- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Umbile la Kigaidi la Kizayuni Limeufanya Ukingo wa Magharibi kuwa Makaburi ya Watoto kama vile Gaza, Huku Majeshi ya Nchi za Waislamu Yakitazama
(Imetafsiriwa)
Habari:
Mnamo tarehe 7 Februari, shirika la ‘Save the Children’ liliripoti kwamba watoto wasiopungua 224 wameuawa katika Ukingo wa Magharibi na wanajeshi au walowezi wa Kizayuni tangu Januari 2023, mdogo zaidi akiwa na umri wa miaka 2 pekee. Kulingana na Umoja wa Mataifa, watoto 171 waliuawa katika Ukingo wa Magharibi tangu tarehe 7 Oktoba 2023 - sawia na karibu 1 kila siku. Hakuna mwanajeshi wa Kizayuni aliyefunguliwa mashtaka au kuwajibika kwa mauaji haya. Afisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ilisema kuwa kumekuwa na ongezeko la mara 20 la idadi ya watoto wa Kipalestina waliouawa na mashambulizi ya anga ya umbile la Kiyahudi katika Ukingo wa Magharibi katika miaka ya hivi karibuni. Shirika la ‘Defence for Children International Palestine (DCIP)’ liliripoti kwamba mtoto wa miaka 10 Saddam Hussein Iyad Mohammad Rajab alipigwa risasi ya tumbo wakati wa kuvamia Tulkarem na uvamizi mnamo tarehe 28 Januari na sasa yuko katika hali mbaya katika hospitali ya Nablus. Vikosi vya Kizayuni pia vilimshambulia babake Saddam, kumtandika na kumpiga ngumi alipokuwa akijaribu kumbeba mwanawe ili kupokea msaada wa matibabu. Wakati wa uhamisho kati ya hospitali, wanajeshi wa uvamizi waliinua gari la wagonjwa ambalo Saddam alikuwa amewekwa, na mmoja akimwambia baba yake, "Mimi ndiye niliyempiga risasi mwanao. Mungu akipenda atakufa." Mnamo tarehe 26 Januari, Laila Al-Khatib mwenye umri wa miaka 2 alipigwa risasi ya kichwa na risasi za mdenguaji wa uvamizi akiwa nyumbani kwake katika kijiji cha Al-Shuhada, kusini mwa Jenin. Na tarehe 1 Februari, iliripotiwa kuwa Ahmad al-Sadi mwenye umri wa miaka 16 alikuwa miongoni mwa Wapalestina 5 waliouawa na shambulizi la anga la Wazayuni ambalo lilipiga kundi la watu mitaani huko Jenin. Baadaye, shambulizi la droni liligonga gari huko Qabatiya, na kuua vijana 2, na dakika chache baadaye, shambulizi jengine la droni huko Jenin liliua vijana 2 zaidi waliokuwa kwenye pikipiki.
Maoni:
Siku chache tu baada ya kutangazwa usitishaji vita huko Gaza, umbile la mauaji la Kizayuni lilianzisha kampeni yake ya "Ukuta wa Chuma" kwa mashambulizi ya mauaji huko Jenin, Tulkarem, Nablus na miji mingine ya Ukingo wa Magharibi, ambapo watoto walikuwa walengwa halali wa vikosi vya uvamizi, kama walivyokuwa huko Gaza. Hakika, uvamizi huu wa kikatili umeruhusiwa kuwachinja watoto wadogo na wachanga bila kuadhibiwa kabisa, bila serikali au dola kuingilia kati kukomesha mauaji haya ya kiholela. Ayed Abu Eqtaish, mkurugenzi wa programu ya uwajibikaji katika DCIP, alisema, "Vikosi vya Israel vimedharau sana maisha ya watoto wa Kipalestina kwani vinalenga kwa makusudi watoto kwa risasi za moto bila uwajibikaji." Haya yote bila shaka yanaambatana ukamataji wa kuendelea na maarufu, kuwekwa kizuizini na kuteswa kwa kimpangilio kwa watoto katika jela za Kizayuni ambayo yamekuwa yakiendelea kwa miongo kadhaa. Ni wazi kwamba mkataba wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za mtoto na sheria zote za kimataifa kuhusu ulinzi wa watoto ni batili linapokuja suala la watoto wa Kipalestina!
Uvamizi huo wa kigaidi wa Kizayuni unaiga katika Ukingo wa Magharibi kile walichokifanya huko Gaza karibu vilevilw - mauaji ya halaiki, kuwekwa kizuizini kiholela, kuziangusha chini nyumba za makaazi, kulipuliwa mabomu nyumba na uharibifu wa miundombinu muhimu, na kusababisha makumi ya maelfu ya watu kuyahama makaazi yao. Mwaka 2024, vikosi vya Kizayuni vilifanya mashambulizi 152 ya anga katika Ukingo wa Magharibi. Meya wa Jenin, Mohammad Jarrar, alisema, "Jeshi la Israel liliwalazimisha takriban wakaazi 15,000 wa kambi kuhama. Wamebomoa, kuchoma, na kulipua zaidi ya nyumba 100 tangu operesheni hiyo ilipoanza... Pia kumekuwa na usambaratishaji mkubwa wa mitaa na uharibifu wa maji, umeme, maji taka, na mitandao ya mawasiliano" ikiongeza “Kilicho kipya katika operesheni ya kijeshi ni kuhamishwa kwa wengi wakaazi wa kambi ya Jenin.” Kwa kuongezea, ripoti mpya ya Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) ilielezea mfumo wa huduma ya afya katika Ukingo wa Magharibi kama "hali ya dharura ya kudumu" tangu Oktoba 2023, na kwamba "Ongezeko kubwa la ghasia, lililosababishwa na uvamizi wa kijeshi wa Israel na vizuizi vikali vya matembezi ... imezuia sana ufikiaji wa huduma muhimu, haswa huduma nyingi za afya, ambazo tayari zinazidisha hali ya maisha ya Wapalestina kuwa mbaya zaidi."
Ni wazi kwamba uvamizi wa Kizayuni, unaosaidiwa na kuungwa mkono na serikali ya Marekani, unalenga sio tu kuwaondoa wakaazi wa Gaza kutoka katika ardhi yao, bali pia kuiunganisha Palestina yote na umbile lake halifu. Tunawauliza wale walio katika majeshi ya Waislamu, ambao wana uwezo wa kung'oa uvamizi huu na kukomesha mauaji haya ya halaiki na mauaji ya kimbari - wanawezaje kutazama huku Palestina nzima ikigeuka kuwa makaburi ya watoto wake? Vipi watabaki kwenye kambi zao huku wakiitazama Al Aqsa na ardhi ya Al-Isra wal Miraj ikinajisiwa siku baada ya siku na ndugu na dada zao wa Kipalestina wakichinjwa na kufukuzwa majumbani mwao? Je, watamwambia nini Mola wao (swt) atakapowauliza kwa nini waliutelekeza Ummah wao na Ardhi Iliyobarikiwa ya Al Aqsa?
Je, wana majibu gani kwa Maneno ya Mwenyezi Mungu (swt),
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انفِرُواْ فِي سَبِيلِ اللّهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الأَرْضِ أَرَضِيتُم بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الآخِرَةِ إِلاَّ قَلِيلٌ]
“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache.” [At-Taubah: 38].
Enyi wana wa majeshi ya Waislamu! Mnangoja nini kabla ya kusonga kuwatetea kaka, dada na watoto wenu wa Palestina? Je, hamujaona kwamba leo hakuna serikali, dola au kiongozi mwenye dhamira ya kisiasa ya kulinda maisha ya Waislamu iwe Palestina, Kashmir, Myanmar au kwengineko? Hamjashuhudia jinsi watawala na tawala hizi mnazozitumikia zinavyocheza tu wimbo inaochezwa na mabwana zao wa kimagharibi, ikiwemo kulinda umbile la Kizayuni kwa kuhalalisha mahusiano na makubaliano yao ya amani? Je, haiko wazi kwamba Palestina haitakombolewa kamwe na kulindwa watu wake isipokuwa tawala hizi za khiyana zing'olewe na kubadilishwa kwa uongozi wa Kiislamu wa Mfumo wa Mwenyezi Mungu (swt), dola ya Khilafah - mlinzi na ngao ya Waislamu kama alivyoeleza Mtume wetu (saw)? Kwa hivyo, tunakulinganieni musichelewe tena na mutoe Nusrah yenu (msaada wa kimada) kwa ajili ya kusimamisha dola hii tukufu ya Khilafah ambayo itakuhamasisheni bila kuchelewa kuung'oa uvamizi huu wa saratani milele, mulinde Ummah wenu na muregeshe mamlaka na nuru ya Uislamu kwenye Ardhi hii Iliyobarikiwa!
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Asma Siddiq
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir