Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uhakiki wa Habari 17/05/2023

Vita dhidi ya Ugaidi Vyasababisha Vifo vya zaidi ya Milioni 4.5

Vita vya baada ya 9/11 vya Marekani vimesababisha vifo vya zaidi ya milioni 4.5, kwa mujibu wa ripoti kuu mpya kutoka kwa Mradi wa Gharama za Vita katika Chuo Kikuu cha Brown. Takriban vifo milioni 1 kati ya hivyo vilitokana na mapigano ya moja kwa moja katika maeneo ya vita kote Afghanistan, Pakistan, Iraq, Libya, Syria, Somalia, na Yemen, huku milioni 3.5 vilivyobaki ni "vifo visivyo vya moja kwa moja" vilivyotokana na mizozo ya "kuharibiwa kwa uchumi, huduma za umma, na mazingira,” kulingana na ripoti hiyo. Matokeo ya kutisha yanaonyesha athari za muda mrefu za Vita vya Kilimwengu dhidi ya Ugaidi, ambavyo vimekuwa vita vibaya zaidi katika karne ya 21 hadi sasa. Idadi ya vifo, ambavyo watafiti wa Brown waliielezea kama "makadirio ya busara na ya kihafidhina," inashindana na mizozo mikubwa ya baada ya WWII, pamoja na vita huko Korea na Vietnam. "Mahali kama Afghanistan, swali kubwa ni kama kifo chochote kinaweza kuchukuliwa kuwa hakihusiani na vita," Stephanie Savell, mwandishi wa ripoti hiyo, alisema katika taarifa. "Vita mara nyingi huua watu wengi zaidi kwa njia isiyo ya moja kwa moja kuliko katika mapigano ya moja kwa moja, haswa watoto wachanga." Savell alielezea kwenye Twitter kwamba, huku kila vita vikiwa na sababu ngumu, alichagua kuijumuisha mizozo ambapo "Kupambana na ugaidi kwa Marekani kumekuwa na dori kuu katika angalau kuzidisha ghasia.”

Uchaguzi Mkuu Unaonyesha Vyema kwa Muungano Tawala katika Urais na Ubunge

Uchaguzi wa urais wa Uturuki utarudiwa baada ya wiki mbili baada ya rais aliyeko madarakani Recep Tayyip Erdogan kupata 49.5% ya kura, mpinzani Kemal Kilicdaroglu akishinda 44.89%, na mgombea mzalendo Sinan Ogan akishinda 5.17%. Katika Bunge la Kitaifa, kwa mujibu wa matokeo ya awali, muungano unaotawala wa People's Alliance ulipata viti 321, muungano wa upinzani wa Nation Alliance ulipata viti 213, na muungano wa upinzani wa Labour and Freedom Alliance ulipata viti 66. Licha ya upigaji kura ambao ulionyesha uwezekano mkubwa wa kupata ushindi kwa upinzani, matokeo ya sasa yanamaanisha kuwa Erdogan na muungano wake tawala wana uwezekano wa kubakisha udhibiti wao juu ya urais na ubunge, kwani wafuasi wengi wa Ogan wanaweza kumgeukia Erdogan wakati wa marudio ya uchaguzi ya Mei 28. Hata hivyo, hii ni mara ya kwanza kwa uchaguzi wa urais wa Uturuki kwenda kwa raundi ya pili, hali inayoashiria kwamba uungwaji mkono kwa Erdogan umeshuka baada ya kipindi cha muda. Iwapo Erdogan atashinda uchaguzi, atakuwa katika nafasi ya kuidhinisha ombi la Uswidi la kujiunga na NATO ifikapo mkutano wa kilele wa Julai. Ingawa mitandao ya kijamii ilizagaa na uvumi kwamba uhesabu wa kura ulikuwa unacheleweshwa kimakusudi katika maeneo ya upinzani, upinzani haukutoa tuhma zozote kuu za udanganyifu au wizi wa kura.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu