- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Vichwa vya Habari: 30/11/2022
Vichwa vya Habari:
• Maandamano Nchini China
• Pakistan Yaitazama Urusi kwa Ajili ya Kawi
• Chini ya Nusu ya Idadi ya Watu Uingereza ni Wakristo, Sensa ya 2021 yaonyesha
• Urusi Yatoa Wito wa Muungano wa Gesi Pamoja na Asia ya Kati
Maelezo:
Maandamano Nchini China
Maandamano ya umma nchini China yanayohusiana na vizuizi vya serikali vya Covid-19 yamegonga vyombo vya habari vya kimataifa kufuatia moto mbaya wa ghorofa moja huko Urumqi, Xinjiang ambao uliua watu kumi. Maandamano yalizuka katika miji kote China kulingana na video zilizochapishwa kwenye Weibo na Twitter za China. Raia kote China walilaumu vifo hivyo kutokana na kushindwa kwa huduma za zimamoto na uokoaji kufikia jengo hilo kwa sababu ya vizuizi vya COVID-19. Maandamano yalianza Urumqi na kufuatiwa na maandamano katika miji mingine kadhaa ya China - ikiwemo Shanghai, Beijing, Wuhan, Guangzhou, Chengdu, Lanzhou na Xi'an. Maandamano mengi yalijumuisha mamia ya watu, mengine yakijumuisha maelfu, na yote yalionekana kulenga kuifanya serikali kurahisisha au kusimamisha sera yake ya "zero-COVID", huku baadhi ya watu wakitaka uhuru na kupinduliwa kwa Xi Jinping na chama cha Kikomunisti cha China.
Hatua za China za Covid ni miongoni mwa kali zaidi ulimwenguni, kwani inaendelea na ufungaji miji ili kukandamiza virusi hivyo - kile inachokiita sera ya "nguvu sufuru ya Covid". Maandamano hayo kwa kweli ni maandamano ya mabarabarani ambapo waandamanaji hutawanyika baada ya kuandamana na kulaani, na lengo kuu la maandamano hayo ni vizuizi vya Covid badala ya kanuni pana za kisiasa. Suala kuu hapa ni kufazaika sio tu na vizuizi vya Covid lakini njia zisizo sawa ambazo hatua hizi zinatekelezwa.
Pakistan Yaitazama Urusi kwa Ajili ya Kawi
Waziri wa petroli wa Pakistan alitembelea Urusi ili kuandika makubaliano juu ya mafuta na gesi. Safari hiyo inajiri huku taifa la Pakistan likijitahidi kukidhi mahitaji ya usambazaji wa gesi majumbani wakati majira ya baridi yanapokaribia huku likipambana kudhibiti nakisi ya sasa ya akaunti iliyochangiwa na malipo ya nishati, hasa mafuta. Katika mkutano huo, Waziri Mkuu Shehbaz Sharif alisema kuwa Pakistan imejitolea kupanua ushirikiano na Urusi katika maeneo yote ya manufaa ya pande zote ikiwemo usalama wa chakula, biashara na uwekezaji, nishati, ulinzi na usalama. Kulingana na vyanzo, Pakistan itaokoa zaidi ya dolari bilioni 2 kila mwaka katika kesi ya utekelezaji wa miradi ya nishati na Urusi ambapo ununuzi wa bidhaa za petroli kutoka Moscow utapunguza shinikizo kwenye akiba ya fedha za kigeni. Mnamo Oktoba, Balozi wa Pakistan jijini Moscow Shafqat Ali Khan alifichua kwamba Islamabad pia ilikuwa ikitafuta mahitaji ya gesi asilia (LNG) kutoka Moscow. Kutokana na kupungua kwa hifadhi ya gesi ya ndani, nchi imeanza kutoa mgao kwa watumiaji wa nyumbani na biashara. Vyombo vya habari vya ndani pia vimeripoti kuwa mahitaji ya mafuta yanabaki kuwa duni kutokana na ugumu wa kulipia bidhaa kutoka nje.
Chini ya Nusu ya Idadi ya Watu Uingereza ni Wakristo, Sensa ya 2021 yaonyesha
Kwa mara ya kwanza chini ya nusu ya watu nchini Uingereza na Wales wanajitaja kama Wakristo, Sensa ya 2021 imefichua. Idadi ya watu waliosema kuwa ni Wakristo ilikuwa 46.2%, chini kutoka 59.3% ya sensa iliyopita ya 2011. Tofauti na idadi ya waliosema hawana dini iliongezeka hadi 37.2% ya idadi ya watu, hii ni 4 kati ya watu 10. Wale waliojitambulisha kuwa Waislamu walipanda kutoka 4.9% mwaka wa 2011 hadi 6.5% mwaka wa 2021. Matokeo haya ya sensa yanafichua mambo mengi kuhusu Uingereza. Dori ya dini imepungua sana kwa miongo kadhaa, licha ya urithi wa Kikristo wa Uingereza. Wale wasio na dini wanaongezeka na watakuwa na athari kubwa kwa sheria na mwelekeo wa mustakbali wa Uingereza. Licha ya angazo lote wanalopokea Waislamu na Uislamu, kwa jumla wao ni milioni 4 tu kati ya jumla ya watu milioni 67 wa Uingereza. Idadi ndogo zaidi kuliko hadith zote za Uingereza kuwa imemezwa au Waislamu kuichukua nchi.
Urusi Yatoa Wito wa Muungano wa Gesi Pamoja na Asia ya Kati
Urusi, Kazakhstan na Uzbekistan zinajadili muungano wa gesi kwa mahitaji ya ndani na kwa masoko ya nchi za tatu, ikiwemo China, Naibu Waziri Mkuu wa Urusi Alexander Novak aliwaambia waandishi wa habari. Msemaji wa Rais wa Kazakh Kassym-Jomart Tokayev alisema juu ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kupendekeza wazo kama hilo katika mkutano na Tokayev hivi karibuni. Wakati Urusi ni muuzaji mkuu wa gesi asilia, Uzbekistan na Kazakhstan huzalisha takriban zaidi ya vile wanavyotumia. Nchi hizo mbili zimeunganishwa kwa bomba la gesi hadi Urusi, na bomba tofauti huvuka zote mbili likielekea China. Tangu Urusi ilipoivamia Ukraine, nchi za magharibi zimeiwekea vikwazo na hii inailazimu Urusi kutafuta watumiaji mbadala na walio tayari. Huku mapato ya nishati ya Urusi yakiongezeka, hii ni kwa sababu ya bei ya juu ya mafuta, kwani viwango vyake vya usafirishaji nje vimepungua na Urusi inajua kwa muda mrefu inakabiliwa na changamoto kubwa za kawi.