- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Vichwa vya Habari 14/12/2022
Vichwa vya Habari:
• Ghasia Nchini Kosovo
• Xi Jinping Azuru Saudi Arabia
Maelezo:
Ghasia Nchini Kosovo
Taharuki umezuka tena huko Kosovo kaskazini huku mamia ya Waserbia wakiweka vizuizi vya barabarani kwa kutumia mashini nzito katika vivuko viwili vya mpaka na Serbia, na kuzuia magari. Haya yanajiri kutokana na mvutano wa hivi majuzi wakati Kosovo ilipoamuru madereva kusalimisha nambari zao za leseni zilizotolewa na Serbia na badala yake kuweka nambari za Kosovo. Hii sasa imesababisha Waserbia wanaoishi kaskazini mwa Kosovo kuweka vizuizi na kusababisha makabiliano na wakaazi wa Kosovo. Katika miaka ya 1990, kulikuwa na vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe kati ya makabila tofauti katika Balkan na kusababisha mauaji ya kikabila na vifo vya Waislamu zaidi ya 100,000. Waserbia walifunga ili kupanua eneo lao na kujaribu kupanua hadi Kosovo, ambayo ilisababisha Marekani kuingilia kati na kufanya mashambulizi ya mabomu katika mji mkuu wa Serb Belgrade. Makubaliano ya mwisho ya kusitisha vita na mkataba wa amani yalishuhudia Kosovo kupata uhuru na kutoaminiana sana na Marekani ambayo ilipanga makubaliano na Waserbia na Urusi. Kwa Waserbia wengi, Kosovo ni eneo lao na haikupaswa kufanywa kuwa huru. Ijapokuwa moto wa sasa ni juu ya nambari za usajili wa magari, katika Balkan, ambapo Vita vya Kwanza vya Dunia vilianza, hili si jambo dogo.
Xi Jinping Azuru Saudi Arabia
Waziri Mkuu wa China Xi Jinping alimaliza safari ya siku tatu, kuanzia tarehe 8 Disemba kwenda Saudi Arabia, kwa fahari kubwa, sherehe ya kuanza kile alichokiita "enzi mpya" katika uhusiano wa Saudi na China. Safari ya Xi iliangaziwa pakubwa na vyombo vya habari vya kilimwengu huku wengi wakiamini kuwa China ni dola mpya katika Mashariki ya Kati. Ziara ya Xi inakuja katika muktadha wa mvutano na Marekani kuhusu Taiwan na pia mvutano mkubwa kati ya kiongozi wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman (MBS) na Rais Joe Biden. Hata hivyo, mbali na kauli na simulizi, ziara ya Xi haikubadilisha uhalisia wa kimkakati wa China katika Mashariki ya Kati kwani uhusiano wake na Saudi Arabia na eneo pana unabaki kuwa wa kawaida. Saudi Arabia na China zilionyesha uhusiano wa kina kwa msururu wa mikataba. Viongozi hao wa China pamoja na Saudi walitia saini "mkataba wa ushirikiano wa kimkakati wa kina" ambao ulijumuisha makubaliano juu ya kawi ya hidrojeni na kuimarisha uratibu kati ya Ruwaza ya Ufalme huo ya 2030 na Mradi wa Ukanda wa Barabara wa China. Makubaliano pia yalipatikana kuhusu Huawei Technologies yanayohusiana na ‘cloud computing’, vituo vya data na ujenzi wa miundo ya hali ya juu. Sababu muhimu zaidi ya China ya kuwepo Mashariki ya Kati ni kawi. Mashariki ya Kati itasalia kuwa chanzo kikuu cha China cha kuagiza mafuta na huo ndio umuhimu wa kimkakati wa Mashariki ya Kati na Saudi Arabia, muuzaji mkuu wa mafuta kwa China. Ushiriki wa China kiuchumi katika Mashariki ya Kati umeongezeka zaidi ya miaka kumi iliyopita, ushiriki wake wa kijeshi na usalama hata hivyo unabakia kuwa mdogo. Mkakati wa China kwa Mashariki ya Kati unajulikana zaidi kama ule wa dragon mwenye tahadhari: ikiwa makini kujihusisha kibiashara na eneo hilo na kubaki na maelewano mazuri na dola zote za Mashariki ya Kati, lakini ikisita zaidi kuimarisha ushirikiano wake, ikiwemo kuimarisha shughuli zake za kidiplomasia na usalama zaidi ya kiwango cha chini kinachohitajika ili kupata pesa na kuhakikisha mtiririko wa kawi.