Jumanne, 17 Sha'aban 1445 | 2024/02/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Je, Uzuiaji wa Nyuklia ya Pakistan ndio Mstari Mwekundu Unaofuata, Kuvukwa?

(Imetafsiriwa)

Habari:

"Pakistan na IAEA zitaongeza ushirikiano katika matumizi ya amani ya sayansi na teknolojia ya nyuklia, hasa katika kilimo na matibabu, kwa manufaa ya nchi na majirani zake. Hayo yalikuwa matokeo ya safari ya siku mbili ya Mkurugenzi Mkuu Rafael Mariano Grossi nchini Pakistan wiki hii, ambapo alikutana na uongozi wa nchi hii - ikiwa ni pamoja na Mawaziri Wakuu na Mawaziri wa Mambo ya Nje - na kutembelea vituo vingi vya nyuklia nchini kote, ambapo baadhi yake alivizindua.” (Chanzo Tovuti ya IAEA)

Maoni:

Ratiba ya kina na makadirio ya ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa IAEA nchini Pakistan mnamo Februari 2023, inasikitisha. Ni kana kwamba watawala wa Pakistan walikuwa wanatafuta idhini ya IAEA ya mpango wetu wa nyuklia. Ni wazi kwamba watawala wetu wamejitolea kwa itikadi ya Bajwa, ya kuipa India hali ya usalama, kwa kubadilisha ujumbe wa kuzuia, pamoja na simulizi ya matumizi ya amani ya teknolojia ya nyuklia. Kufuatia mtindo wa Musharraf wa kuvuka mistari mekundu, huku akionyesha mstari mwekundu unaofuata, baya zaidi linatarajiwa. Uregeshaji wa simulizi ya uzuiaji inaweza kufuatiwa na upokonyaji silaha za nyuklia kama Khilafah haitasimamishwa hivi karibuni.

Hebu na tuzingatie mistari mekundu ambayo imevukwa. Baada ya 9/11, wakati marehemu Jenerali Pervez Musharraf alivuka mstari mwekundu kuhusiana na Afghanistan. Alifinika usaliti wake kwa hoja kwamba mali za nyuklia, Kashmir na uchumi vitaokolewa. Kisha akavuka mstari mwingine mwekundu, kwa kuwakandamiza mujahidina huko Kashmir, kwa ombi kwamba mali za nyuklia na uchumi vitaokolewa.

Mistari mekundu inaendelea kuvukwa. Wasiwasi uliongezeka wakati wakoloni walipoiweka Pakistan katika orodha ya kijivu ya FATF, na tishio la kugeuza kuiweka kwenye orodha nyeusi. Wakikabiliwa na shinikizo, watawala wa Pakistan walikosa msaada wowote kwa Waislamu wa Kashmir Inayokaliwa kimabavu, kutoka Pakistan. Walifanya hivyo kwa gharama ya kuisalimisha Kashmir kwa Dola ya Kibaniani, wakati Modi alipoliunganisha kwa nguvu mnamo Agosti 2019. Ni ukweli ambao umekubaliwa hata na duru tawala. Baada ya kuvuka mstari huu mwekundu, watawala walisema kwamba uchumi utakuwa salama.

Sasa ni uchumi wa Pakistan unaoporomoka kutokana na watawala kujiingiza katika matakwa ya kiuchumi ya wakoloni, ikiwa ni pamoja na kushuka kwa thamani ya sarafu, malipo ya riba, kupanda kwa bei ya mafuta na nishati na ongezeko la kodi. Baada ya mstari huu mwekundu pia kuvukwa, watu sasa wanajadili mstari mwekundu unaofuata, ambao ni mali za nyuklia.

Ilikuwa ni katika hali hii ambapo IAEA ilitembelea Pakistan. Watu wa Pakistan walifadhaishwa na kiwango cha ziara hiyo, pamoja na wakati wake. Ilikuja baada ya Rais Joe Biden, alipokuwa akihutubia harambee ya kuchangisha fedha kwa Bunge la Kidemokrasia mnamo Oktoba 2022, kusema kwamba Pakistan "inaweza kuwa moja ya mataifa hatari zaidi ulimwenguni" kwa kumiliki "silaha za nyuklia bila mshikamano wowote."

Watu wenye nguvu lazima wasongee sasa ili kuzuia mstari mwekundu unaofuata usivukwe. Hakuna jengine zaidi ya kusimamisha kwao Khilafah kwa Njia ya Utume itakayozuia hilo. Khilafah itachukua nafasi ya itikadi ya uzuiaji mdogo, na utawala wa wigo kamili. Haitaomba utaratibu wa kimataifa wa Magharibi kwa uhalali wa kimataifa wa mpango wetu wa nyuklia. Badala yake itachochea hofu nyoyoni mwao.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Shahzad Shaikh
Naibu Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu