Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Maamuzi ya ICJ juu ya umbile la Kiyahudi: Kumtaka Mvamizi huyo huyo Kujichunguza katika Vita vyake dhidi ya Gaza ni Upuuzi!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Uamuzi uliitaka Israel kuzuia na kuadhibu uchochezi wowote wa umma wa kufanya mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina huko Gaza na kuhifadhi ushahidi kuhusiana na madai yoyote ya mauaji ya halaiki huko.

Israel pia lazima ichukue hatua za kuboresha hali ya kibinadamu kwa raia wa Palestina katika eneo hilo, ulisema.

Haihitaji kusitisha mapigano ya kudumu. (Reuters 26/01/2024)

Uamuzi wa mpito uliotolewa na mahakama uliamuru hatua sita za muda, ikiwa ni pamoja na Israel kuchukua hatua zote kuzuia vitendo vya mauaji ya halaiki, kuzuia na kuadhibu uchochezi wa moja kwa moja na wa umma wa mauaji ya halaiki, na kuchukua hatua za haraka na madhubuti kuhakikisha utoaji wa msaada wa kibinadamu kwa raia huko Gaza. (Aljazeera)

Maoni:

ICJ haikuamuru kukomesha vita dhidi ya Gaza! Kumtaka mvamizi huyo huyo kujichunguza katika vita vyake dhidi ya Gaza ni upuuzi! Bomba lisilokuwepo kwenye mkono ndilo lililotolewa kwenye mkono wenye damu wa ‘Israel’ na majeshi yake. Madai ya ukosefu wa ushahidi katika mauaji ya halaiki kwa raia na uharibifu kamili wa hospitali, shule na nyumba yanashangaza. Katika enzi ya upeperushaji moja kwa moja wa matukio na unakilishaji habari pindi zichipuzapo, hili linawezaje kuwa?!

Ni hali halisi ya milat al-kufr (muungano wa makafiri) dhidi ya Waislamu hata wakati wanawake hawa, watoto na wazee hawana silaha na wako katika hali ya uhamisho na kutafuta hifadhi katika shule na mahema ya Umoja wa Mataifa. Huku Marekani ikiendelea kusisitiza kwamba "Israel" ina haki ya kujilinda, maisha zaidi yataangamizwa na kupotea.

Funzo la kweli kwa Waislamu, haki kamwe haitatolewa kwao kutoka katika mahakama za jumuiya ya kimataifa! Ni ujinga na upumbavu kutarajia hatua kama hiyo kutoka Ulaya au Marekani kuwaegemea watu wa Palestina dhidi ya umbile la Kiyahudi ambalo Uingereza na Marekani zililiasisi na kufadhili uwepo wake na kusababisha maafa mengi kwa watu wa Palestina.

Ni jambo ukarimu kwa Afrika Kusini na mataifa yanayoiunga mkono kuendelea na hatua ya kijasiri katika kujaribu kulitaka umbile la Kiyahudi juu kukomesha ukatili wao lakini wakiwa na Marekani kama mshirika wake mkuu, matokeo hayapaswi kutarajiwa. Uadilifu utatolewa tu kwa watu wa Gaza na Palestina mikononi mwa mahakama ya Kiislamu inayotabikisha na kutekeleza sheria zake chini ya Dola ya Kiislamu yenye nguvu yaani Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ambayo itawalinda Waislamu na kueneza rehema na uadilifu wake kwa wanadamu wengine kuwalinda dhidi ya mauaji ya halaiki. Pia itamhesabu kila mvamizi na muuaji wa Waislamu na watawala wa Waislamu waliokaa kimya huku vita dhidi ya Waislamu vikiendelea.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Manal Bader

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu