Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali

Tofauti baina ya Upokezi wa Usomaji wa Aya za Qur'an (Tilawa) na Upokezi wa Rasimu ya Aya za Mwenyezi Mungu Kwetu Sisi

Kwa: Bakr Ash-Shami

(Imetafsiriwa)

Swali:

Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah

Tafadhali waweza kunifafanulia mimi Hadith hii, kwa sababu nimechanganyikiwa, ambapo sikupambanukiwa baada ya kuregelea kauli za wanazuoni:

قَالَ ابْنُ شِهَابٍ وَأَخْبَرَنِي خَارِجَةُ بْنُ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ سَمِعَ زَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ قَالَ فَقَدْتُ آيَةً مِنْ الْأَحْزَابِ حِينَ نَسَخْنَا الْمُصْحَفَ قَدْ كُنْتُ أَسْمَعُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ بِهَا فَالْتَمَسْنَاهَا فَوَجَدْنَاهَا مَعَ خُزَيْمَةَ بْنِ ثَابِتٍ الْأَنْصَارِيِّ [مِنْ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ] ، فَأَلْحَقْنَاهَا فِي سُورَتِهَا فِي الْمُصْحَف

“Ibn Shihab asema alinijuza mimi Kharijah ibn Zain ibn Thabit kuwa alimsikia Zaid bin Thabit akisema, nilipoteza Ayah katika Surat Ahzab pindi tulipo nakili msahafu ambayo nilikuwa nikimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu () akiisoma. Basi tukaitafuta na tukaipata iko na Khuzayma bin Thabit Al-Answari. (Aya yenyewe ilikuwa): "Miongoni mwa Waumini kuna wanaume waliosadikisha yale waliyo muahidi Mwenyezi Mungu juu yake." [Al-Ahzab: 23] basi tukaikutanisha na surah yake katika msahafu”

Bado ningali sijafahamu vipi maswahaba waliikubali kutoka kwake, ingawa alikuwa ni mtu mmoja pekee, na hali hili halifidii Tawatur (kutegemewa kusoshaka). Na ikiwa tunatambua kuwa ushahidi wake ni sawa na ushahidi wa wawili, bado itakuwa hivyo hivyo, kuwa haifikii Tawatur!

Allah akubariki Sheikh wetu

Jibu:

Wa Alaikum Assalam Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Inaonekana kana kwamba kuchanganyikiwa kwako ni baina ya upokezi wa usomaji wa aya za Qur'an (Tilawa) kwetu sisi kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), na upokezi wa mpangilio wa uandishi, rasimu ya aya za Mwenyezi Mungu, kama zilivyo andikwa mbele ya Mtume (saw). Upokezi wa usomaji wa aya ni kwa njia ya Tawatur, kupitia vikundi vya maswahaba, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), hadi itakufikia sisi kwa njia ya Tawatur na itahifadhiwa kwa hifadhi ya Mwenyezi Mungu na tawfiq yake mpaka Siku ya Kiyama. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ ]

“Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.” [Al-Hijr: 9]

Ama kuhusu upokezi wa rasimu ya aya, maswahaba hawakukubali kuziandika aya kwa kutegemea hifdhi yao pekee, bali walitaka kukusanya uandishi wao, uliokuwa umeandikwa mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt). Ingekuwa imetosheleza kuzikusanya nyaraka zilizo andikwa (Suhuf) zilizokuwa katika milki ya maswahaba, lakini wao Mwenyezi Mungu awe radhi nao walijitolea kupata mashahidi wawili ili kuthibitisha usahihi wa kila ukurasa ulio andikwa mbele ya Mtume (saw) kama tahadhari ya ziada, na hii ni tawfiq (mafanikio) kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) ili kukihifadhi Kitabu Chake kutokana na batili.

 [لَا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِنْ بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ تَنْزِيلٌ مِنْ حَكِيمٍ حَمِيدٍ ]

“Hautakifikia upotovu mbele yake wala nyuma yake. Kimeteremshwa na Mwenye hikima, Msifiwa.” [Fussilat: 42]

Hii ndio kadhia, na ufuatao ni ufafanuzi wake:

Kwanza: Mada ya ukusanyaji Qur'an:

Tumeifafanua mada hii ya ukusanyaji Qur'an katika kitabu, Shakhsiya ya Kiislamu Sehemu ya Kwanza, mlango wa "Ukusanyaji Qur'an", kama pia tulivyo fanya katika kitabu "Tayseer Al-Wusul ila Al-Usul" katika mlango "Uteremshwaji Qur'an na Rasimu Yake" na "Ukusanyaji Qur'an". Muulizaji aweza kurudi katika vitabu hivi viwili vilivyo tajwa juu kwa maelezo zaidi ya jambo hili na dalili zake za kina… Nitakunukulia baadhi ya yaliyo elezwa katika vitabu vyetu ili kukusaidia kuielewa kadhia hii kwa usahihi, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt):

1- Nakunukulia kutoka katika kitabu changu, "Tayseer Al-Wusul Ila Al-Usul," katika mlango wa “Ukusanyaji Quran”:

(... Kwa sababu ya vita dhidi ya walio ritadi Abu Bakr, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, alihofia kuwa idadi kubwa ya walio hifadhi Qur'an tukufu huenda wakauwawa (kupata shahada), wao ndio waliokuwa wawehifadhi aya zake kwa mpangilio sahihi katika Surah zake, aliagiza ukusanyaji wa aya zilizo andika kwa kila Surah mahali pamoja na kupangiliwa kwa mpangilio ulio idhinishwa na Mtume (saw). Surah zilipangiliwa kwa mtiririko ulio andikwa katika vipande vilivyo kusanywa baada ya kuthibitishwa kuwa ziliandikwa mbele ya Mtume (saw) na kulikuwepo na sharti la ushahidi wa maswahaba wawili katika kila kipande kilicho andikwa; ili kuthibitisha kuwa kiliandikwa mbele ya Mtume (saw), na wao (maswahaba) hawakuridhika tu na kuwiana kwa aya zilizo andikwa na zilizo hifadhiwa pekee. Zingatia kuwa kila aya ilikuwa imehifadhiwa na kikundi cha maswahaba kwa njia ya tawatur.

Hivyo walipopata kuwa aya za mwisho za Surat At-Tawba ziliandikwa na Khuzayma pekee, na kwamba ni Khuzayma (ra) pekee aliye thibitisha kuwa ziliandikwa mbele ya Mtume (saw) waliacha kuzikusanya hadi walipopata ushahidi kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alitabanni kuwa ushahidi wa Khuzayma ni sawa na ushahidi wa Waislamu wawili waadilifu, hapo ndipo walikikusanya kipande hicho kilicho andikwa; ambacho Khuzayma alikitolea ushahidi. Zingatia kuwa wao walikuwa wameihifadhi aya hiyo pasi na shaka yoyote, lakini hilo lilikuwa kwa ajili ya uthibitisho wa ziada kwao, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, kwa sababu walitaka kuzikusanya nyaraka (suhuf) zilizo andikwa mbele ya Mtume (saw) na sio kuziandika kutokana na hifdhi.  

Hivyo basi, ukusanyaji wa Abu Bakr al-Siddiq, ulikuwa ni ukusanyaji wa nyaraka zilizo kuwa na aya zilizo andikwa na kupangiliwa katika Surah zake kama ilivyo idhinishwa na Mtume (saw) yaani kuziweka nyaraka za aya za kila Surah kwa mpangilio moja nyuma ya nyengine katika sehemu moja kwa Surah zote za Qur'an) Mwisho.

2- Na nakunukulia kutoka katika Shakhsiya ya Kiislamu Sehemu ya Kwaza baada ya ukusanyaji wa Abu Bakr wa nyaraka zilizo kuwa na aya zilizo andikwa katika Surah zake kama zilivyo andikwa mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw):

(Hiyo ndio sababu agizo la Abu Bakr (ra) la kukusanywa Qur'an halikuwa ni agizo la kuiandika katika msahafu mmoja, bali lilikuwa ni agizo la kuzileta pamoja nyaraka zilizo kuwa zimeandikwa mbele ya Mtume (saw) katika sehemu moja na lilikuwa ni agizo la kuyakinisha; kuwa ziko katika umbile sawia kama zilivyo kuwa kwa kuzithibitisha kwa ushahidi wa mashahidi wawili … Nyaraka zilibakia zimehifadhiwa mikononi mwa Abu Bakr (ra) wakati wa uhai wake na kisha 'Umar (ra) wakati wa uhai wake na kisha Hafswa binti yake 'Umar (ra), mama wa Waumini kwa mujibu wa turathi ya 'Umar (ra).  

Hii ilikuwa ni kuhusiana na ukusanyaji wa Abu Bakr (ra). Ama ukusanyaji wa 'Uthman (ra), katika mwaka wa tatu au (baadhi wanasema) mwaka wa pili wa Khilafah yake yaani 25 H, Hudhaifah ibn al-Yaman (ra) alimwendea 'Uthman (ra) mjini Madina katika wakati ambapo watu wa al-Sham na watu wa Iraq walikuwa wanatangaza vita vya kuiteka Armenia na Azerbaijan. Hudhaifah (ra) alikuwa na hofu ya ikhtilafu zao (watu wa al-Sham na Iraq) katika usomaji wao wa Qur'an.

Hivyo alisafiri hadi kwa 'Uthman. Hudhaifah (ra) alikuwa na hofu ya ikhtilafu zao (watu wa al-Sham na Iraq) katika usomaji wao wa Qur'an, hivyo alimwambia, "Uthman Amiri wa Waumini! Liokoe taifa hili kabla hawajatofautiana kuhusu Kitabu (Qur'an) kama walivyo tofautiana Mayahudi na Manaswara kabla." Hivyo 'Uthman (ra) akatuma ujumbe kwa Hafswa (ra) akisema, "Tutumie nyaraka za Qur'an ili tuzikusanye ziwe rasimu madhubuti na kisha kuziregesha nyaraka hizo kwako." Hafswa (ra) akazituma kwa 'Uthman (ra). 'Uthman (ra) kisha akamwagiza Zaid bin Thabit (ra), 'Abd Allah ibn al-Zubair, Said ibn al-'As na 'Abd al-Rahman ibn Harith ibn Hisham kuziandika upya nyaraka hizo katika rasimu madhubuti. Walifanya hivyo, na baada ya kuandika nakala nyingi, 'Uthman (ra) alizirudisha nyaraka asili kwa Hafswa (ra). 'Uthman (ra) alituma nakala moja kwa kila wilaya ya Waislamu, na kuamuru kuwa nyaraka zote nyenginezo za Qur'an, ima ziwe zimeandikwa vipande vipande au nyaraka nzima nzima, zichomwe. Idadi ya nakala zilizo tengezwa ilikuwa ni saba. Misahafu hiyo saba ilitumwa Makkah, al-Sham, Yemen, Bahrain, Basra, Kufah, na nakala moja ilibakishwa mjini Madina.   

Hivyo basi, kitendo cha 'Uthman (ra) hakikuwa ni ukusanyaji wa Qur'an bali kilikuwa tu ni kukariri na kunakili kitu kile kile kilicho nakiliwa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kama kilivyo kuwa. Hakufanya chochote chengine isipokuwa kutengeza nakala saba kutokana na nakala iliyo hifadhiwa mikononi mwa Hafswa (ra), mama wa Waumini na kuwaunganisha watu katika rasimu hii moja na kupiga marufuku rasimu au nakala nyengine yoyote kinyume na hii. Jambo lililoafikiwa ni rasimu na nakala hii. Ni rasimu na nakala hii hii ndiyo iliyo andikwa kutokana na nyaraka zilizo andikwa mbele ya Mtume wa Allah (saw) wakati wahyi ulikuwa ukiteremka. Na ni nakala hii hii ambayo Abu Bakr (ra) alikuwa ameikusanya. Kisha Waislamu wakaanza kutengeza nakala kutokana na nakala hii na sio nakala nyengineyo yoyote. Hakuna kilicho bakia isipokuwa msahafu wa 'Uthman (ra) katika rasimu yake. Pindi wachapishaji walipokuja, msahafu ukapigwa chapa kutokana na nakala hii ikiwa na rasimu hiyo hiyo).   

3- Hivyo kama unavyo ona, kadhia haikuwa ni upokezi wa usomaji wa Qur'an, hii ilipokezwa kupitia kikundi cha maswahaba kutoka kwa Mtume (saw) ambayo bila shaka ni Tawatur, bali ni upokezi wa kile kilicho andikwa mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) … Hivyo basi, rasimu hii ya Qur'an ni Tawqeefi (ni lazima ichukuliwe kama ilivyo pasi na kubadilishwa) na lazima kujifunga kwayo pekee. Ni haramu kuiandika Qur'an kwa rasimu yoyote nyengine isipokuwa kwa rasimu hii. Kamwe hairuhusiwi kuibadilisha … Bali, ni lazima tujifunge kwa rasimu ya Qur'an ya Uthman (ra), ni khaas kwa uandishi wa Qur'an nzima, lakini katika kuandika Qur'an kunukuu dalili au kuandika katika ubao kwa ajili ya elimu au mengineyo, au katika sehemu nyengine isiyo kuwa msahafu: inaruhusiwa kuandika kwa herufi tofauti, kama vile [الرِّبَوا ]  “riba”. 

Katika Qur'an, yaweza kuandikwa katika ubao kama (الربا) kwa sababu uidhinishaji wa Mtume (saw) na ijma ya maswahaba (ra) ilikuwa kwa Qur'an (msahafu) pekee sio pengine popote, na sio kipimo cha vitu vyengine kwa sababu ni Tawqeefi, haina sababu ya kisheria ('Illah), na hakuna nafasi ya Qiyas hapa.

Pili, mada ya Hadith uliyo ulizia kuihusu imesimuliwa na al-Bukhari kama ifuatavyo:

 (4604- حَدَّثَنَا مُوسَى حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ حَدَّثَنَا ابْنُ شِهَابٍ أَنَّ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ حَدَّثَهُ أَنَّ حُذَيْفَةَ بْنَ الْيَمَانِ قَدِمَ عَلَى عُثْمَانَ وَكَانَ يُغَازِي أَهْلَ الشَّأْمِ فِي فَتْحِ إِرْمِينِيَةَ وَأَذْرَبِيجَانَ مَعَ أَهْلِ الْعِرَاقِ فَأَفْزَعَ حُذَيْفَةَ اخْتِلَافُهُمْ فِي الْقِرَاءَةِ فَقَالَ حُذَيْفَةُ لِعُثْمَانَ يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ أَدْرِكْ هَذِهِ الْأُمَّةَ قَبْلَ أَنْ يَخْتَلِفُوا فِي الْكِتَابِ اخْتِلَافَ الْيَهُودِ وَالنَّصَارَى فَأَرْسَلَ عُثْمَانُ إِلَى حَفْصَةَ أَنْ أَرْسِلِي إِلَيْنَا بِالصُّحُفِ نَنْسَخُهَا فِي الْمَصَاحِفِ ثُمَّ نَرُدُّهَا إِلَيْكِ فَأَرْسَلَتْ بِهَا حَفْصَةُ إِلَى عُثْمَانَ فَأَمَرَ زَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ وَعَبْدَ اللَّهِ بْنَ الزُّبَيْرِ وَسَعِيدَ بْنَ الْعَاصِ وَعَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ الْحَارِثِ بْنِ هِشَامٍ فَنَسَخُوهَا فِي الْمَصَاحِفِ وَقَالَ عُثْمَانُ لِلرَّهْطِ الْقُرَشِيِّينَ الثَّلَاثَةِ إِذَا اخْتَلَفْتُمْ أَنْتُمْ وَزَيْدُ بْنُ ثَابِتٍ فِي شَيْءٍ مِنْ الْقُرْآنِ فَاكْتُبُوهُ بِلِسَانِ قُرَيْشٍ فَإِنَّمَا نَزَلَ بِلِسَانِهِمْ فَفَعَلُوا حَتَّى إِذَا نَسَخُوا الصُّحُفَ فِي الْمَصَاحِفِ رَدَّ عُثْمَانُ الصُّحُفَ إِلَى حَفْصَةَ وَأَرْسَلَ إِلَى كُلِّ أُفُقٍ بِمُصْحَفٍ مِمَّا نَسَخُوا وَأَمَرَ بِمَا سِوَاهُ مِنْ الْقُرْآنِ فِي كُلِّ صَحِيفَةٍ أَوْ مُصْحَفٍ أَنْ يُحْرَقَ.)

(4604- Musa alituhadithia, Ibrahim alituhadithia, Ibn Shihab alituhadithia kuwa Anas bin Malik alimuhadithia kuwa Hudhaifah bin al-Yaman alikwenda kwa 'Uthman na katika wakati ambapo watu wa al-Sham pamoja na watu wa Iraq walikuwa wakipigana kuifungua Armenia na Azerbaijan. Hudhaifah akawa na hofu ya tofauti zao katika kuisoma Qur'an, hivyo akamwambia 'Uthman, "Ewe Amiri wa Waumini! Uokoe Umma huu kabla haujatofautiana katika Kitabu (Qur'an) kama walivyo tofautiana  Mayahudi na Manaswara." Basi 'Uthman akatuma ujumbe kwa Hafswa akisema, "Tutumie nyaraka za Qur'an ili tuzikusanye katika nakala madhubuti kisha tutakurudishia nakala hizo kwako." Hafswa akazituma kwa 'Uthman. Akamuamrisha Zaid bin Thabit, `Abdullah bin Az-Zubair, Sa`id bin Al-As na `AbdurRahman bin Harith bin Hisham kuziandika upya nyaraka hizo katika nakala madhubuti. 'Uthmani akawaambia Maquraishi hao watatu, "endapo mutakhitalifiana na Zaid bin Thabit kitu katika Qur'an basi kiandikeni kwa lahaja ya kiquraishi, kwani hakika iliteremka kwa lahaja yao." Wakafanya hivyo, walipo kwisha kuiandika nakala nyingi, 'Uthman akazirudisha nakala asili kwa Hafswa. Na akapeleka katika eneo nakala moja ya msahafu walio uandika na akaamrishwa nakala nyengine zozote za Qur'an isiyokuwa, ima zilizo andikwa vipande vipande au nzima nzima, hii zichomwe).

 (4604 - قَالَ ابْنُ شِهَابٍ وَأَخْبَرَنِي خَارِجَةُ بْنُ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ سَمِعَ زَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ قَالَ فَقَدْتُ آيَةً مِنْ الْأَحْزَابِ حِينَ نَسَخْنَا الْمُصْحَفَ قَدْ كُنْتُ أَسْمَعُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ بِهَا فَالْتَمَسْنَاهَا فَوَجَدْنَاهَا مَعَ خُزَيْمَةَ بْنِ ثَابِتٍ الْأَنْصَارِيِّ [ مِنْ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ]، فَأَلْحَقْنَاهَا فِي سُورَتِهَا فِي الْمُصْحَفِ.)

(4604 - Ibn Shihab asema na amenijuza Kharijah ibn Zaid Ibn Thabit kuwa alimsikia Zaid bin Thabit akisema, "Aya niliipoteza aya katika Surat Ahzab tulipokuwa tukinakili msahafu niliyo kuwa nikimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akiisoma. Basi tukaitafuta na kuipata kwa Khuzayma bin Thabit Al-Answari, (nayo ni): “Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza walio ahidiana na Mwenyezi Mungu.” [Al-Ahzab: 23] tukaikutanisha na Surah yake katika msahafu huo.

Ni wazi kutokana na Hadith hii kuwa inazungumzia kuhusu tukio la kuinakili Qur'an wakati wa utawala wa Uthman, Mwenyezi Mungu awe radhi naye. Yeye (ra) alimpa Zaid Ibn Thabit na wengineo jukumu la kuinakili Qur'an kutoka katika nyaraka na vipande vilivyo kuwa vimekusanywa zama za Abu Bakr (ra), vilikuwa katika nyumba ya Hafswa (ra). Yaani, Hadith hii inazungumzia kuhusu kunakiliwa kutoka katika nyaraka zilizo kuwa zimeandikwa mbele ya Mtume, na sio kuhusu upokezi wa usomaji wake. Hivyo Qur'an iliandikwa kwa rasimu ile ile iliyo andikwa mbele ya Mtume (saw). Hili kimsingi halihitaji Tawatur, bali inatosheleza tu upokezi wa riwaya Sahih kuhusiana nalo. Lakini wao, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, wamejitolea kuleta mashahidi wawili kwa ajili ya rasimu hiyo, kutokana tu na tahadhari na uangalifu wa ziada. Usomaji wa aya za Qur'an ulipokezwa kwetu kutoka kwa vikundi vya maswahaba kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu.

Hivyo, Mwenyezi Mungu akipenda, Yeye (swt) aliye kihifadhi Kitabu Chake, jibu la swali lako limekuwa wazi sasa,

 [ إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ]

“Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.” [Al-Hijr: 9]

Tatu, kadhia mbili zingali zahitaji kufafanuliwa:

Kwanza, ni aya zipi hizo zilizo patikana zimeandikwa na Khuzayma pakee …

Na pili, je zilipatikana kwa Khuzayma au kwa Abu Khuzayma...

Jibu lake, kwa Tawfiq ya Mwenyezi Mungu, ni haya yafuatayo:

1. Ama kuhusu kadhia ya kwanza kuhusiana na aya hizo, Al-Bukhari ana riwaya mbili chini ya Na. 4311 na chini ya Na. 4604 kama ifuatavyo:

(4311 حدثنا أَبُو الْيَمَانِ أَخْبَرَنَا شُعَيْبٌ عَنْ الزُّهْرِيِّ قَالَ أَخْبَرَنِي ابْنُ السَّبَّاقِ أَنَّ زَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ الْأَنْصَارِيَّ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ وَكَانَ مِمَّنْ يَكْتُبُ الْوَحْيَ قَالَ أَرْسَلَ إِلَيَّ أَبُو بَكْرٍ مَقْتَلَ أَهْلِ الْيَمَامَةِ وَعِنْدَهُ عُمَرُ فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ إِنَّ عُمَرَ أَتَانِي فَقَالَ إِنَّ الْقَتْلَ قَدْ اسْتَحَرَّ يَوْمَ الْيَمَامَةِ بِالنَّاسِ وَإِنِّي أَخْشَى أَنْ يَسْتَحِرَّ الْقَتْلُ بِالْقُرَّاءِ فِي الْمَوَاطِنِ فَيَذْهَبَ كَثِيرٌ مِنْ الْقُرْآنِ إِلَّا أَنْ تَجْمَعُوهُ وَإِنِّي لَأَرَى أَنْ تَجْمَعَ الْقُرْآنَ قَالَ أَبُو بَكْرٍ قُلْتُ لِعُمَرَ كَيْفَ أَفْعَلُ شَيْئاً لَمْ يَفْعَلْهُ رَسُولُ اللَّهِ rفَقَالَ عُمَرُ هُوَ وَاللَّهِ خَيْرٌ فَلَمْ يَزَلْ عُمَرُ يُرَاجِعُنِي فِيهِ حَتَّى شَرَحَ اللَّهُ لِذَلِكَ صَدْرِي وَرَأَيْتُ الَّذِي رَأَى عُمَرُ قَالَ زَيْدُ بْنُ ثَابِتٍ وَعُمَرُ عِنْدَهُ جَالِسٌ لَا يَتَكَلَّمُ فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ إِنَّكَ رَجُلٌ شَابٌّ عَاقِلٌ وَلَا نَتَّهِمُكَ كُنْتَ تَكْتُبُ الْوَحْيَ لِرَسُولِ اللَّهِ r فَتَتَبَّعْ الْقُرْآنَ فَاجْمَعْهُ فَوَاللَّهِ لَوْ كَلَّفَنِي نَقْلَ جَبَلٍ مِنْ الْجِبَالِ مَا كَانَ أَثْقَلَ عَلَيَّ مِمَّا أَمَرَنِي بِهِ مِنْ جَمْعِ الْقُرْآنِ قُلْتُ كَيْفَ تَفْعَلَانِ شَيْئاً لَمْ يَفْعَلْهُ النَّبِيُّ r فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ هُوَ وَاللَّهِ خَيْرٌ فَلَمْ أَزَلْ أُرَاجِعُهُ حَتَّى شَرَحَ اللَّهُ صَدْرِي لِلَّذِي شَرَحَ اللَّهُ لَهُ صَدْرَ أَبِي بَكْرٍ وَعُمَرَ فَقُمْتُ فَتَتَبَّعْتُ الْقُرْآنَ أَجْمَعُهُ مِنْ الرِّقَاعِ وَالْأَكْتَافِ وَالْعُسُبِ وَصُدُورِ الرِّجَالِ حَتَّى وَجَدْتُ مِنْ سُورَةِ التَّوْبَةِ آيَتَيْنِ مَعَ خُزَيْمَةَ الْأَنْصَارِيِّ لَمْ أَجِدْهُمَا مَعَ أَحَدٍ غَيْرِهِ: [لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِنْ أَنْفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم ] إِلَى آخِرِهِمَا وَكَانَتْ الصُّحُفُ الَّتِي جُمِعَ فِيهَا الْقُرْآنُ عِنْدَ أَبِي بَكْرٍ حَتَّى تَوَفَّاهُ اللَّهُ ثُمَّ عِنْدَ عُمَرَ حَتَّى تَوَفَّاهُ اللَّهُ ثُمَّ عِنْدَ حَفْصَةَ بِنْتِ عُمَرَ...)،

Kwanza: (4311- Abu Al-Yaman alitwambia, Shu’aib alitwambia kutoka kwa Az-Zahri, alisema, Ibn As-SAbbaq aliniambia kuwa Zaid Ibn Thabit Al-Ansari (ra), aliyekuwa mmoja wa wale waliokuwa wakiandika Wahyi: Abu Bakr aliniita baada ya majeraha (mabaya) miongoni mwa wapiganaji wa Yamama (ambapo idadi kubwa ya walio hifadhi Qur'an (Qurra') waliuwawa). 'Umar alikuwepo pamoja na Abu Bakr aliyesema, 'Umar alikuja kwangu na kuniambia, watu wamepata majeraha mabaya siku ya (vita) vya Yamama, na nahofia kuwa kutakuwepo na majeruhi zaidi miongoni mwa walio hifadhi Qur'an (Qurra') katika vita vyenginevyo, ambapo sehemu kubwa ya Qur'an huenda ikapotea, isipokuwa ikiwa utaikusanya. Na rai yangu ni kuwa uikusanye Qur'an." Abu Bakr akaongeza, "Nilimwambia 'Umar, 'Nitafanya vipi kitu ambacho hakukifanya Mtume wa Mwenyezi Mungu?' 'Umar aliniambia, 'Naapa kwa Mwenyezi Mungu, (hakika) ni kheri.' Hivyo 'Umar aliendelea kusisitiza, akijaribu kunishawishi ili nikubali pendekezo lake, hadi Mwenyezi Mungu akafungua kifua changu kwa ajili yake na nikawa na rai hiyo hiyo kama 'Umar." (Zaid bin Thabit akaongeza:) 'Umar alikuwa ameketi naye (Abu Bakr) na hakuwa akizungumza). "Wewe ni kijana mwenye busara na hatukushuku (kusema urongo au usahailivu): na ulikuwa ukiandika wahyi kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ). Hivyo basi, itafute Qur'an uikusanye (katika waraka mmoja). "Naapa kwa Mwenyezi Mungu, endapo yeye (Abu Bakr) angeniagiza kuliondoa moja ya majabali mahali pake haingekuwa uzito kwangu kuliko lile aliloniamrisha kwalo kuhusiana na ukusanyaji Qur'an. Nikawaambia wote, "Munasubutuje kufanya kitu ambacho Mtume hakukifanya?" Abu Bakr akasema, "Naapa kwa Mwenyezi Mungu, (hakika) ni kheri. Hivyo nikaendelea kujadiliana naye kuhusu hilo hadi Mwenyezi Mungu akafungua kufua changu kwa lile ambalo Mwenyezi Mungu alifungua kifua cha Abu Bakr na 'Umar kwalo. Hivyo nikaanza kuzitafuta nyaraka za Qur'an kutoka katika ngozi zilokauka, mifupa, matawi ya mitende na kutoka kwa walioihifadhi nyoyoni. Kwa Khuza'ima nilipata Aya mbili za Surat al-Tauba ambazo sikuwa nimezipata kwa mtu mwengine, (nazo ni):-- "Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana.Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma." (9.128). Rasimu ya Qur'an iliyo kusanywa, ilibakia na Abu Bakr hadi Mwenyezi Mungu alipomchukua, na kisha ikawa na 'Umar hadi Mwenyezi Mungu alipomchukua, na hatimaye ikabakia na Hafswa, binti ya 'Umar.)          

Kama ilivyo nasi ya Hadith, ilikuwa katika zama za Abu Bakr, Mwenyezi Mungu awe radhi naye na ni wazi kuwa waraka ulio andikwa walioupata kwa Khuzayma ulikuwa na aya za mwisho za Surah At-Tawbah.

 [لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِنْ أَنْفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم ]

“Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana.Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma.” [At-Tawba: 128].

والثانية: (4604- حَدَّثَنَا مُوسَى حَدَّثَنَا إِبْرَاهِيمُ حَدَّثَنَا ابْنُ شِهَابٍ أَنَّ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ حَدَّثَهُ أَنَّ حُذَيْفَةَ بْنَ الْيَمَانِ قَدِمَ عَلَى عُثْمَانَ وَكَانَ يُغَازِي أَهْلَ الشَّأْمِ فِي فَتْحِ إِرْمِينِيَةَ وَأَذْرَبِيجَانَ مَعَ أَهْلِ الْعِرَاقِ فَأَفْزَعَ حُذَيْفَةَ اخْتِلَافُهُمْ فِي الْقِرَاءَةِ فَقَالَ حُذَيْفَةُ لِعُثْمَانَ يَا أَمِيرَ الْمُؤْمِنِينَ أَدْرِكْ هَذِهِ الْأُمَّةَ قَبْلَ أَنْ يَخْتَلِفُوا فِي الْكِتَابِ اخْتِلَافَ الْيَهُودِ وَالنَّصَارَى فَأَرْسَلَ عُثْمَانُ إِلَى حَفْصَةَ أَنْ أَرْسِلِي إِلَيْنَا بِالصُّحُفِ نَنْسَخُهَا فِي الْمَصَاحِفِ ثُمَّ نَرُدُّهَا إِلَيْكِ فَأَرْسَلَتْ بِهَا حَفْصَةُ إِلَى عُثْمَانَ فَأَمَرَ زَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ وَعَبْدَ اللَّهِ بْنَ الزُّبَيْرِ وَسَعِيدَ بْنَ الْعَاصِ وَعَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ الْحَارِثِ بْنِ هِشَامٍ فَنَسَخُوهَا فِي الْمَصَاحِفِ وَقَالَ عُثْمَانُ لِلرَّهْطِ الْقُرَشِيِّينَ الثَّلَاثَةِ إِذَا اخْتَلَفْتُمْ أَنْتُمْ وَزَيْدُ بْنُ ثَابِتٍ فِي شَيْءٍ مِنْ الْقُرْآنِ فَاكْتُبُوهُ بِلِسَانِ قُرَيْشٍ فَإِنَّمَا نَزَلَ بِلِسَانِهِمْ فَفَعَلُوا حَتَّى إِذَا نَسَخُوا الصُّحُفَ فِي الْمَصَاحِفِ رَدَّ عُثْمَانُ الصُّحُفَ إِلَى حَفْصَةَ وَأَرْسَلَ إِلَى كُلِّ أُفُقٍ بِمُصْحَفٍ مِمَّا نَسَخُوا وَأَمَرَ بِمَا سِوَاهُ مِنْ الْقُرْآنِ فِي كُلِّ صَحِيفَةٍ أَوْ مُصْحَفٍ أَنْ يُحْرَقَ.)

Pili: (4604 – Musa alitwambia, Ibrahim alitwambia, Ibn Shihab alitwambia kuwa Anas bin Malik alimwambia kuwa Hudhaifa bin Al-Yaman alikuja kwa 'Uthman katika zama ambapo watu wa Sham na watu wa Iraq walikuwa wakipigana ili kuifungua Armenia na Azerbaijan. Hudhaifa alihofia ikhtilafu zao (watu wa Sham na Iraq) katika usomaji wa Qur'an, hivyo akamwambia 'Uthman, "Ewe amiri wa Waumini! Uokoe Umma huu kabla hawajakhitilafiana kuhusu Kitabu (Qur'an) kama walivyo khitilafiana Mayahudi na Manaswara kabla." Hivyo, 'Uthman akatuma ujumbe kwa Hafswa akisema, "Tutumie nyaraka za Qur'an ili tuikusanye Qur'an katika nakala madhubuti na kisha kurudisha nyaraka hizo asili mwako." Hafswa akazituma kwa 'Uthman. 'Uthman kisha akawaamuru Zaid bin Thabit, 'Abdullah bin Az-Zubair, Sa'id bin Al-As na AbduRahman bin Harith bin Hisham kuandika upya nyaraka hizo katika nakala zake madhubuti. 'Uthman akawaambia Maqurayshi hao watatu, "Endapo mutakhitilafiana na Zaid bin Thabit juu ya nukta yoyote katika Qur'an, basi iandikeni kwa lahaja ya Kiqureishi, kwani Qur'an iliteremshwa kwa lahaja yao." Wakafanya hivyo, na baada ya kuandika nakala nyingi, 'Uthman akarudisha nakala asili kwa Hafswa. 'Uthman akatuma katika kila wilaya ya Waislamu nakala moja, na kuamuru kuwa nakala zote nyenginezo za Qur'an, ima ziwe zimeandikwa vipande vipande au nzima nzima, zichomwe.)

قَالَ ابْنُ شِهَابٍ وَأَخْبَرَنِي خَارِجَةُ بْنُ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ سَمِعَ زَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ قَالَ فَقَدْتُ آيَةً مِنْ الْأَحْزَابِ حِينَ نَسَخْنَا الْمُصْحَفَ قَدْ كُنْتُ أَسْمَعُ رَسُولَ اللَّهِ r يَقْرَأُ بِهَا فَالْتَمَسْنَاهَا فَوَجَدْنَاهَا مَعَ خُزَيْمَةَ بْنِ ثَابِتٍ الْأَنْصَارِيِّ [مِنْ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ ] ، فَأَلْحَقْنَاهَا فِي سُورَتِهَا فِي الْمُصْحَفِ.)،

(Ibn Shihab amesema na akanijuza Kharijah ibn Zaid Ibn Thabit kuwa alimsikia Zaid bin Thabit akisema, "Niliikosa Aya kutoka katika Surat Ahzab tulipo nakili Qur'an na nilikuwa nikimsikia Mtume (ﷺ) akiisoma. Hivyo tuliitafuta na kuipata kwa Khuzayma bin Thabit Al-Answari, na tukaiongeza katika Surah yake ndani ya Msahafu. (Aya hiyo ilikuwa): “Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza walio ahidiana na Mwenyezi Mungu.” [Al-Ahzab: 23]

Kutokana na nasi hii ya Hadith ni katika zama za Uthman (ra) na ni dhahiri kuwa nyaraka walizozipata kwa Khuzaymah zilikuwa ni aya kutoka katika Surat Al-Ahzab:

 [مِنْ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ ]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza walio ahidiana na Mwenyezi Mungu.” [Al-Ahzab: 23]

Kwa kuziangalia kwa makini Hadith (4311) na (4604), zilizo simuliwa na al-Bukhari, yaani ni Sahih katika silsila (Sanad) zake, ni wazi kuwa:

A- Kwanza, tunaweka wazi kuwa Hadith hizo mbili hazihusiani na tawatur ya aya hizo mbili. Katika riwaya zote mbili, mada ni kuhusu rasimu na sio Tawatur ya hifdhi. Kila aya ilihifadhiwa na kikundi cha maswahaba wa Mtume (saw). Maswahaba hao walitaka kuipokeza rasimu halisi iliyo andikwa mbele ya Mtume (saw), hawakutaka watu waandike kwa mujibu wa hifdhi zao na kupelekea tofauti ya herufi, bali walitaka kuziandika aya kwa rasimu ile ile iliyo andikwa mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Kutokana na tahadhari ya ziada na tawfiq kutoka kwa Al-Aziz, Al-Hakim anaye sema:   

 [إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ]

“Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.” [Al-Hijr: 9]

Hii ndio sababu hukmu ya kisheria ilivuliwa, kuwa hairuhusiwi kuchapisha Msahafu isipo kuwa kwa rasimu ya 'Uthman, Mwenyezi Mungu awe radhi naye.  

B- Ukusanyaji wa nyaraka zilizo andikwa ulikuwa katika zama za Abu Bakr kama ilivyo elezwa katika dalili Sahih, kutabanni mashahidi wawili kwa kila waraka pia ni Sahih … Wakati wa utawala wa Uthman, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, nakala za Qur'an kutoka katika nyaraka zilizo kusanywa zama za Abu Bakr zilitengezwa, ambapo wakati wa kunakiliwa kwake alikuwa nazo Hafswa, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, Uthman alitaka ziletwe na akamwagiza Zaid na watu watatu wengine waliokuwa naye kutengeza nakala kadhaa za Qur'an kutokana na nyaraka hizi.

Hakuna uwezekano hapa, yaani, katika utawala wa Uthman, wa kupotea waraka hata mmoja ulioandikwa, hili kama ni kutokea basi lingetokea wakati wa ukusanyaji nyaraka hizo katika utawala wa Abu Bakr, yaani, nyaraka ambamo aya hizo mbili za At-Tawba zimeandikwa:

 [لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِنْ أَنْفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُمْ بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَحِيمٌ * فَإِنْ تَوَلَّوْا فَقُلْ حَسْبِيَ اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ ]

“Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana.Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma. Basi wakikengeuka, wewe sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Hapana mungu isipokuwa Yeye, na Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi” [At-Tawba: 128 - 129].

Hivyo waraka huo haukuwa wakati wa kunakili katika utawala wa Uthman, kwa sababu ujumuishaji ulifanywa zama za Abu Bakr na sio Uthman, hivyo basi Hadith ya mwisho ya Al-Bukhari, Na. 4604 maana yake inakataliwa (kupitia Diraya) nayo ni:

 (قَالَ ابْنُ شِهَابٍ وَأَخْبَرَنِي خَارِجَةُ بْنُ زَيْدِ بْنِ ثَابِتٍ سَمِعَ زَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ قَالَ فَقَدْتُ آيَةً مِنْ الْأَحْزَابِ حِينَ نَسَخْنَا الْمُصْحَفَ قَدْ كُنْتُ أَسْمَعُرَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقْرَأُ بِهَا فَالْتَمَسْنَاهَا فَوَجَدْنَاهَا مَعَ خُزَيْمَةَ بْنِ ثَابِتٍ الْأَنْصَارِيِّ [مِنْ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ] ، فَأَلْحَقْنَاهَا فِي سُورَتِهَا فِي الْمُصْحَفِ.)

(Ibn Shihab amesema na Kharijah ibn Zaid Ibn Thabit akanipa habari kuwa alimsikia Zaid bin Thabit akisema, "Niliikosa Aya katika Surat Ahzab tulipokuwa tukinakili Qur'an na ambayo nilikuwa nikimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akiisoma. Hivyo tuliitafuta na kuipata kwa Khuzayma bin Thabit Al-Ansari, na tukaiongeza katika Sura yake Msahafuni. (Aya hiyo ilikuwa): “Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza walio ahidiana na Mwenyezi Mungu.” [Al-Ahzab: 23]

2- Ama kuhusu kadhia ya pili, ambayo ni, je, yule swahaba ambaye kwake Zaid alizipata aya mbili za At-Tawba, katika waraka ulioandikwa, na hakuzipata kwa mwengine yeyote, ni Khuzayma au Abu Khuzayma? Jibu ni kama ifuatavyo:

- Al-Bukhari amezisimulia riwaya hizi mbili: (4311) na (4603

Usimulizi wa nambari 4311 uliotajwa juu, unaeleza:

[Hivyo nikaanza kuitafuta Qur'an na kuikusanya kutoka (kwa yale yalioandikwa katika) matawi ya mitende, vijiwe vyeupe na pia kutoka kwa watu walioihifadhi kwa moyo, mpaka nikaipata Aya ya mwisho ya Surat At-Tauba kwa Abi Khuzaima Al-Ansari, na sikuipata kwa mwengine yeyote asiyekuwa yeye. Aya hii ni: 

 [لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِنْ أَنْفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُمْ بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَحِيمٌ * فَإِنْ تَوَلَّوْا فَقُلْ حَسْبِيَ اللَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَهُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْعَظِيمِ]

“Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana.Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma. Basi wakikengeuka, wewe sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Hapana mungu isipokuwa Yeye, na Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi” [at-Tauba:128-129]).

[4603 - حَدَّثَنَا مُوسَى بْنُ إِسْمَاعِيلَ عَنْ إِبْرَاهِيمَ بْنِ سَعْدٍ حَدَّثَنَا ابْنُ شِهَابٍ عَنْ عُبَيْدِ بْنِ السَّبَّاقِ أَنَّ زَيْدَ بْنَ ثَابِتٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ أَرْسَلَ إِلَيَّ أَبُو بَكْرٍ مَقْتَلَ أَهْلِ الْيَمَامَةِ فَإِذَا عُمَرُ بْنُ الْخَطَّابِ عِنْدَهُ قَالَ أَبُو بَكْرٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ إِنَّ عُمَرَ أَتَانِي فَقَالَ إِنَّ الْقَتْلَ قَدْ اسْتَحَرَّ يَوْمَ الْيَمَامَةِ بِقُرَّاءِ الْقُرْآنِ وَإِنِّي أَخْشَى أَنْ يَسْتَحِرَّ الْقَتْلُ بِالْقُرَّاءِ بِالْمَوَاطِنِ فَيَذْهَبَ كَثِيرٌ مِنْ الْقُرْآنِ وَإِنِّي أَرَى أَنْ تَأْمُرَ بِجَمْعِ الْقُرْآنِ قُلْتُ لِعُمَرَ كَيْفَ تَفْعَلُ شَيْئاً لَمْ يَفْعَلْهُ رَسُولُ اللَّهِ r قَالَ عُمَرُ هَذَا وَاللَّهِ خَيْرٌ فَلَمْ يَزَلْ عُمَرُ يُرَاجِعُنِي حَتَّى شَرَحَ اللَّهُ صَدْرِي لِذَلِكَ وَرَأَيْتُ فِي ذَلِكَ الَّذِي رَأَى عُمَرُ قَالَ زَيْدٌ قَالَ أَبُو بَكْرٍ إِنَّكَ رَجُلٌ شَابٌّ عَاقِلٌ لَا نَتَّهِمُكَ وَقَدْ كُنْتَ تَكْتُبُ الْوَحْيَ لِرَسُولِ اللَّهِ r فَتَتَبَّعْ الْقُرْآنَ فَاجْمَعْهُ فَوَاللَّهِ لَوْ كَلَّفُونِي نَقْلَ جَبَلٍ مِنْ الْجِبَالِ مَا كَانَ أَثْقَلَ عَلَيَّ مِمَّا أَمَرَنِي بِهِ مِنْ جَمْعِ الْقُرْآنِ قُلْتُ كَيْفَ تَفْعَلُونَ شَيْئاً لَمْ يَفْعَلْهُ رَسُولُ اللَّهِ rقَالَ هُوَ وَاللَّهِ خَيْرٌ فَلَمْ يَزَلْ أَبُو بَكْرٍ يُرَاجِعُنِي حَتَّى شَرَحَ اللَّهُ صَدْرِي لِلَّذِي شَرَحَ لَهُ صَدْرَ أَبِي بَكْرٍ وَعُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا فَتَتَبَّعْتُ الْقُرْآنَ أَجْمَعُهُ مِنْ الْعُسُبِ وَاللِّخَافِ وَصُدُورِ الرِّجَالِ حَتَّى وَجَدْتُ آخِرَ سُورَةِ التَّوْبَةِ مَعَ أَبِي خُزَيْمَةَ الْأَنْصَارِيِّ لَمْ أَجِدْهَا مَعَ أَحَدٍ غَيْرِهِ [لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِنْ أَنْفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ] حَتَّى خَاتِمَةِ بَرَاءَةَ فَكَانَتْ الصُّحُفُ عِنْدَ أَبِي بَكْرٍ حَتَّى تَوَفَّاهُ اللَّهُ ثُمَّ عِنْدَ عُمَرَ حَيَاتَهُ ثُمَّ عِنْدَ حَفْصَةَ بِنْتِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ.]

[4603- Musa Ibn Ismail alituhadithia kutoka kwa Ibrahim Ibn Saad, alituhadithia Ibn Shihab kutoka kwa Ubaid Ibn As-Sabbaq kuwa Zaid Ibn Thabit (ra) amesema: Abu Bakr As-Siddiq aliniita wakati wa mauwaji ya watu wa Yamama (yaani, idadi ya Maswahaba wa Mtume waliopigana na Musailama). (Nilimwendea) na kumpata 'Umar bin Al-Khattab akiwa ameketi pamoja naye. Abu Bakr kisha akaniambia: "'Umar amekuja kwangu na kuniambia: "Majeraha yalikuwa mazito miongoni mwa waliohifadhi Qur'an siku ya Vita vya Yamama, na nahofia kuwa majeraha mazito zaidi huenda yakatokea kwa waliohifadhi Qur'an katika vita vyenginevyo, ambapo sehemu kubwa ya Qur'an huenda ikapotea. Hivyo basi napendekeza, wewe (Abu Bakr) uamuru kuwa Qur'an ikusanywe." Nikamwambia 'Umar, "Unawezaje kufanya kitu ambacho Mtume wa Mwenyezi Mungu hakukifanya?" 'Umar akasema, "Naapa kwa Mwenyezi Mungu, hii ni kheri." 'Umar aliendelea kunisisitiza kukubali pendekezo hili hadi Mwenyezi Mungu akakifungua kifua changu na nikaanza kuitambua kheri ya wazo hili ambayo 'Umar ameitambua." Kisha Abu Bakr akaniambia, 'Wewe ni kijana mwenye hekima na hatuna shaka yoyote kuhusu wewe, na ulikuwa ukiandika wahyi kwa Mtume (ﷺ). Hivyo tafuta (vipande vya nyaraka za) Qur'an na uikusanye kiwe kitabu kimoja." Naapa kwa Mwenyezi Mungu lau ungeniamrisha kuliondoa moja ya majabali mahali pake, halingekuwa zito kwangu kushinda huku kuniamrisha niikusanye Qur'an. Kisha nikamwambia Abu Bakr, "Vipi utafanya kitu ambacho Mwenyezi Mungu (ﷺ) hakukifanya?" Abu Bakr akajibu, "Naapa kwa Mwenyezi mungu, hiyo ni kheri." Abu Bakr akaendelea kunisihi kulikubali wazo lake hadi Mwenyezi Mungu akakifungua kifua changu kwa lile alichovifungua vifua vya Abu Bakr na 'Umar kwalo. Hivyo nikaanza kuitafuta Qur'an na kuikusanya (kutoka kwa yaliyo andikwa katika) matawi ya mitende, vijiwe vyeupe na pia kutoka katika watu waliyoihifadhi moyoni, hadi nikazipata Aya za mwisho za Surat at-Tauba kwa Abi Khuzaima Al-Ansari, na sikuzipata kwa mwengine yeyote isipokuwa yeye. Aya hizo ni: “Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana.Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma. Basi wakikengeuka, wewe sema: Mwenyezi Mungu ananitosheleza. Hapana mungu isipokuwa Yeye, na Yeye ndiye Mola Mlezi wa Kiti Kikuu cha Enzi” [at-Tauba:128-129]. Kisha nakala kamili ya Qur'an ikabaki na Abu Bakr hadi kifo chake, kisha 'Umar hadi mwisho wa uhai wake, na kisha Hafswa, binti ya 'Umar.]     

Ni wazi kutokana na maneno yake:

 [فَتَتَبَّعْتُ الْقُرْآنَ أَجْمَعُهُ مِنْ الْعُسُبِ وَاللِّخَافِ وَصُدُورِ الرِّجَالِ حَتَّى وَجَدْتُ آخِرَ سُورَةِ التَّوْبَةِ مَعَ أَبِي خُزَيْمَةَ الْأَنْصَارِيِّ لَمْ أَجِدْهَا مَعَ أَحَدٍ غَيْرِهِ [لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِنْ أَنْفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ] حَتَّى خَاتِمَةِ بَرَاءَةَ]

[Hivyo nikaanza kuitafuta Qur'an na kuikusanya (kutoka kwa yaliyo andikwa katika) matawi ya mitende, vijiwe vyeupe na pia kutoka katika watu waliyoihifadhi moyoni, hadi nikaipata Aya ya mwisho ya Surat at-Tauba kwa Abi Khuzaima Al-Ansari, na sikuipata kwa mwengine yeyote isipokuwa yeye. Aya hii ni:

 [لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِنْ أَنْفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ]

“Hakika amekwisha kujieni Mtume kutokana na nyinyi wenyewe; yanamhuzunisha yanayo kutaabisheni; anakuhangaikieni sana.Kwa Waumini ni mpole na mwenye huruma.” [At-Tawba: 128].

Na kwa kupitia kuangalia kwa makini na kutafakari juu ya yale yaliyo semwa katika Hadith hizo mbili, ni dhahiri kuwa jina la swahaba huyo ni Khuzayma ibn Thabit al-Ansari na sio Abu Khuzayma, na dalili ya hili ni kuwa Abu Bakr, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, aliagiza kuwa mashahidi mawili watoe ushahidi juu ya kila waraka utakao tajwa: kuwa umeandikwa mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Zaid aliwapata mashahidi wawili kwa kila aya iliyo andikwa aliotabanni isipokuwa katika aya mbili za mwisho za Surat At-Tauba. Alizipata zimeandikwa katika waraka aliokuwa nao Khuzayma pekee katika riwaya moja, na kwa Abu Khuzayma katika riwaya nyengine, na natija yake ni ukatabanniwa kwa waraka huo. Hivyo basi yule uliopatikana kwake ndiye yule unayestahiki ushahidi wake kuwa sawia na ushahidi wa watu wawili, la sivyo waraka huo haunge tabanniwa kama alivyo agiza Abu Bakr, Mwenyezi Mungu awe radhi naye. Kile ambacho ni Sahih kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ni kuwa ushahidi sawia na ushahidi wa mashahidi wawili ni ule wa Khuzayma ibn Thabit al-Ansari, kana kwamba Hadith hiyo ni kwa ajili ya hali hii: ujumuishaji wa waraka huo wake ulioandikwa. Ametukuka Mwenyezi Mungu Al-Aziz Al-Hakim Mlinzi wa Kitabu Chake; usomaji wake na rasimu yake. Hadith ya Khuzayma ni kama ifuatavyo: Imesimuliwa na Ahmad katika Musnad yake na Abu Daud katika Sunan yake na lafdhi yake (Hadith) ni ya Ahmad:

 (حَدَّثَنَا أَبُو الْيَمَانِ حَدَّثَنَا شُعَيْبٌ عَنِ الزُّهْرِيِّ حَدَّثَنِي عُمَارَةُ بْنُ خُزَيْمَةَ الْأَنْصَارِيُّ أَنَّ عَمَّهُ حَدَّثَهُ وَهُوَ مِنْ أَصْحَابِ النَّبِيِّ r أَنَّ النَّبِيَّ r ابْتَاعَ فَرَساً مِنْ أَعْرَابِيٍّ فَاسْتَتْبَعَهُ النَّبِيُّ r لِيَقْضِيَهُ ثَمَنَ فَرَسِهِ فَأَسْرَعَ النَّبِيُّ r الْمَشْيَ وَأَبْطَأَ الْأَعْرَابِيُّ فَطَفِقَ رِجَالٌ يَعْتَرِضُونَ الْأَعْرَابِيَّ فَيُسَاوِمُونَ بِالْفَرَسِ لَا يَشْعُرُونَ أَنَّ النَّبِيَّ r ابْتَاعَهُ حَتَّى زَادَ بَعْضُهُمْ الْأَعْرَابِيَّ فِي السَّوْمِ عَلَى ثَمَنِ الْفَرَسِ الَّذِي ابْتَاعَهُ بِهِ النَّبِيُّ r فَنَادَى الْأَعْرَابِيُّ النَّبِيَّ r فَقَالَ إِنْ كُنْتَ مُبْتَاعَا هَذَا الْفَرَسَ فَابْتَعْهُ وَإِلَّا بِعْتُهُ فَقَامَ النَّبِيُّ r حِينَ سَمِعَ نِدَاءَ الْأَعْرَابِيِّ فَقَالَ أَوَلَيْسَ قَدْ ابْتَعْتُهُ مِنْكَ قَالَ الْأَعْرَابِيُّ لَا وَاللَّهِ مَا بِعْتُكَ فَقَالَ النَّبِيُّ r بَلَى قَدْ ابْتَعْتُهُ مِنْكَ فَطَفِقَ النَّاسُ يَلُوذُونَ بِالنَّبِيِّ r وَالْأَعْرَابِيِّ وَهُمَا يَتَرَاجَعَانِ فَطَفِقَ الْأَعْرَابِيُّ يَقُولُ هَلُمَّ شَهِيداً يَشْهَدُ أَنِّي بَايَعْتُكَ فَمَنْ جَاءَ مِنْ الْمُسْلِمِينَ قَالَ لِلْأَعْرَابِيِّ وَيْلَكَ النَّبِيُّ r لَمْ يَكُنْ لِيَقُولَ إِلَّا حَقّاً حَتَّى جَاءَ خُزَيْمَةُ فَاسْتَمَعَ لِمُرَاجَعَةِ النَّبِيِّ r وَمُرَاجَعَةِ الْأَعْرَابِيِّ فَطَفِقَ الْأَعْرَابِيُّ يَقُولُ هَلُمَّ شَهِيداً يَشْهَدُ أَنِّي بَايَعْتُكَ قَالَ خُزَيْمَةُ أَنَا أَشْهَدُ أَنَّكَ قَدْ بَايَعْتَهُ فَأَقْبَلَ النَّبِيُّ r عَلَى خُزَيْمَةَ فَقَالَ بِمَ تَشْهَدُ فَقَالَ بِتَصْدِيقِكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ فَجَعَلَ النَّبِيُّr شَهَادَةَ خُزَيْمَةَ شَهَادَةَ رَجُلَيْنِ)

Amesimulia Ammi yake Umarah ibn Khuzaymah:

(Abu Al-Yaman alituhadithia, Shuaib alituhadithia kutoka kwa Az-Zahri, aliniambia, Umara Ibn Khuzayma Al-Ansari, kuwa ammi yake, aliyekuwa ni swahaba wa Mtume, alimwambia, kuwa Mtume (ﷺ) alinunua farasi kutoka kwa Mbedui mmoja. Mtume (ﷺ) akamchukua (mbedui) kwenda kumlipa thamani ya farasi wake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akatembea haraka haraka huku mbedui akitembea pole pole. Watu wakamsimamisha mbedui huyo na kuanza mtaradhilia awashukishie bei ya farasi huyo kwani hawakujua kuwa Mtume (ﷺ) tayari alishamnunua.

Mbedui huyo akamwita Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) akisema: Ikiwa unamtaka farasi huyu, (basi mnunue), au nitamuuza. Mtume (ﷺ) akasimama aliposikia Mbedui huyo anamwita, na kusema: Je, kwani bado sijamnunua kwako? Mbedui akasema: Naapa kwa Mwenyezi Mungu, bado sijakuuzia. Mtume (ﷺ) akasema: Bila shaka, nimemnunua kutoka kwako. Mbedui akaanza kusema: Lete shahidi. Khuzayma ibn Thabit kisha akasema: Nashuhudia kuwa umemnunua. Mtume (ﷺ) akamgeukia Khuzayma akamuuliza: Washuhudia kwa (misingi) gani?

Akasema: Kwa kuzingatia kuwa wewe ni mwaminifu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ)! Mtume (ﷺ) akaufanya ushahidi wa Khuzayma sawia na ushahidi wa watu wawili). Hii pia ilisimuliwa na Al-Hakim katika Al-Mustadrak juu ya Hadith hizi mbili Sahih na kusema: (hii ni Hadith yenye Silsila (Sanad) Sahih, na wapokezi wake ni waaminifu, kwa mujibu wa makubaliano ya Masheikh wawili, lakini hawakuisimulia).

Yote haya yanathibitisha kuwa swahaba ambaye kwaye nyaraka zilizo andikwa aya za At-Tawbah zilipatika, na hazikupatikana kwa mwengine yeyote ni Khuzayma, sio Abu Khuzayma, kwa sababu aya hiyo ilitabanniwa kwa sababu ushahidi wa mwenye aya hiyo ni sawa na ushahidi wa mashahidi wawili. Hili ni sahihi kwa Khuzayma na sio Abu Khuzayma na inaonekana kana kwamba majina yalikanganywa, hili hutokea wakati mwengine… Katika hali yoyote ile ni Khuzayma ibn Thabit al-Answari kama ilivyo onyeshwa juu.

Hivyo basi, jibu hili limejibu swali lako… Jibu hili pia ni juu ya hizo kadhia mbili za juu… Mwenyezi Mungu ni Mjuzi zaidi Mwingi wa hekima.

Ndugu yenu,

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

12 Rabii’ Al-Awwal 1441 H    

9/11/2019 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 09 Aprili 2020 17:50

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu