Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Tanzania na Janga la Utegemezi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Jumapili ya tarehe 02 Juni, Juni 2024, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya Korea Kusini zilitia saini mikataba ya makubaliano ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili jijini Seoul. Mikataba hiyo ilijumuisha mkopo wa dolari bilioni 2.5 (Tsh trilioni 6.5) uliotolewa na Korea Kusini chini ya Mfuko wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Korea Kusini (EDCF) kwa ajili ya miradi mbalimbali ya miundombinu.

Maoni:

Wakati nchi kubwa za kibepari zikiwa kati kinyang’anyiro baina yao kwa rasilimali nyingi za Afrika, Seoul pia imeungana na miji mikuu mingine kama vile Beijing, Washington na Moscow kufanya kongamano la viongozi wa Kiafrika kwa dhamira kama hiyo hiyo

Hii sio mara ya kwanza kwa Tanzania kuhudhuria mkutano wa Afrika na Korea Kusini. Kongamano la kwanza la Afrika na Korea Kusini lilifanyika jijini Seoul mnamo mwaka 2006.

Kama walivyo mabepari wengine, biashara baina ya Tanzania na Korea Kusini haina usawa, ni ya kinyonyaji na inainufaisha zaidi Korea Kusini. Kwa mfano, kwa miaka mitano (2016 hadi 2020) thamani ya mauzo ya nje kutoka Tanzania kwenda Korea Kusini imepungua kutoka wastani wa dolari milioni 38.794 mwaka 2016 hadi dolari milioni 29.818 mwaka 2019. Bidhaa za Tanzania zilizouzwa Korea Kusini zilikuwa na thamani ya dolari milioni 47 mwaka 2020, ilhali Tanzania iliagiza bidhaa za thamani ya dolari milioni 151 kutoka Korea Kusini.

Kama si ukoloni na unyonyaji dhidi ya Afrika, mikataba ya kibiashara baina ya Tanzania na Korea Kusini na mataifa mengine ingekuwa na manufaa, yenye kuleta msukumo mkubwa wa maendeleo ya kiuchumi. Mauzo ya nchi za Kiafrika kwa Korea Kusini kwa bidhaa kama shaba, kahawa, karafuu, mazao ya miti, mboga, alumini, mbegu za mboga, mbao na madini yana thamani kubwa, kwa taifa lolote makini lililobeba mfumo thabiti, ambapo lingeweza kuboresha viwanda vyake vya usindikaji kama vile korosho, mbegu za mafuta, viungo na samaki na hivyo kuzalisha viatilifu vyake vya maabara, nguo na bidhaa nyingine za viwandani ambazo Tanzania sasa inaagiza kutoka Korea Kusini kwa gharama kubwa.

Miongoni mwa mambo mengine ambayo ushirikiano kati ya Korea Kusini na Tanzania ulizingatia ni nishati, miundombinu, uchumi wa samawati, usalama wa chakula na madini.

Ni zaidi ya aibu kwa nchi kama Tanzania kutegemea Korea Kusini katika masuala ya usalama wa chakula, huku ikiwa na eneo la hekta milioni 44 za ardhi ya kilimo na inakadiriwa kuwa hekta milioni 29.4 inayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji, ni nchi ya pili kuwa na idadi kubwa ya mifugo barani Afrika, bila ya kusahau rasilimali watu zaidi ya milioni 61, yenye vyanzo vikubwa vya maji kama vile Ziwa Victoria, ambalo ni miongoni mwa maziwa makubwa duniani yenye ukubwa wa mita mraba 65,583, ambapo Tanzania pekee ina sehemu ya 49% ya kilomita za mraba 33,700. Ziwa Tanganyika, ziwa la pili kwa ukubwa kwa ujazo duniani na lenye kina kirefu zaidi barani Afrika ambalo lina kiasi kikubwa cha maji safi. Zaidi ya yote ina bahari ya eneo la kilomita za mraba 64,000, nk.

Tanzania kama yalivyo mataifa mengine yanayoendelea, kwa kuwa yamekosa nguzo ya mfumo madhubuti, yanashindwa kutumia rasilimali zao kwa ajili ya usalama wa chakula na maendeleo ya kilimo!

Unyonyaji wa rasilimali za Afrika kupitia mahusiano haya ya kikoloni kati ya Afrika na mataifa ya kibepari utaendelea kama mfumo wa kishetani muovu wa kibepari utaendelea kubakia na kulazimishwa duniani badala ya Uislamu.

Uislamu chini ya serikali yake ya Khilafah kwa Manhaj ya Utume, utahakikisha uanzishwaji wa tafiti na maendeleo ya viwanda na kilimo, na kukomesha mikopo ya kikoloni na masharti yao ya kinyonyaji kwa njia mbadala za mapato ya Kiislamu, yakiwemo mapato ya mali za Umma kutokana na rasilimali hizi nyingi za Afrika.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Said Bitomwa

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu