Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 07/10/2021

Vichwa vya Habari:

  • Viongozi wa Muungano wa Ulaya Watafuta Umoja wa Namna ya Kuikabili China na Amerika
  • Balozi wa Amerika Kufanya Mazungumzo Muhimu juu ya Kadhia ya Afghan
  • Taipei Aonya Kwamba China Itaweza Kuivamia Taiwan Kufikia 2025

Maelezo:

Viongozi wa Muungano wa Ulaya Watafuta Umoja wa Namna ya Kuikabili China na Amerika

Viongozi wa EU watakuwa na majadiliano magumu juu ya nafasi ya Ulaya ulimwenguni mnamo siku ya Jumanne huku wakitafuta umoja juu ya jinsi ya kushughulikia mafungano na dola kuu za China na Amerika. Wakuu wa nchi na serikali 27 wanatarajiwa kukusanyika kwenye Kasri la Brdo katika jamhuri ya zamani ya Yugoslavia ya Slovenia, nchi ambayo kwa sasa inashikilia urais wa EU unaozunguka. Huku matokeo madhubuti yakiwa hayatarajiwi kutoka kwa mkutano huo, "hii ndio mara ya kwanza kwa viongozi kukutana tangu Juni, na kwa kila kitu kilichotokea, hiyo inaonekana kana kwamba ni miaka mingi iliyopita", mwanadiplomasia mwandamizi wa EU alisema. Hafla ya chakula cha jioni itafanyika mkesha wa kuamkia mkutano wa EU wa Magharibi mwa Balkan ambao nchi za kambi ya mashariki zitatafuta hakikisho siku moja ya kujiunga na Jumuiya ya Ulaya. Katika chakula hicho cha jioni, viongozi watakuwa na "majadiliano ya kimkakati juu ya dori ya Muungano katika hatua ya kimataifa", kwa mujibu wa barua ya mwaliko iliyotumwa na mkuu wa Baraza la EU Charles Michel, waziri mkuu wa zamani wa Ubelgiji ambaye huandaa mikutano. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anatarajiwa kuwaonya tena washirika wake kwamba utiifu wa karibu wa Washington kwa Ulaya hautolewi tena, huku Paris ikiwa bado ina machungu ya kubatilishwa kwa mkataba mkubwa wa nyambizi kwa manufaa ya Amerika. "Itakuwa makosa kujifanya kana kwamba hakuna kilichotokea," kilisema chanzo cha afisi ya rais wa Ufaransa kabla ya mazungumzo hayo. Ufaransa ilikasirika mwezi uliopita wakati Australia ilighairi makubaliano ya  nyambizi za Ufaransa zenye thamani ya mabilioni ya dolari, ikisema itafuata mitazamo ya kinyuklia ya Amerika huku taharuki ikiongezeka kwa China. Washirika wa EU wameelezea mshikamano na Paris kwa viwango tofauti, na nchi za Baltic na Nordic zikisita kukosoa dola kuu ya Vita Baridi ambayo wanaiona kama mlinzi wao wa mwisho dhidi ya Urusi. Chansela wa Ujerumani Angela Merkel, kiongozi mwenye ushawishi mkubwa wa EU kwa muda wa miaka 15 iliyopita, atahudhuria huku mazungumzo ya muungano yakisonga mbele kwa shubiri kadhaa huko Berlin ili kuja na serikali ambayo itachukua nafasi yake. Mkakati wa tahadhari wa Merkel, unaounga mkono Amerika umeitawala Ulaya na kuondoka kwake karibu kutasababisha viongozi kama Macron, Mario Draghi wa Italia na Waziri Mkuu wa Uholanzi Mark Rutte watafute kuweka alama yao. Kama kiongozi wa Ujerumani, kituo cha usafirishaji nguvu nje cha EU, Merkel pia amehimiza uhusiano wa karibu na China, lakini hili pia limethibitika kuwa vigumu kulitetea huku uongozi wa Rais wa China Xi Jinping ukigeuka kuwa mgumu na mkali zaidi. Uhusiano na Beijing umekuwa mgumu zaidi wakati dili moja ya uwekezaji kati ya EU na China iliyokuwa ikitakiwa na Ujerumani ilisitishwa kwa muda usiojulikana baada ya pande zote mbili kubadilishana vikwazo vya kulipizana juu ya namna Waislamu wachache wa Uyghur walivyoamiliwa nchini China. [Chanzo: France24]

Ulaya haitaweza kupata msimamo wa umoja juu ya Amerika na China, isipokuwa muungano huo utakapokabiliana na nguvu mgawanyiko zinazotishia kuharibu mradi huo wa EU. Urusi, Uingereza na Amerika zinatafuta EU iliyogawanyika pamoja na harakati za upande wa mbali wa kulia barani kote. Usitishaji nguvu hizi ni lazima kabla ya msimamo wa umoja juu ya Amerika na China kuzungumziwa.

Balozi wa Amerika Kufanya Mazungumzo Muhimu juu ya Kadhia ya Afghan

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Amerika Wendy Sherman awasili jijini Islamabad mnamo siku ya Alhamisi kwa mazungumzo yaliyolenga kuziba mzozo unaokua kati ya Amerika na Pakistan juu ya suala la Afghanistan. Vyanzo vya kidiplomasia jijini Washington vilibainisha kuwa hii itakuwa muhimu na "ziara ya Amerika ya kiwango cha juu kabisa hadi sasa chini ya utawala wa Biden." Bi Sherman ndiye afisa mkuu zaidi katika Wizara ya Mambo ya Nje baada ya Waziri wa Mambo ya Nje Antony Blinken. "Ziara hiyo inafanyika katika wakati muhimu sana, katika muktadha wa Afghanistan na maendeleo katika eneo hilo zima," kilisema chanzo kimoja kikuu cha kidiplomasia kilipoulizwa kuelezea ni kwa nini Islamabad inaiona hii kama ziara muhimu. Chanzo hicho kilisema kwamba uongozi wa Biden "haukuonekana kusita kusafiri kwenda India na Pakistan kwa mara moja, ambayo ndio iliyokuwa hali hapo zamani." "Ziara hiyo inafanyika katika wakati muhimu sana, katika muktadha wa Afghanistan na maendeleo katika eneo zima," kilisema chanzo kimoja kikuu cha kidiplomasia kilipoulizwa kuelezea ni kwa nini Islamabad inaiona hii kama ziara muhimu. Chanzo hicho kilisema kwamba uongozi wa Biden "haukuonekana kusita kusafiri kwenda India na Pakistan kwa mara moja, ambayo ndio iliyokuwa hali hapo zamani." "Hii ni ziara muhimu, na tunatarajia kushirikiana na Naibu Waziri Sherman," Balozi wa Pakistan Asad Majeed Khan aliiambia Dawn. "Pamoja, tutafuta njia za kuimarisha na kupanua ushirikiano wetu wa pande mbili katika maeneo ya maslahi ya pamoja na kujaliana." Kulingana na vyanzo hivi, utawala wa Biden unazingatia hoja nne kuu katika mazungumzo yake na Pakistan, kutambuliwa kwa serikali ya Taliban jijini Kabul, vikwazo vya kimataifa dhidi ya Afghanistan, uingiaji Afghanistan na ushirikiano wa kupambana na ugaidi. Vyanzo hivyo vinasema kuwa Amerika haitaki Pakistan iutambue utawala wa Taliban kabla ya jamii yote ya kimataifa. Badala yake, inataka Pakistan iendelee na juhudi zake za kulainisha msimamo wa Taliban juu ya maswala yenye utata, kama vile utawala shirikishi, haki za binadamu, elimu ya wasichana na kuruhusu wanawake kufanya kazi. Waamerika wanaamini kuwa mabadiliko ya msimamo juu ya maswala haya yanaweza kuwa na athari nzuri kwa picha ya Taliban na kufungua njia ya kukubalika kwao katika Umoja wa Mataifa. Mataifa kama Pakistan, yanapaswa kuchelewesha utambuaji wao hadi wakati huo. [Chanzo: Dawn]

Amerika imeitumia Pakistan kuitegemea Taliban kuchukua mamlaka. Sasa Amerika inataka matakwa ya Biden. Je! Ni lini uongozi wa kiraia na kijeshi wa Pakistan utakomesha utumwa wake kwa Amerika? Miongo kadhaa ya utiifu kwa sera ya kigeni ya Amerika imedhoofisha ubwana wa kieneo wa Pakistan, na zaidi ya hayo  itasababisha matatizo zaidi kwa Pakistan kuitumia Pakistan ili kuhakikisha kuwa mtego wa kisiasa nchini Afghanistan unaendelea barabara.

Taipei Aonya Kwamba China Itaweza Kuivamia Taiwan Kufikia 2025

Waziri wa ulinzi wa Taiwan ameonya kuwa China itakuwa na uwezo kamili wa kukivamia kisiwa hicho ifikapo mwaka 2025, katika ujumbe wa kwanza wazi wa serikali kwa umma kwamba nchi hiyo inakabiliwa na tishio la vita. Chiu Kuo-cheng alitoa onyo hilo baada ya karibu ndege 150 za kivita za China kuendeshwa katika anga ya kimataifa karibu na Taiwan kati ya Ijumaa na Jumatatu. "Hali ya sasa ni hatari zaidi ambayo nimeona katika zaidi ya miaka 40 katika jeshi," Chiu alisema katika kikao cha maswali na majibu na wabunge kuhusu Bajeti maalum ya ulinzi ya NT $ 240 bilioni ($ 8.6 bilioni) makombora ya meli na meli za kivita." Ikiwa wanataka kushambulia sasa, tayari wana uwezo. Lakini lazima wahesabu itagharimu kiasi gani na matokeo yatakuwa ni gani,” Chiu alisema. "Kuanzia 2025, watakuwa tayari wameshusha gharama na hasara kwa kiwango cha chini kabisa, kwa hivyo... watakuwa na uwezo kamili.” Maneno hayo yanafuata maombi ya Taipei kwa jamii ya kimataifa kuisaidia nchi hiyo dhidi ya uvamizi wa Wachina. Mnamo Jumanne Tsai Ing-wen, raisi, alitoa ombi la dharura la kusimama na Taiwan. Nchi nyengine za kidemokrasia "zinapaswa kukumbuka kwamba ikiwa Taiwan itaanguka, matokeo yatakuwa mabaya kwa amani ya eneo na mfumo wa muungano wa kidemokrasia. Itaashiria kuwa katika kinyang'anyiro cha leo cha kiulimwengu cha maadili, utawala wa kimabavu kitakuwa na nguvu juu ya demokrasia," aliandika katika Mambo ya Nje. Katika mwaka uliopita, Beijing imeongeza kwa kasi shughuli za anga na majini karibu na Taiwan. Kulingana na wizara ya ulinzi ya Taiwan, ndege za kivita za Wachina 672 zimeruka katika ukanda wa kitambulisho cha ulinzi wa angani wa Taiwan mwaka huu, ikizidi 380 zilizorekodiwa mnamo 2020. Maafisa wengine wa Amerika na wataalam wengi wamepuuzia umuhimu wa ndege za Jeshi la Ukombozi wa Watu, wakisema kuwa sio mwanzo wa vita lakini walilenga kutisha Taiwan na kuvunja jeshi lake la angani, ambalo hujibu kwa kuwashambulia wapiganaji. Tiffany Ma, mtaalam wa Taiwan katika Bower Group Asia, shirika la ushauri, alisema ilikuwa mapema sana kupiga kengele za tahadhari. "Ukweli kwamba China huenda ikawa na uwezo chini ya mandhari na hali maalum haimaanishi kwamba nia hiyo iko," alisema Ma. "Kwa PLA kuchukua Taiwan kijeshi, itakuwa gharama kubwa sana. China inaunda zana kubwa za njia za kuishinikiza Taiwan kabla ya kufyatua risasi na kuipandisha hadi kiwango cha msukumo." Lakini, kuna wasiwasi jijini Washington. Mnamo Machi Admiral Philip Davidson, wakati huo akiwa mkuu wa kikosi cha Amerika eneo la Indo-Pacifiki, aliliambia Bunge kwamba China inaweza kuishambulia Taiwan ndani ya miaka sita. Makamanda wengine pia wameelezea kibinafsi kwamba China inaweza kuchukua hatua haraka zaidi kuliko wataalam wengi wa jeshi la China wanavyoamini. Lakini serikali ya Taiwan imekuwa na hofu kwa muda mrefu kuwa majadiliano juu ya kujiandaa kwa shambulizi la Wachina yatadhoofisha ari ya umma. Maafisa na wataalamu wa Amerika mara kwa mara wamemkosoa Taipei kwa kutoridhika na kufanya machache mno kuimarisha ulinzi wake. [Chanzo: Financial Times].

Suala sio kwamba China ina uwezo wa kijeshi kuichukua tena Taiwan au la. Suala halisi linahusiana na utayari wa China wa kuikamata Taiwan. Leo, China haina dhamira ya kisiasa ya kupambana na Amerika, na hii itabaki kuwa ndio hali kwa muda mrefu.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu