Jumanne, 17 Sha'aban 1445 | 2024/02/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kinachoitwa Ubwana wa Dola za Kitaifa na Ushirikiano wa Dola Vibaraka na Kafiri Mkoloni Dhidi ya Watu wao wenyewe

(Imetafsiriwa)

Habari:

Takriban watu 40 wameripotiwa kuuawa katika ulipizaji kisasi wa Marekani, ambao pia ulihusisha utumiaji wa mabomu ya kimkakati aina ya B-1B. Iraq kwa upande mwingine ilitangaza kuwa watu 16 wakiwemo raia wameuawa katika mashambulizi ya Marekani katika saa zilizopita. (Milliyet 03.02.2024)

Maoni:

Mkoloni kafiri Marekani, ili kulipiza kisasi cha kifo cha wanajeshi 3 waliouawa kwa shambulizi la droni katika kambi yake ya kijeshi nchini Jordan, ilizishambulia kwa mabomu nchi za Waislamu, ikipuuza kile kinachoitwa ubwana wa nchi za Waislamu na kuangalia macho ya watawala wao, na kuwaua Waislamu bila ya kuwaita wazee, watoto na raia. Watawala wasaliti katika nchi za Waislamu, wanaozungumzia kile kinachoitwa ubwana wa kujitawala, ima husema kwamba wamefurahishwa na jambo hili, au wanakaa kimya kuhusu Marekani kuwashambulia kwa mabomu watu wao katika ardhi zao, au wanalaani shambulizi hilo kwa kutoa kauli dhaifu kama Iraq ilivyofanya, au wanashirikiana na kafiri mkoloni Marekani katika mauaji ya Waislamu kama Jordan. Inasemekana kuwa ndege zilizotumika katika mashambulizi ya Marekani dhidi ya Iraq na Syria zilipaa kutoka Jordan. Hakuna udhalilifu na usaliti mkubwa kuliko huu.

Marekani inaweza kuua makumi, mamia au hata maelfu ya Waislamu, kama ilivyo Afghanistan, kulipiza kisasi vifo vya wanajeshi au raia wake. Lakini zaidi ya Waislamu elfu 25 wameuawa kinyama huko Gaza kwa karibu miezi 4. Wako wapi watawala katika nchi za Waislamu? Je, maisha haya ya mashahidi elfu 25 hayana thamani? Wakati Marekani inaua makumi ya Waislamu kwa wanajeshi 3 waliouawa bila kupepesa macho, kwa nini watawala wa nchi za Waislamu hawafanyi vivyo hivyo wakati wanajeshi wao au raia wanauawa? Kwa nini hawalipizi kisasi cha uhai kwa uhai na jino kwa jino? Je, wameanguka na kuzama kwenye shimo la usaliti na utumwa? Je, nyoyo zao haziumi kwa ajili ya watoto na wanawake waliouawa? Je, wamepoteza kabisa hisia zao na ubinadamu?

Je, majeshi wanayotumia mamilioni ya dolari kwao yapo tu kulinda viti vyao au kupata maslahi ya mabwana zao, Marekani na Uingereza? Huku Marekani ikitoa kila aina ya msaada wa vifaa kwa Wazayuni ambao wamekuwa wakiwachinja Waislamu huko Gaza kwa karibu miezi 4, watawala wasaliti wa Waislamu hawawezi hata kutoa msaada wa kibinadamu. Inabidi wapate kibali kutoka Marekani au umbile la Kiyahudi kutoa msaada. Au wanakula njama na makafiri wa Riyadh, Cairo na Paris dhidi ya Waislamu ili kuliokoa umbile la Kiyahudi kutokana na kufungwa na kushindwa lilikoangukia.

Marekani inatoka umbali wa kilomita 20,000 na kuwaua ndugu na dada zetu Waislamu katika ardhi yetu, lakini kwa nini hatuwezi kuua raia wake katika ardhi yake ili kulipiza kisasi cha vifo vya ndugu na dada zetu Waislamu? Hatuwezi hata kuwaua wanajeshi na raia wa Marekani katika ardhi yetu, achilia mbali kuwaua raia wake katika ardhi yake ili kulipiza kisasi cha vifo vya ndugu na dada zetu Waislamu. Kwa sababu ya utumishi na utumwa wao kwa Marekani, hawana ujasiri na hatuna ndege za kufikia bara la Amerika. Ndege walizonazo majeshi yetu ni ndege za Marekani, Ulaya au Urusi. Sisi tunategemea makafiri kwa kila kitu. Hatuwezi hata kununua au kubadilisha ndege za kisasa bila idhini yao.

Sababu pekee ya hali mbaya tuliyo nayo leo ni mfumo wa kibepari na watawala wasaliti wanaotabikisha mfumo huu. Iwapo tunataka kurudisha heshima na izza yetu ya awali kama katika Khilafah Umawiyya, Abbasiyya na Uthmaniyya, lazima kwanza tuwaondoe watawala hawa wasaliti na mfumo wa kibepari uliopitwa na wakati wanaoutabikisha. Kisha ni lazima tusimamishe Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume. Khilafah italipiza kisasi hata kwa mwanamke wa Kiislamu anayetukanwa au ambaye anafunguliwa staha na makafiri, achilia mbali kulipiza kisasi cha mauaji ya raia wake. Ushahidi bora kabisa wa hili ni kulipizwa kisasi kwa Mayahudi mjini Madina ambao walimvua abaya mwanamke wa Kiislamu, na kulipizwa kisasi kwa mwanamke aliyeomba msaada kutoka kwa Khalifa Mutasim kwa sababu ya mashambulizi aliyoyapata huko Amuriyah.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ercan Tekinbaş

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu