Jumatano, 04 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hotuba katika Msikiti Uliobarikiwa wa Al-Aqsa kufuatia Upandishaji Bendera na Kunajisiwa kwa Msikiti wale ambao wameibua Hasira [Yenu]  
(Imetafsiriwa)

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu ambaye mkononi mwake imo izza na ushindi, na rehema na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake, na maswahaba zake, na waliomfuata.

Enyi Waislamu... Enyi Majeshi ya Waislamu...

Hakika, umefika wakati umewadia wa nyinyi kumnusuru Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw)... hakika wakati umefika kwenu kuchukua nyadhifa zenu za heshima zinazomridhisha Mola wenu Mlezi.

Je, hamuyaoni makundi ya walowezi yakiinajisi Al-Aqsa, Mahali pa Safari ya Usiku ya Israa ya Mtume wenu (saw)?

Je, hamuyasikii makundi ya walowezi yakimtukana Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) katika nyua za Al-Aqsa?

Je, hamujafahamishwa kwamba wamezuia Adhaan ya swala katika Al-Masjid Al-Aqsa wakati wa uchafuzi wao?

Je, hamujaziona bendera za wale ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewakasirikia, zikiinuliwa katika Al-Masjid Al-Aqsa?! Basi ni lini ulinzi wa Kiislamu utazuka katika nafsi zenu?! Lini mtaasi katika kumnusuru Mwenyezi Mungu na Mtume wake?

Tuambieni, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ni lini fahari italipuka kutoka pande zenu?!

Je, kuna madhara yoyote kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) endapo mtakuwa na jicho la itikadi kali?!

Enyi Wanajeshi wa Misri, ash-Sham, Jordan, Pakistan na Uturuki, je nafsi zenu hazitamani Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa ushindi?!

Kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) tunakulinganieni kwa wito wa Mwenyezi Mungu (swt),

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ ‌انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَابًا أَلِيمًا وَيَسْتَبْدِلْ قَوْمًا غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئًا وَاللَّهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]

Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache (38) Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu. (39)” [Surah At-Tawba 9:38-39].

Enyi Waislamu:

Heshima yetu imedhalilishwa na wale ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewakasirikia, na wameichafua Dini yetu, Mtume wetu (saw), heshima yetu, na wakatutoa Mahali pa Safari ya Usiku ya Isra'a ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)... Kwa hiyo munasubiri nini? Tujibuni, kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, ni kipi kitakachowasha ulinzi ndani yenu, ili tuweze kukuhutubieni kwacho?

Watawala makhaini Rubaybidah wanakusanyika katika ardhi ya Hijaz, ardhi takatifu zaidi kwa Waislamu, ili kuthibitisha mfarakano wenu, kwa ajili ya kudhalilika kwenu na kula njama kwao na adui yenu kukuueni na kupora mali zenu. Hivyo mnafanya nini? Je, mtakubali udhalilifu na fedheha chini ya utawala wao?

Enyi Waislamu... Enyi Maafisa, Makamanda na Wakuu:

Kutoka Al-Masjid Al-Aqsa, tunakulinganieni kumnusuru Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw), je, mtaitikia?

Kutoka kwa Al-Masjid Al-Aqsa, tunaomba Nusrah yenu ili kusimamisha Khilafah na kukomboa Mahali pa Isra'a ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw).

Kutoka Msikiti wa Al-Aqsa, tunaomba ulinzi wa Uislamu ndani yenu, ili atokee kiongozi muongofu kutoka kwenu, ambaye anajadidisha wasifu wa mujahidina, washindi, Salah al-Din na Khalid ibn al-Walid (ra).

Nusra kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na nusra kwa Msikiti wa Al-Aqsa ni heshima kubwa ambayo inaweza kupatikana tu kwa yule anayeibeba nafsi yake kama sadaka kwenye kiganja cha mkono wake. Ni kheri kwake kujitolea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw). Nusra kwa Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume wake (saw) na ukombozi wa Msikiti wa Al-Aqsa ni heshima kubwa ambayo wazembe wala waliodhalilishwa wa tawala hizi hawawezi kamwe kuipata. Ni heshima kubwa ambayo inaweza kupatikana tu kwa waheshimiwa, waongofu, ambao hawaogopi lawama ya mwenye kulaumu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt).

Huu ni wito wetu kwenu, na tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) akujulisheni wito wetu na afungue nyoyo zenu kwake Yeye, ili tukutane nanyi katika viwanja vya Al-Masjid Al-Aqsa, tukipiga takbira “Allahu Akbar” na kutangaza wito uleule wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alipoingia Makka.

[وَقُلْ جَاءَ الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا]

Na sema: Kweli imefika, na uwongo umetoweka. Hakika uwongo lazima utoweke! [Surah Al-Isra’a 17:81].

Walhamdulilah Rabb Alameen

H. 29 Shawwal 1444
M. : Ijumaa, 19 Mei 2023

Hizb-ut-Tahrir
Ardhi ya Baraka-Palestina

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu