- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Vichwa vya Habari 24/08/2022
Vichwa vya Habari:
- Japan Kutuma Makombora ya Masafa Visiwani dhidi ya China
- China Kusamehe Madeni ya Afrika
- Pakistan Yatafuta Mikopo
Maelezo:
Japan Kutuma Makombora ya Masafa Visiwani dhidi ya China
Japan inazingatia kutuma makombora 1,000 ya masafa marefu ili kuongeza uwezo wake wa kukabiliana na China. Makombora hayo yatakuwa yale yaliyo karabatiwa ili kupanua masafa yake kutoka kilomita 100 (maili 62) hadi kilomita 1,000. Silaha hizo, zinazorushwa na meli au ndege, zitawekwa karibu na Visiwa vya Nansei vilivyo kusini na kuweza kufika maeneo ya pwani ya Korea Kaskazini na China, gazeti la Yomiuri lilisema. Japan, ambayo inatafsiri katiba yake ya baada ya vita iliyoacha vita kumaanisha kuwa huenda ikatumia jeshi lake kwa kujilinda pekee, imeongeza matumizi yake kwa jeshi na kuchukua mkakati wa udhibiti zaidi katika miaka ya hivi karibuni. Lakini imejiepusha na kutuma makombora ya masafa marefu, miongoni mwa vidhibiti vyake kwa silaha zinazoweza kulenga shabaha katika ardhi ya kigeni. Kwa kuongezeka kwa uungaji mkono wa China na Amerika, Japan imekuwa ikijipanga tena kisilaha kwa kile kitakacho kuwa ushindani ujao kati ya dola kuu China na Amerika. Japan imeweka mayai yake imara katika kambi ya Marekani.
China Kusamehe Madeni ya Afrika
China, mkopeshaji mkuu wa serikali kwa nchi zinazoibukia kiuchumi, ilisema itasamehe mikopo 23 isiyo na riba kwa nchi 17 za Afrika na kuelekeza dolari bilioni 10 za akiba yake ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa kwa mataifa ya bara hilo. Waziri wa Mambo ya Nje Wang Yi alitangaza kufutilia mbali huko katika mkutano mmoja wiki iliyopita wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika, kwa mujibu wa chapisho kwenye tovuti ya wizara hiyo. Haikutoa maelezo kuhusu thamani ya mikopo hiyo ambayo ilisema ilikomaa mwishoni mwa 2021, wala haikueleza ni mataifa gani yanadaiwa pesa hizo. Tangu 2000, Beijing imetangaza awamu nyingi za msamaha wa deni la mikopo isiyo na riba kwa nchi za Afrika, na kufutilia mbali angalau $ 3.4 bilioni ya deni hadi 2019, kulingana na utafiti uliochapishwa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins Shule ya Mafunzo ya Juu ya Kimataifa. Deni lililofutiliwa mbali lilikuwa ni kwa mikopo ya misaada ya nje, iliyo komaa, na isiyo na riba, huku Zambia ikipokea ufutiliwaji mkubwa zaidi katika kipindi hicho. Hata hivyo, idadi kubwa ya mikopo ya hivi majuzi ya China barani Afrika kama vile mikopo ya masharti nafuu na mikopo ya kibiashara haijawahi kuzingatiwa kufutiliwa mbali, ripoti hiyo iliongeza, ingawa baadhi yake imefanyiwa marekebisho. China imetumia ufutaji wa mikopo kama chombo cha kujenga uhusiano na nchi zinazoendelea, aghlabu mikopo yake huwa na masharti rahisi zaidi kuliko taasisi za kimagharibi ambazo mikopo yao hutazamwa kama aina ya ukoloni.
Pakistan Yatafuta Mikopo
Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif katika wiki hii alikuwa akitafuta usaidizi wa kiuchumi na mikataba ya nishati ili kusaidia kupunguza baadhi ya matatizo katika uchumi wa Pakistan. Qatar, Saudi Arabia na Imarati za Kiarabu kwa pamoja zitatoa msaada wa dolari bilioni 4 katika mwaka ujao, huku Mfuko wa Fedha wa Kimataifa utaamua katika siku zijazo ikiwa utaidhinisha mkopo wa dolari bilioni 1.2 kwa Pakistan. Serikali ya mseto inayoongozwa na Pakistan Muslim League-Nawaz (PML-N) ilichukua uamuzi wa kuondoa ruzuku kwa bidhaa za petroli na kuanza kukusanya ushuru wa maendeleo ya mafuta ya petroli (PDL) kwa bidhaa za petroli ili kujishindia mpango wa mkopo. Ucheleweshaji wa muda mrefu wa kuanza tena kwa mpango wa IMF na ukosefu wa utulivu wa kisiasa ulishusha thamani ya sarafu ya nchi kwa 13.75% (au Rs 31.31) hadi kiwango cha chini kabisa cha Rs 240 dhidi ya dolari tangu katikati ya Aprili. Mnamo siku ya Jumatatu, rupia ilifunga siku kwa Rs 216.66 kwa dolari moja.