Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

[وَإِنِ ‌اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]
Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Surah Al-Anfaal 8:72]
Al-Aqsa Imezingirwa na Mashambulizi… Hivyo Ulinzi wa Waongofu Utafanya Mapinduzi Lini?!
(Imetafsiriwa)

Ewe Mwenyezi Mungu, Ewe Mwenyezi Mungu, kutoka kwenye Msikiti wako wa Mbali, enyi Waislamu... Ewe Mwenyezi Mungu, Ewe Mwenyezi Mungu, kutoka kwa sehemu ya Isra’a ya Mtume wako (saw)... Enyi Umma wa Muhammad (saw)!

Uko wapi ulinzi wa wanaume?... Je, bidii ya waumini iko wapi?

Je, sio wakati wa Takbira za Al-Masjid Al-Aqsa, kuzigonga nyoyo za majeshi ya Kiislamu?!

Je, sio wakati wa vilio vya wanawake watukufu wa Ardhi Tukufu, kutikisa nguzo za wakuu wa majeshi katika majeshi ya Kiislamu?

Tujibuni, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt), lini mutataharaki?! Mutaamka lini?! Je, ni lini shauku ya Uislamu na ulinzi wa waumini utalipuka ndani yenu?!

Ikiwa Al-Masjid Al-Aqsa haiamshi ari yenu, basi ni nini kitakachoweza kuchochea shauku yenu?!

Enyi Jeshi la Misri: Je! Hakuna miongoni mwenu mwanamume mithili ya al-Zahir Rukn al-Din Baybars au Salah al-Din, atakayefufua historia ya ufunguzi wa mujahidina?

Enyi Vikosi Mahiri vya Jeshi la Jordan: Je, ari ya wanaume haikusukumini kwenye ulinzi wa wanawake wasafi, wanaonyanyaswa katika uwanja wa Al-Masjid Al-Aqsa?

Je, jeshi la Uturuki lina nini, ambalo limefungwa pingu kutokana na kuinusuru Al-Masjid Al-Aqsa, lakini liko huru nchini Syria?!

Je, Jeshi la Pakistan lina nini, kwamba limefungwa pingu kutokana na kuinusuru sehemu ya Isra'a ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), lakini liko huru kupigana na Waislamu?!

Je, jeshi la Hijaz lina nini kwamba limefungwa pingu kutokana na kukinusuru Qiblah cha kwanza kati ya vibla viwili, na eneo tukufu la tatu katika ya maeneo matukufu matatu, lakini liko huru kuwaua Waislamu nchini Yemen?!

Enyi Majeshi ya Waislamu:

Sisi katika ardhi iliyobarikiwa hatutamzungumzisha yeyote ila nyinyi, kwani nyinyi mnao uwezo wa kupakomboa Mahali pa Isra’a ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), basi je hamfurukuti?

Sisi katika Ardhi Iliyobarikiwa tunaomba msaada wenu ili kuunusuru Uislamu, na hatutaomba msaada kwa mtu mwengine yeyote, kwa sababu nyinyi muna uwezo wa hilo, je nyinyi sio wakujibu?

Enyi Waislamu: Wito wetu kwenu kutoka katika Ardhi Iliyobarikiwa ni kuwahimiza watoto wenu katika majeshi kuitikia wito wa Mwenyezi Mungu (swt). Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَإِنِ ‌اسْتَنْصَرُوكُمْ فِي الدِّينِ فَعَلَيْكُمُ النَّصْرُ]

Lakini wakiomba msaada kwenu katika Dini, basi ni juu yenu kuwasaidia.” [Surah Al-Anfaal 8:72]

Wito wetu kwenu ni kuwalilia watoto wenu na ndugu zenu katika jeshi ili waitikie wito wa Mwenyezi Mungu (swt),

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ ‌انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]

“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache * Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [Surah At-Tawbah 9:38-39].

Enyi Waislamu: Kauli za kukemea na kushutumu zinazotoka kwa watawala duni Ruwaibidhah, au ile miito wanayotoa kwa ajili ya kufanya vikao na mikutano, au maombi yao ya kufedhehesha kwa taasisi za kimataifa, lazima mukutane nayo kwa wito wa kuwapindua na kuuondolea Ummah maovu yao. Watawala hawa ndio kichwa cha uovu na chanzo cha maradhi. Wao ndio walinzi halisi wa umbile la Kiyahudi. Wao ndio wanaousambaratisha Ummah na kuzuia umoja wake. Wanaipiga vita Dini yake na hao ndio wanaowafunga minyororo watoto wake kutokana na jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt).

Ukombozi wa Al-Masjid Al-Aqsa unaweza kupatikana tu kupitia kubomoa viti vya utawala vya khiyana na kuukomboa Ummah kutokana na maovu yao.

Ndio, kukombolewa kwa Msikiti wa Al-Aqsa ni kupitia kuyakomboa tu majeshi ya Kiislamu kutokana na udhalima wa vibaraka, wanaoyafunga minyororo kutokana na kuunusuru Uislamu, Al-Masjid Al-Aqsa na Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt).

Enyi Waislamu:

Umbile hili lililolaaniwa ni umbile dhaifu. Wanajeshi wake hawasimami imara katika vita, kama Mwenyezi Mungu (swt) alivyowasifia, watu wao wana tamaa ya maisha. Hivyo basi, ukombozi wa Al-Masjid Al-Aqsa uko karibu zaidi na nyinyi kuliko munavyofikiri. Tuko kwenye miadi na ushindi wa Mwenyezi Mungu (swt). Basi yaunganisheni mambo yenu na muwe kama moyo wa mtu mmoja katika kutafuta msaada wa watoto wenu na ndugu zenu katika vita. Majeshi yanatakiwa kutekeleza wajibu wao wa kuunusuru Uislamu na Al-Masjid Al-Aqsa, kwa sababu wana uwezo wa kuunusuru Uislamu na kuukomboa Al-Masjid Al-Aqsa. Kila mazungumzo yaliyo mbali na hili, ni mazungumzo yaliyo mbali na haki, na yaliyo mbali na amri ya Mwenyezi Mungu (swt) na amri ya Mtume wake (saw).

Na sisi katika Hizb ut Tahrir tunauhutubia Umma wa Kiislamu na majeshi yake kwa yale aliyowaamrisha Mwenyezi Mungu (swt) ya kuunusuru Uislamu. Tunawahutubia kwa Maneno ya Mwenyezi Mungu (swt),

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِنْ ‌تَنْصُرُوا اللَّهَ يَنْصُرْكُمْ وَيُثَبِّتْ أَقْدَامَكُمْ]

Enyi mlio amini! Mkimnusuru Mwenyezi Mungu naye atakunusuruni na ataithibitisha miguu yenu.” [Surah Muhammad 47:7]

Tunaomba nusra kutoka kwa Umma wa Kiislamu, na majeshi yake, ili kusimamisha Khilafah na kuikomboa Al-Quds, kwani huu ndio ukweli. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

فَمَاذَا ‌بَعْدَ ‌الْحَقِّ إِلَّا الضَّلَالُ﴿

Na kipo kitu gani baada ya haki, isipokuwa upotovu tu?” [Yunus 10:32]. Na wallahi hakika hii ndio njia ya Mwenye nguvu, Mwenye kushukuriwa,

[وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيماً فَاتَّبِعُوهُ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ ‌فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَنْ سَبِيلِهِ ذَلِكُمْ وَصَّاكُمْ بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ]

Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu.[Surah Al-Anaam 6:153]

Ewe Mwenyezi Mungu, tufikishie kheri hii kutoka kwetu, na ufungue vifua vya Waislamu kwa dalili za wahyi na hekima iliyokuja ndani yake. Na utujaalie kutoka Kwako mamlaka yenye kutunusuru.

Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu (swt), Mola wa Walimwengu wote.

  

H. 15 Ramadan 1444
M. : Alhamisi, 06 Aprili 2023

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu