Jumamosi, 23 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Moscow Yaongeza Ushawishi wake eneo la Asia ya Kati

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 24 Mei, shirika la habari la Sputnik Kyrgyzstan liliripoti: “Mkutano wa 54 wa Baraza la Wakuu wa Vyombo vya Usalama na Huduma Maalumu za nchi za CIS ulifanyika leo jijini Bishkek. Mkutano huo ulifunguliwa na Kamchybek Tashiev, Mwenyekiti wa SCNS wa Kyrgyzstan.

Alexander Bortnikov, mkuu wa Huduma ya Usalama ya Shirikisho la Urusi, alifuatia kuzungumza. Alitoa kauli kadhaa kama vile: nchi zinazozungumza Kiingereza (anglo-Saxons) zinataka kupata nafasi katika Asia ya Kati kwa njia yoyote ile; Marekani, Uingereza, washirika wao wa NATO katika jitihada za kudumisha utawala wa kimataifa wanatumia safu nzima ya vita vya mseto dhidi ya dola huru ambazo hazikubaliani na sera yao; Ujasusi wa kijeshi wa Ukraine unahusika moja kwa moja katika shambulizi la kigaidi huko Crocus.”

Sergei Naryshkin, Mkurugenzi wa Huduma ya Ujasusi wa Kigeni wa Urusi, pia alizungumza. Hasa alisema kuwa: “Magharibi inatumia mashirika ya kigaidi kwa malengo yake; shambulizi la kigaidi huko Crocus ni moja ya viungo katika silsila hiyo katika juhudi za maadui za kuvuruga hali ya utulivu nchini Urusi na kuvuruga maelewano ya makabila katika CIS; vipote vya Wamagharibi wako katika hali fulani ya kuchanganyikiwa - wamegundua kuwa mpango wa kimkakati kwenye uwanja wa vita umepitishwa kikamilifu hadi Urusi.

Maoni:

Haikuwa kwa bahati kwamba Moscow ilipanga na kufanya mkutano huo wa wakuu wa huduma maalum za CIS huko Kyrgyzstan. Kama kawaida, walijadili usalama, kukabiliana na itikadi kali na ugaidi. Walikumbuka shambulizi la kigaidi katika Ukumbi wa Jiji la Crocus. Lakini dhidi ya muktadha wa vita vya muda mrefu nchini Ukraine na kuongezeka kwa Magharibi huko Asia ya Kati, Moscow ilitaka kuonyesha kila mtu kwamba bado inadhibiti hali katika eneo lake na imeleta utulivu hata katika Kyrgyzstan huria.

Katika miaka michache iliyopita, siasa nchini Kyrgyzstan zimebadilika kutoka mfumo huria wa vyama vingi hadi udikteta katili kama vile Tajikistan na Kazakhstan. Ingawa hapo awali vyama vyenye maoni tofauti vilikuwepo bungeni na vilipata fursa huru ya kushindana, leo kila kitu kinaamuliwa na Rais S. Zhaparov. Kremlin imepata mtumishi-dikteta mtiifu ndani ya shakhsiya ya S. Zhaparov na K. Tashiev, ambao hawana hofu ya kuchafua mikono yao na kufuata sera kali kwa maslahi ya Moscow.

Nchi za Magharibi zimejaribu mara kwa mara kuhujumu hali nchini humo na kupata ushawishi wa kisiasa, lakini juhudi zote zimeambulia patupu. Moscow imefaulu kuitakasa nchi hiyo kutokana na waliberali wasiohitajika wanaounga mkono Magharibi na kubatilisha majaribio yote ya nchi za Magharibi kujiimarisha nchini humo.

Sheria ya “NGOs zinazofanya kazi za uwakilishi wa kigeni” ni mfano halisi. Msingi na maudhui ya sheria hiyo yanaendana kikamilifu na sheria iliyopitishwa na Moscow katika Shirikisho la Urusi, kama wataalamu wengi walivyoandika kuihusu. Sheria hiyo inahusu udhibiti wa mashirika ya umma yanayofadhiliwa kutoka ng’ambo. Mahakama ya Upeo, Afisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu na Ombudsman ya Kyrgyzstan walipinga mswada huu. Hata E. Blinken mwenyewe aliingilia kati na kueleza wasiwasi wake, lakini Rais S. Zhaparov alimwomba E. Blinken asiingilie siasa za ndani za serikali na bado akaidhinisha mswada huu.

Kwa muda mrefu nchi za Magharibi zimetumia na zinatumia NGOs kueneza fikra za demokrasia, uliberali, uhuru wa kusema na haki za binadamu katika jamii ili kufikia malengo yake ya kisiasa. Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani na tume na kamati mbalimbali za Muungano wa Ulaya zinazungumza mara kwa mara kuhusu kuheshimu haki za kiraia na kuunda taasisi za kiraia za mtindo wa Magharibi katika Asia ya Kati.

Waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Shoigu pia alizungumza kuhusu chombo hiki kama ushawishi wa kisiasa. Katika msimu wa mchipuko, katika mkutano wa kawaida wa Wizara ya Ulinzi, alisema: “Kuna zaidi ya mashirika 100 makubwa yasiyo ya kiserikali yanayounga mkono Magharibi yanayofanya kazi katika eneo hili, yenye afisi na matawi zaidi ya 16,000. Dhidi ya muktadha wa operesheni maalum za kijeshi, mashirika haya yasiyo ya kiserikali yameongeza kwa kiasi kikubwa shughuli zao dhidi ya Urusi ili kupunguza ushirikiano wa kijeshi-kiufundi, kiuchumi na kiutamaduni kati ya dola za Asia ya Kati na Shirikisho la Urusi. Tunachukua hatua changamfu.

Hapo awali mswada huo huo ulipitishwa nchini Tajikistan, baada ya hapo zaidi ya NGOs 700 zilisitisha shughuli zao. Hali ni sawia nchini Kazakhstan. Sasa zamu imefika kwa Kyrgyzstan. Udhibiti mkali wa mashirika yasiyo ya kiserikali na kufungwa kwao huacha nchi za Magharibi bila ya kuwa na mamlaka juu ya wale walio mamlakani katika eneo hilo na, matokeo yake, kusababisha kupoteza ushawishi wa kisiasa.

Kwa mfano, kupitishwa kwa sheria kama hiyo huko Georgia kulisababisha machafuko na kutoridhika kwa watu wengi katika jamii. Mamlaka zililazimika kutumia nguvu kuwatawanya waandamanaji. Hii ilionyesha ni jinsi gani nchi za Magharibi zimepenyeza katika jamii fikra za haki za binadamu, uhuru wa kusema na uliberali.

Pia, hakuna hata mmoja wa viongozi wa Asia ya Kati aliyeshiriki katika “mkutano wa amani” nchini Uswizi, wakionyesha utiifu wao kamili kwa Moscow. Hasa, Rais wa Kyrgyzstan S. Zhaparov alikataa kwenda. Kwa hivyo, Moscow inaonyesha wazi uwezo wake kwa kuondoa kimfumo uwepo wowote wa ushawishi wa Magharibi katika eneo hilo.

Matokeo yake, Waislamu wa nchi hiyo pia wameteseka. Katika miezi michache iliyopita, makumi ya Waislamu, wanaume kwa wanawake, wabebaji wa dhati wa ulinganizi wa Kiislamu, wamekamatwa. Hii imekuwa ndio kanuni: katika mapambano baina ya wakoloni makafiri kwa nyanja za makafiri, Waislamu ndio wanaoteseka. Suluhisho pekee sahihi la kukombolewa kutoka katika minyororo ya wakoloni makafiri na fursa ya kutekeleza dini yao kwa uhuru itakuwa ni kufanya kazi ya kuhuisha Dola ya Khilafah Rashida ya Pili kwa njia ya Utume, inayoongozwa na mtawala muadilifu. Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu katika Kitabu chake kitukufu:

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [24:55].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Eldar Khamzin
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu