Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali:
Fi’l ul-Amr (Kitenzi cha Kuamrisha)
Kwa: Abdulrahman al-Ziuod
(Imetafsiriwa)

Swali

Kaka yangu mpendwa, Mwenyezi Mungu akuhifadhi na akulinde, na akusaidie pamoja na waumini wenye nguvu na ikhlasi, na Mwenyezi Mungu akusaidie katika jukumu lako zito, na atujumuishe karibuni mikono yetu iushike mkono wako, kutoa ahadi ya utiifu kuwa tutasikiza na kutii kila lenye kutufurahisha na kutuchukiza. 

Assalamu Alaikum wa Rahmatullahi wa Barakatuh,

Nilipokuwa najitayarisha katika Shakhsiya ya Kiislamu Juzuu ya 3, katika mada ya kitenzi (al-Fi’l), ukurasa wa 168 nakala ya kielektroniki, niligundua nasi hii (Ama kitenzi cha kuamrisha (Fi’l ul-Amr) ni kile ambacho herufi ya muundo wa kitenzi cha muda uliopo sasa imeondolewa kutokana nacho.) 

Swali ni: ikiwa herufu ya muundo wa kitenzi cha muda uliopo sasa itaondolewa katika kitenzi cha muda uliopo sasa "yaf'alu", je hakigeuki kuwa kitenzi kilicho pita fa'ala? Yaani, je, si kitenzi cha kuamrisha. Je, kuna makosa ya kisarufi katika neno letu? Mwenyezi Mungu akubariki, na uwe katika uangalizi wa Mwenyezi Mungu.

Jibu

Wa Alaikum Assalam wa Rahmatullahi wa Barakatuh,

Mwenyezi Mungu akubariki katika dua zako njema, na namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu mafanikio na usahihi kwako na kwetu.

Taarifa katika kitabu cha Shakhsiya ya Kiislamu Juzuu ya 3 juu ya Fi’l ul-Amr: (Ama Fi’l ul-Amr (kitenzi cha kuamrisha), ni kile ambacho herufi ya muundo wa kitenzi cha sasa imeondolewa kutokana nacho pekee). Hili linapatikana katika vitabu vya Usul (Misingi ya Fiqh), kwa mfano imekuja katika kitabu cha al-Ihkam fi Usul al-Ahkam cha Al-Amadi (1/58):

(Kitenzi (Al-fi’l) ni kile kinacho ashiria tukio (Hadath) linalo husiana na wakati wa kutokea kwake, na tukio ni shina (Masdar) ambalo ni nomino kitenzi, na wakati unaotukia kwake ni uliopita, ulioko na ujao, na vimegawanyika kwa mujibu wa kigawanyo cha wakati, hivyo neno amesimama (قام) na ameketi (قعد) ni mifano ya vitendo vilivyo pita.

Kitenzi cha muda uliopo na kitakacho kuja vina maneno yayo hayo na huitwa kitenzi cha muda uliopo (Mudhari'), kinacho anza na moja ya herufi tangulizi nne iliyo ambatanishwa mwanzoni mwa neno: Hamza (أ), Taa (تـ), Nun (نـ), and Yaa (يـ), kama kusema: ninasimama (أقوم), unasimama (mwanamume) (تقوم), tunasimama (نقوم). Kitenzi kijacho huvuliwa kutokana na kitenzi cha muda uliopo kwa kuongeza tu herufi (سـَ) au (سوف) kabla ya kitenzi katika muundo wa kilichoko kama kusema atasimama: سيقوم /سوف يقوم)). Ama kitenzi cha kuamrisha (Fi’l ul-Amr) ni kile ambacho herufi ya muundo wa kitenzi cha muda uliopo sasa imeondolewa pekee kutokana nacho, kama kusema: anasimama (mwanamume) (يقوم) na simama (mwanamume) (قم) na kadhalika) Mwisho wa nukuu.   

Kwa mfano, imekuja katika usherehesho wa al-Uthaymeen juu ya kitabu cha al-Alfiyah cha Ibn Malik (3/11, katika ash-Shamilah uwekaji nambari kwa njia ya otamatiki):

[Mwandishi (Mwenyezi Mungu amrehemu) asema: "Vitenzi katika muundo wa amri na uliopita havibadiliki (Mabni), na vitenzi  vya muundo wa sasa ni vitendo vinavyo badilika mwisho wake kutokana na irabu (Mu'rabah) ikiwa havikuambatanishwa moja kwa moja na 'Nun' ya kusisitiza (Nun al-Tawkeed) au 'Nun' ya kike (Nun an-Niswa) kama يرعن من فتن. Kisha asema: وفعل أمر ومضي بنيا) na kitenzi cha kuamrisha na kitenzi kilicho pita havibadiliki mwisho wake (Buniyaa), na Alif (ا) iliyo katika neno (بنيا) ni kwa muundo wa idadi ya mbili kwa sababu inaashiria mbili.

Hivyo basi, kitenzi cha kuamrisha hakibadiliki (Mabni), na imesemwa: ni Mu'raba (maneno ambayo hubadiliki mwisho wake kutokana na I'rab), na sahihi ni Mabni, na kimewekewa irabu ya Jazm katika kitenzi chake kilichopo. Hivyo, ikiwa Jazm katika kitenzi chake kilichopo imeashiriwa kwa alama ya Sukun, basi (kitenzi chake cha kuamrisha) huwekewa Sukun, na ikiwa Jazm ya kitenzi chake kilichopo imefichika na imeashiriwa kwa herufi ya illa au Nun, basi (kitenzi chake cha kuamrisha) pia Jazm yake hufichika na huashiriwa kwa herufi ya illa au Nun. Hivyo basi, tunasema: ikiwa unataka kuunda kitenzi cha kuamrisha, basi chukua kitenzi chake kilicho katika muundo wa sasa yaani hali ya Jazm, na kisha ondoa herufi ya muundo wa sasa kutokana nacho na alama ya Jazm.] Mwisho.

Kuonyesha hili kwa msingi wa utafiti wa nahau kutoka katika machimbuko yake, tunasema, na Mwenyezi Mungu ni mwongozi wa mafanikio:

1- Kitenzi cha kuamrisha huchukuliwa mpangilio wake kutoka katika kitenzi cha muda uliopo baada ya kuondoa herufi ya muundo wa muda uliopo, lakini kwa sababu kitenzi cha kuamrisha kiko katika hali ya Jazm, mpangilio wake wa neno huchukuliwa kutoka katika kitenzi cha muda uliopo ambacho kiko katika hali ya Jazm baada ya kuondolewa kwa herufi ya muundo wa muda uliopo na bila shaka baada ya kuondolewa herufi ya Jazm kwa sababu si sehemu ya kitenzi hicho. Hivyo basi, ikiwa unataka kuvua kitenzi cha kuamrisha kutoka katika kitenzi cha muda uliopo, kwanza iweke herufi ya Jazm kama "لم" katika kitenzi cha muda uliopo katika hali ya Jazm na kisha ondoa herufi "لم" yaani, ubakishe muundo wa kitenzi cha muda uliopo bila ya herufi ya Jazm, na kisha ondoa herufi ya kitenzi cha muda uliopo katika hali ya Jazm, na kitenzi cha kuamrisha kitajitokeza kwako.

2-Kwa mfano, kitenzi "anaogopa (mwanamume) "يخاف", inakuwa "hakuogopa (mwanamume)" "لم يخَفْ" baada ya kuingizwa “لم”, na kwa kuiondoa “لم”, inakuwa "يخاف" na kwa kuifuta herufi ya muundo wa muda uliopo "ي" ambayo iko mwanzoni mwa kitenzi inakuwa "خَفْ" "ogopa" ambacho ni kitenzi cha kuamrisha cha kitenzi "خاف" “anaogopa (mwanamume)”; hivyo hivyo yaweza kufanywa kwa vitenzi (analala, anasimama, anasema, anazuru …)

3- Kwa mfano, kitenzi "يفي" "anatimiza” inakuwa "لم يفِ" "hakutimiza", baada ya kuingiza herufi ya “لم”, na kwa kuondoa “لم” inakuwa "يفِ", na kwa kufuta herufi ya muda uliopo "ي" ambayo iko mwanzoni mwa kitenzi inakuwa "فِ" "timiza", ambacho ni kitenzi cha kuamrisha cha kitenzi "وفى" “ametimiza”. Hivyo hivo yaweza kufanywa kwa vitenzi (amediriki, amezuia, ameona …)     

4-Kwa mfano, kitenzi "يضرب" "anapiga" inakuwa "لم يضْرِبْ" "hakupiga", baada ya kuingiza “لم”, na kwa kuiondoa “لم” inakuwa "يضْرِبْ" "anapiga", na kwa kufuta herufi ya muda uliopo "ي" ambayo iko mwanzoni mwa kitenzi inakuwa "ضْرِبْ", lakini kwa kuwa herufi yake ya kwanza ambayo ni الضاد ina sukun, na haiwezekani kuanza kwa kutamka herufi iliyo na sukun isipokwa kwa hamzat ul-wasl au Hamza yenye kuunganisha, basi itakuwa "اضْرِبْ" "piga", ambacho ni kitenzi cha kuamrisha cha kitenzi "anapiga". Hivyo hivyo yaweza kufanywa kwa vitenzi vifuatavyo: (amefanya kazi, ameita, amejenga …).

5- Tamati ni kuwa ikiwa herufi ya muda uliopo kutoka katika kitenzi cha muda uliopo ambacho kiko katika hali ya Jazm itaondolewa, kitenzi kinacho patikana ni kitenzi cha kuamrisha (Fi’l ul-Amr) na sio kitenzi cha muda uliopita, na hivyo basi yale yaliyo elezwa katika Shakhsiya ya Kiislamu Juzuu ya 3 ni sahihi kwa mujibu wa maelezo ya juu, na hakuna "makosa ya kisarufi" yoyote ndani yake.

Nataraji jambo hili liko wazi sasa.

Ndugu yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

14 Shawwal 1440 H

17/06/2019 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu