la Matumaini kwa Waislamu!

(Imetafsiriwa)

Kufuatia kuporomoka kwa Jamhuri na kumalizika uvamizi wa kimabavu, masekula walipatwa na mshtuko wa ubongo kwani tayari walikuwa wamekata uhusiano wao na Mwenyezi Mungu (swt) kwa kujikinga mikononi mwa dola za Kimagharibi; hata hivyo cha kushangaza, nchi za Magharibi hazikufikia mahitaji yao wala hazikuweza kulinda mfumo, mamlaka na madaraka watakao wao. Ndiyo maana mabaki ya uvamizi huo kwa kawaida huona jinamizi usiku na kueneza uvumi siku inayofuata. Mojawapo ya sehemu ambazo kwazo hisia hizo za uwongo na batili huchapishwa ni Gazeti la Hasht-e-Subh, ambalo kwa mara nyingine tena limeonyesha chuki dhidi ya Hizb ut Tahrir kwa kuchapisha tahariri yake ya Jumatatu chini ya kichwa “Hizb ut Tahrir Yazidi Kukoleza Misimamo mikali nchini Afghanistan.”

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Afghanistan pamoja na kukataa vikali msimamo mchafu wa Gazeti la Hasht-e-Subh, inalichukulia shirika hili kuwa liko maili nyingi mbali na ukweli halisi uwanjani kwani madai yao yamejaa migongano iliyo na habari na siasa za udanganyifu. Wakati huo huo gazeti hili linajaribu kuvihusisha vyama vya Kiislamu na siasa za Kimagharibi ilhali wao wenyewe wameangukia mikononi mwa Magharibi kwa nyoyo pamoja na akili zao. Masekula, mufakkirina na taasisi zao walikuwa wakifanya kazi kwa uchangamfu chini ya mwavuli wa uvamizi na ukoloni wa Kimagharibi. Wakiibuka kama uyoga, waliungwa mkono kwa nguvu na uvamizi wa Kimagharibi kwani walipewa nyadhifa na huduma za kiserikali na pia walikuzwa na kulishwa kama watoto wachanga na wavamizi hao.

Hizb ut Tahrir ni chama cha kifikra na kisiasa ambacho lengo na njia yake ni Uislamu na hakuna chochote ndani yake isipokuwa Uislamu. Hivyo basi, masekula (waliochoshwa na mfumo wa Kiislamu) hawana haki ya kusema na/au kutoa maoni kuhusu Uislamu na vyama vya Kiislamu. Mbali na hayo, wale ambao hawana ufahamu wa kina wa Uislamu; wale ambao shakhsiya yao haikujengwa juu ya Uislamu na imani ya Kiislamu, na wale ambao daima huona mambo kwa mtazamo wa Kimagharibi, hawapaswi kuwa Polisi wa Trafiki kwa Waislamu na vyama vya Kiislamu. Kwa upande mwingine, watu hawa, waigaji wa maoni ya kisekula, hawajui vizuri sana falsafa yao wenyewe [Usekula]; ndio maana, wanatokea kumnasibisha Machiavelli na makundi ya Kiislamu. Wakati Machiavelli alikuwa baba wa madhehebu ya Usekula kwani ulimwengu wa Kirasimali hutekeleza kanuni zake katika siasa zao. Kwa hivyo, Hasht-e-Subh na mithili ya wale wanaotokea kueneza habari potofu, uongo na propaganda kila siku wanapaswa kutambua kwamba wao wenyewe ni wanafunzi watiifu wa Machiavelli ambapo Machiavelli alikuwa mfuasi mkuu wa Shetani!

Hii ni kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwamba Muumini anaweza kuwa mwoga na bakhili, lakini hawezi kuwa muongo. Wanafikra walioutoa Uislamu katika anwani ya Uislamu katika kipindi cha miaka 20 iliyopita ya Jamhuri, wanajulikana kuwa waongo mbele ya umma kwani hata leo wako mstari wa mbele katika kueneza uwongo, propaganda na kuchochea maasi. Kwa miaka mingi, wameng’ang’ana kuubakisha hai uvamizi na kuingizia maadili ya Kimagharibi kitaasisi kwani bado wangali wanashughulika na hilo hadi leo. Walisema uwongo kwamba Hizb ut Tahrir ilimuomba Gaddafi Nussrah; hata hivyo, ni kweli kwamba kundi la wanachama wa Hizb ut Tahrir walikwenda kwa Gaddafi ili kumwongoza kutafuta wema kwani alitokea kuikataa Sunnah - kama ambavyo masekula na wanafikra wamekuwa wakifanya siku hizi, wakikashifu mfumo wa kisiasa wa Kiislamu kwa miaka mingi na hata kutokubaliana na machimbuko ya Shariah, Sunnah ya Mtume (saw) na Maswahaba zake, na kumzulia Mwenyezi Mungu (swt) uwongo mkubwa kwa kutangaza kuwa Uislamu sio dini ya kisiasa na mfumo wa maisha:

 (وَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ افْتَرَى عَلَى اللَّـهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِآيَاتِهِ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الظَّالِمُونَ)

“Na nani dhaalimu zaidi kuliko anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na akazikanusha Ishara zake? Hakika madhaalimu hawafanikiwi.” [Al-Anaam: 21]. Tunaelekea kwenye ahadi za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwamba Uislamu utaregea tena katika maisha na siasa zetu. Wale wanaowaita Waislamu kuwa ni wajinga wanapaswa kujua kwamba leo Jamhuri imeanguka, uvamizi umemalizika na ulimwengu wa Kimagharibi uko katika mporomoko, na tunawapa bishara njema wanaadamu kwamba Khilafah Rashida itasimamishwa tena na wanadamu wote wataokolewa kutokana na ukatili wa Usekula hata kama Masekula hawataki litokee.

 (فَسَتُبْصِرُ وَيُبْصِرُونَ * بِأَيِّيكُمُ الْمَفْتُونُ) “Karibu utaona, na wao wataona. Ni nani kati yenu aliye pandwa na wazimu.” [Al-Qalam 5-6].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Afghanistan
Address & Website
Tel: 
http://hizb-afghanistan.org/
E-Mail: info@hizb-afghanistan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu