Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir/ Wilayah Pakistan: Mapenzi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)

Wale Wanaompenda Kikweli Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ni lazima Wasimamishe Tena Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo ndiyo itakayolinda Heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

Imesimuliwa kuwa Anas (ra) alisema kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«لَا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ مَالِهِ وَأَهْلِهِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ»

“Hatoamini mmoja wenu mpaka anipende mimi zaidi kuliko mali yake, jamaa zake na watu wote kwa jumla.” [An-Nisa’a].

Kama ufafanuzi wa mapenzi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), Imam Abu Sulayman al-Khattabi

 (الْإِمَامُ أَبُو سُلَيْمَانَ الْخَطَّابِيُّ) ameeleza kuwa فَمَعْنَاهُ لَا تَصْدُقُ فِي حُبِّي حَتَّى تُفْنِيَ فِي طَاعَتِي نَفْسَكَ وَتُؤْثِرَ رِضَايَ عَلَى هَوَاكَ وَإِنْ كَانَ فِيهِ هَلَاكُكَ  “Maana yake ni kuwa: 'Hamtakuwa wakweli katika mapenzi yenu kwangu mpaka mjitolee nafsi zenu katika kunitii mimi, mpaka mchague radhi zangu badala ya matamanio yenu hata kama itawapelekea katika kifo’”.

Hata katika zama dhaifu kabisa za Khilafah, mapenzi na utiifu wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) yalidhihirika katika matendo ya Khalifah wa Kiuthmani, Abdul Hameed II, wakati Uingereza na Ufaransa, dola kuu za ulimwengu za wakati huo, zilipopanga kushambulia heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

Tishio tu la Jihad la vikosi vya jeshi la Khilafah lilitosha kuwatisha mashetani wa makruseda ambao walirudi nyuma, wasiendelee tena na mpanga huo mpaka baada ya kuvunjwa Khilafah.

Leo, ni juu ya kila mmoja wetu kuwa mkweli katika mapenzi yetu kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na utiifu kwake (saw), kwa kujitahidi kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume, ambayo itaikomesha mikono na ndimi ovu.

#KhilafahOnTheMethodOfProphethood.

Jumapili, 24 Rabi-ul Awwal 1443 H - 17 Oktoba 2021 M

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu