- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Jibu la Swali
Rai za Kifiqhi Katika Kulipa Funga
Kwa: Ig Purwantama
Swali:
Asalaam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh,
Sheikh wetu, nataka kujua hukmu ya Mwenyezi Mungu ili moyo wangu upate utulivu.
Nilikuwa katika jahiliyyah na kwa makusudi nikaacha funga ya Ramadhani bila ya udhuru, Kisha, Alhamdulillah Mwenyezi Mungu akanirehemu nikatubu, vipi nilipe funga niliyoiacha? Je ni juu yangu kulipa fidiyah kila mwaka au inatosha kulipa tu?
Nataraji Sheikh wetu utanijibu swali.
Jibu:
Waalaykum Salam Warahmatullah Wabarakatuh,
Ndugu yangu, umesema ulikuwa hufungi kwa muda mrefu tena kwa makusudi bila ya udhuru wa kisheria. Kisha baada ya miaka hiyo Mwenyezi Mungu akakuongoza kwenye njia iliyo nyoka ukawa unafunga huli mchana… Na kwa sababu ya uchamungu unataka kulipa miezi ya Ramadhani zilizopita ambazo hukufunga … Namshukuru Mwenyezi Mungu kuwa amekuongoza kwenye utiifu mzuri kiasi ambacho hukutosheka kufunga tu baada ya Mwenyezi Mungu kukuongoa, bali una pupa ya kulipa miezi ya Ramadhani ambayo hukuifunga. Mwenyezi Mungu akubariki, aifanye njema toba yako na akuenezee neema zake na rehema zake.
Ndugu mkarimu, sisi hatutabbani katika ibadati bali tunaliacha jambo kwa Muislamu mwenyewe afuate madhehebu yoyote katika funga au swala …nk. Na mimi hapa nitakutajia baadhi ya rai za kifiqhi katika kulipa funga, na linalokuwa wazi katika kifua chako na moyo wako ukatulizana kwalo unaweza ukalifuata:
1-Imeelezwa katika kitabu kiitwacho “Nihayat Al-Matlab Fi Dirayat Al-Mazhab” cha mwandishi Abdul Malik al-Juwaini, anayejulikama kama Imamu wa Misikiti Miwili Mitukufu (aliyefariki 478H), madhehebu ya Shafi’i:
(Mwenye kupitwa na funga ya Ramadhani kwa masiku kadhaa, na akapata uwezo wa kuzilipa, basi haifai yeye kuchelewesha kuzilipa mpaka (ukaingia) katika mwaka ujao, hili tunalolitaja sio sunna bali ni la lazima, ila awe anaweza na udhuru uwe umeondoka. Na kama itakuwa kuchelewesha kulipa mpaka mwaka ujao bila ya udhuru basi itakuwa kulipa pamoja na kibaba cha chakula kila siku, na kama atachelewesha kulipa kwa miaka miwili au miaka kadhaa, ongezeko la fidiyah litakua kwa njia mbili: Moja – ni kwamba haiongezeki, na wala si wajibu kuchelewesha kwa miaka kadhaa isipokuwa kwa kilichowajibu (ikabidi kuchelewesha) hata kwa mwaka mmoja… na lililosahihi hasa katika hali hii ni kuongezeka kwa fidiyah na kuifanya upya, kwa hiyo ni wajibu kwa kuchelewesha kwa kila mwaka (kutolewa) kibaba. Basi akichelewesha miaka miwili, ni wajibu vibaba viwili kwa kila siku anayolipa, hivi ndivyo inavyozidi na kuendelea. Huu ndio msimamo katika fidiyah…). Hii ina maana kulipa funga ya Ramadhani kwa ambaye hakuifunga ailipe kabla ya Ramadhani inayofuata na akichelewesha mpaka baada kuingia Ramadhani (nyingine) basi ni juu yake kulipa na kutoa fidiya… Rai yake nyingine, ni kwamba kwa mfano, akichelewesha kulipa kwa miaka miwili atawajibika kulipa pamoja na fidiya mbili. Na kuendelea hivyo.
This means that making up the fast of Ramadan for those who have not fasted it, must be made up before the next Ramadan, if there is delay after the arrival of Ramadan, then one must make up the fast and pay the “fidiyah”. His other opinion is that if the person delays making up the fast for two years for example, he must pay two “fidiyah” with making up the fasts, and so on.
2 – Katika cha “Kashaf Al-Qina’ ‘An Matn Al-Iqna” kilichoandikwa na mwandishi Mansur Bin Younis Al-Bahouti Al-Hanbali (aliyefariki: 1051 H) aliandika:
(Yeyote aliyekosa kufunga Ramadhani yote au nusu … Lazima alipe siku hizo … Inaruhusiwa kuchelewesha kuzilipa kwa sharti kuwa muda wao haujapita, ambazo ni kuonekana kwa mwezi wa Ramadhani … Hairuhusiwi kuchelewesha kuzilipa baada ya Ramadhani nyingine isipokuwa na udhuru … Lau kuchelewesha kutakuwa ni katika Ramadhani inayofuata au Ramadhani nyingine, basi mtu huyo lazima azifunge pamoja na kuwalisha Masikini kwa kila siku aliyokosa ambayo itakuwa ni kafara, “fidiya” hairudiwi kwa kutegemea idadi ya Ramadhani kwa sababu muda wa kuchelewesha hauzidishi wajib kama vile lau angelichelewesha miaka ya Hajj, anatakiwa tu kutekeleza Hajj moja). Hii inamaanisha kwamba wale waliokosa kufunga kuanzia Ramadhani na hawakulipa kabla Ramadani inayofuata, lazima walipe funga na watoe “fidiya.”
3-Ama katika madhehebu ya Abu Hanifa ni kuwa, kwa namna yoyote atakayochelewesha kulipa hawajibiki (kutoa fidiya) isipokuwa ni kulipa funga tu, ikiwa itafika Ramadhani nyIngine … atalipa ile iliyompita na wala hawajibiki fidiya kwa kuchelewesha:
-Imeelezwa katika kitabu cha Al-Mabsout cha mwandishi Al-Surkhusi (aliyefariki 483 H (madh-hab ya Hanafi):
Amesema: (Mtu ambaye ana wajibu wa kulipa masiku katika mwezi wa Ramadhani na akawa hakulipa mpaka ikaingia Ramadhani ijayo… ni juu yake kulipa Ramadhani iliyopita na wala hatolipa fidiya kwa mujibu wa rai yetu. Na kwa mujibu wa Shafi Mwenyezi Mungu amrehemu, analazimika kulipa pamoja na kulisha masikini kwa kila siku… Sisi tumejifunga na kauli ya Mwenyezi Mungu (swt): [[فَعِدَّةٌ مِنْ أَيَّامٍ أُخَرَ “basi atimize hisabu katika siku nyingine.” [Al-Baqarah: 184]. Hakuna muda maalumu. Muda baina ya Ramadhani mbili ni ziada na hii ni ibada ya muda na kulipiza hakujafunga kwa muda maalum…)
-Na imeelezwa katika kitabu cha “Bada'i al-Sanaye’ Fi Tarteeb Ash-Sharaye’” cha mwandishi Alaa al-Din, al-Kasani al-Hanafi (d. 587 AH):
(…madhehebu ya wenzetu – wanavyuoni wetu – ni kwamba wajibu wa kulipa hauna wakati maalumu, kutokana na kile tulichoeleza kuwa jambo hili la kulipa ni la kukata kiujumla halina wakati maalumu, kwa hiyo libakie kwa ujumla wake. Hivyi basi, twasema: Lau mtu atachelewesha kulipa funga ya Ramadhani mpaka kuwasili kwa Ramadhani nyingine, hatakiwi kulipa “fidiya”).
Hii ina maana kwa mujibu wa madhehebu ya Abu Hanifa kilichowajibu ni kulipa tu bila fidiya, yaani atalipa miezi ambayo hakufunga tu.
Na kama nilivyokueleza mwanzoni, kuwa sisi hatutabbani katika ibadat, nilichokutajia ni baadhi ya rai za madhehebu ya Abu Hanifa, Shafi’i na Faqhi Al-Hanbali. Linalokua wazi katika kifua chako basi lifanye… Mwenyezi Mungu akusaidie kwa alipendalo na kuliridhia.
Nataraji haya kuwa yametosheleza. Na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi na mwenye hekima zaidi.
Ndugu yenu,
Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah
8 Ramadan 1440 H
Jumatatu, 13/5/2019 M