- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Vichwa vya Habari: 24/12/2022
Vichwa vya Habari:
• Maafisa wa Serikali ya Afghanistan Waliwasaidia Walanguzi Kupenya na takriban $1 bilioni Pesa Taslimu na Dhahabu Nje ya Afghanistan
• Marekani Yatangaza Rekodi ya US $200m ya Kukuza Usawa wa Kijinsia nchini Pakistan
• Hisa za Makampuni ya Kichina ya Semiconductor Zaongezeka huku Ushindani wa Vipuri vya Chip Ukipamba Moto
Maelezo:
Maafisa wa Serikali ya Afghanistan Waliwasaidia Walanguzi Kupenya na takriban $1 bilioni Pesa Taslimu na Dhahabu Nje ya Afghanistan
Katika kipindi cha miezi ya mwisho ya Jamhuri ya Kiislamu ya Afghanistan, wakati Taliban waliposonga mbele kwenye mji mkuu, serikali iliyochaguliwa ilijitahidi kuwahakikishia wakuu wake wa Marekani kwamba inaweza kudumisha udhibiti. Hata hivyo wakati huo huo, walanguzi walikuwa wakibeba mamia ya mamilioni ya dolari pesa taslimu na dhahabu nje ya nchi kinyume cha sheria kwa usaidizi wa maafisa kutoka ndani ya serikali ya Afghanistan, kwa mujibu wa nyaraka za ndani za serikali na maafisa wa zamani wa Afghanistan. Afisi ya Ashraf Ghani, rais wa Afghanistan anayeungwa mkono na Marekani, ilikuwa imefahamishwa kuhusu tatizo hilo, wadadisi wa mambo wanasema. Lakini haikufanya chochote kuzuia. Nyaraka zilizokusanywa na serikali iliyobanduliwa na kupatikana na Insider zinaonyesha kuwa dolari milioni 59.7 pesa taslimu na dhahabu zilitoka Afghanistan hadi Uzbekistan kupitia bandari ya Hairatan katika miezi mitatu ya kwanza ya 2021, wakati Amerika ikifikiria kuondoa vikosi vyake na Taliban wakijipanga kwa mashambulizi ya majira ya masika ambayo hatimaye yaliiangusha Kabul. Katika kipindi cha miezi 13 kuanzia Mei 2019 hadi Mei 2020, jumla ilikuwa $824 milioni. Ingawa wasafirishaji walishindwa kutangaza pesa hizo kwa maafisa wa Afghanistan walipokuwa wakiondoka nchini, mawakala wa forodha wa Uzbekistan waliokuwa upande wa pili wa mpaka walirekodi pesa hizo taslimu na dhahabu kwenye fomu za forodha zilizoandikwa kwa mkono. Rekodi hizo zilipatikana na maafisa wa kupambana na ufisadi wa Afghanistan kama sehemu ya uchunguzi wa ulanguzi wa pesa, na zinaunda msingi wa ripoti kali inayoandika mto wa pesa zilizotiririka kutoka kwa taifa hilo masikini. Pesa nyingi, fomu za forodha za Uzbekistan zinaonyesha, zilikuwa zikielekea Umoja wa Falme za Kiarabu, ambako maafisa wakuu wa Afghanistan wangekimbilia wakati serikali yao ilipoanguka baadaye mwaka huo. [Chanzo: Business Insider]
Marekani ilimsaidia Ashraf Ghani kukimbia Kabul pamoja na uporaji na kisha kuweka vikwazo vikali kwa Taliban kubadili sera. Tangu wakati huo, Marekani imekuwa katika eneo hilo Afghanistan na Pakistan zote zinakabiliwa na machafuko na ghasia. Njia pekee ya kutoka katika machafuko haya, ni Waislamu wa nchi zote mbili kusimamisha tena Khilafah, ambayo itakomesha utawala wa Magharibi milele.
Marekani Yatangaza Rekodi ya US $200m ya Kukuza Usawa wa Kijinsia nchini Pakistan
Baraza la Wawakilishi la Marekani linalodhibitiwa na Democrat mnamo Ijumaa lilipitisha mswada wa ufadhili wa serikali wa dolari trilioni 1.66 ambao unatoa rekodi ya dolari milioni 200 kwa usawa wa kijinsia nchini Pakistan.
Ufadhili huo uliotengwa kwa ajili ya Pakistan kwa mwaka wa fedha wa 2023 ni mara 20 zaidi ya ule uliotolewa mwaka wa 2020 wakati bunge la Marekani lilipotangaza $10m kwa usawa wa kijinsia na $15m kwa ajili ya kuimarisha demokrasia katika nchi hiyo ya Kusini mwa Asia. Pakistan iliorodheshwa ya 145 kati ya 146 kwenye fahirisi ya usawa wa kijinsia iliyotolewa na Jukwaa la Uchumi Duniani (WEF) katika Ripoti yake ya Pengo la Jinsia Duniani 2022. Mswada huo unaongeza matumizi yanayohusiana na ulinzi wa Marekani kwa asilimia 10 hadi jumla ya $858 bilioni huku $772.5 bilioni zikiwa zimetengwa kwa ajili ya programu za ndani zisizo za ulinzi.
Mswada wa matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha unaoishia Septemba 30 uliidhinishwa kwa kura nyingi za vyama za 225-201, kufuatia kupitishwa kwa Seneti siku iliyotangulia. Rais Joe Biden alisema atatia saini sheria iliyopiganiwa sana, ambayo pia inajumuisha misaada zaidi kwa wanafunzi wenye ulemavu, ufadhili wa ziada ili kulinda haki za wafanyikazi na rasilimali zaidi za mafunzo ya kazi, pamoja na nyumba za bei nafuu kwa familia, wakongwe na wale wanaotoroka ukatili wa kinyumbani. Mswada huo pia unatoa ufadhili wa juu wa kijeshi na kutuma msaada wa dharura kwa Ukraine. Nchi hiyo iliyokumbwa na vita itapata dolari bilioni 44.9 katika msaada mpya wa dharura wa Marekani. [Chanzo: Dunya News].
Pasi na kuridhika na kukuza LGBTQ plus na usawa wa kijinsia nyumbani, Marekani sasa inataka kukuza 'maadili' haya chafu nchini Pakistan. Baya zaidi, uongozi wa kijeshi na wa kiraia hadi sasa umeshindwa kupinga uendelezaji wa maadili hayo ndani ya nchi, na kwa malipo ya fedha za Marekani wataangalia njia nyengine.
Hisa za Makampuni ya Kichina ya Semiconductor Zaongezeka huku Ushindani wa Vipuri vya Chip Ukipamba Moto
Kampuni za Kichina za kutengeneza semiconductor ziko katikati ya kushamiri kwa viwango vya IPO, huku msukumo wa serikali wa kuendeleza tasnia ya kutengeneza chips nchini humo ikichota mtaji mkubwa. Kampuni zinazozalisha chips au vifaa vya kutengenezea chip zilikusanya sawa na dolari bilioni 12 kutoka kwa matoleo ya awali ya umma katika mwaka hadi Disemba 15, karibu mara tatu ya yale waliyokusanya mwaka wa 2021. Wamewasilisha maombi ya IPO nyingine zenye thamani ya $17 bilioni nchini China Bara. Haja ya wafanyibiashara wa chips za China kujenga vifua vikubwa vya vita vya kifedha imeongezeka huku Amerika ikiweka changamoto kwa dori ya China katika silsila ya usambazaji wa teknolojia ya kimataifa. Vikwazo vilivyowekwa na serikali ya Marekani vya kuuza bidhaa nje kwa China kwa chip za hali ya juu na vifaa vya kutengenezea chip mwezi Oktoba na kufanya iwe vigumu kwa makampuni ya China katika sekta hiyo kuajiri Wamarekani. Vikwazo hivyo vilikuwa hatua kutoka kwa sheria za awali, ambazo zilijumuisha orodha finyo zaidi ya teknolojia na zililenga tu mauzo ya nje kwa makampuni mahususi ya China kama vile Huawei Technologies Co. na Semiconductor Manufacturing International Corp. Kuimarishwa kwa sekta ya chips za Marekani kunaashiria kwamba China inazidi kuwa peke yake katika juhudi zake za kupatana na Marekani katika teknolojia ya hali ya juu, wachambuzi walisema. Hiyo imeongeza mafuta kwa msukumo wa serikali ya China kuendeleza tasnia ya chips nchini. Mnamo 2021, sekta ya semiconductor ilikuwa mahali maarufu zaidi kwa pesa za ubia kwani wawekezaji walisema wanafurahi kurudisha nyuma vipaumbele vya serikali ya China. Kupanda kwa uorodheshaji wa chip kunamaanisha kuwa idadi jumla ya uorodheshaji hisa (IPO) imeongezeka kidogo nchini China-tofauti kubwa na kushuka kwengineko. [Chanzo: Jarida la Wall Street]
Juhudi za China kuifikia Marekani katika mbio za chips, zinasisitiza jinsi China isivyokuwa tayarisha kupambana na ukuu wa Amerika katika eneo hilo. Isipokuwa Beijing itengeneza rundo lake la teknolojia pamoja na nia thabiti ya kisiasa, haitaweza kupambana na Marekani kwa mustakbali wa karibu.