- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Uhakiki wa Habari 07/06/2023
Iran Yazindua Kombora Jipya la Hypersonic
Iran ilizindua kombora lake la kwanza la balestiki lililotengenezwa nchini wakati wa hafla moja kwa mujibu wa shirika la habari la serikali IRNA. Kombora hilo lililopewa jina la "Fattah" liliwasilishwa wakati wa hafla iliyohudhuriwa na Rais Ebrahim Raisi na makamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC). Kombora hilo linaweza kufikia kasi ya juu ya kilomita 15,000 kwa saa, iliripoti IRNA. "Kombora la Fattah la Hypersonic lina masafa ya umbali wa kilomita 1,400 na lina uwezo wa kupenya ngao zote za ulinzi," alisema Amirali Hajizadeh, mkuu wa kikosi cha anga cha IRGC, kama alivyonukuliwa katika vyombo vya habari vya serikali. Iran kwa miaka mingi imekuwa na mpango wa hali ya juu wa makombora lakini Tehran mara nyingi imekuwa ikishutumiwa na wachambuzi wa kijeshi kwa kutia chumvi uwezo wake wa kijeshi na hadi kombora hilo litakapojaribiwa hakuna uwezekano wa uwezo wake kuthibitishwa.
Bwawa la Nova Kakhovka Lashambuliwa
Mamia ya watu wamehamishwa kutoka kwenye makaazi kando ya eneo la kusini la Mto Dnipro nchini Ukraine baada ya maji kufurika kwenye bwawa la Nova Kakhovka lililopasuka, yakizamisha mitaa na viwanja vya mji. Kuporomoka kwa jengo hilo ni katika eneo la kusini mwa Ukraine ambalo Moscow imelidhibiti kwa zaidi ya mwaka mmoja. Kyiv ilishutumu vikosi vya Urusi kwa kulipua bwawa hilo na kituo cha kuzalisha umeme kwa maji, huku maafisa wa Urusi wakilaumu shambulizi la bomu la Ukraine. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy alisema uvunjaji wa bwawa hilo ni "janga kubwa zaidi la kimazingira lililosababishwa na mwanadamu barani Ulaya katika miongo kadhaa". Kwa mashambulizi ya hivi majuzi dhidi ya Kremlin na mashambulizi nchini Urusi inaonekana kuwa Urusi inajitahidi katika vita vyake dhidi ya Ukraine ambavyo sasa vinaendelea kurefuka.