Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Jamii ya Rohingya ni Ummah Uliosahauliwa bila ya Khilafah

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 11 Agosti 2023, BBC iliripoti kwamba Waislamu 23 wa Rohingya walikufa na 30 hawajulikani waliko baada ya mashua iliyobeba wahamiaji wanaotoroka serikali kandamizi ya Myanmar kuzama. Miili ya Warohingya 23 wanaokimbia kwa ajili ya maisha yao kutoka Jimbo la Rakhine wamepatikana baada ya mashua yao kuzama. Wengine thelathini bado hawajulikani waliko, huku watu wanane wakiripotiwa kuwa walinusurika ajali hiyo. Walionusurika walisema walikuwa wanajaribu kufikia Malaysia wakati mashua yao iliyobeba abiria zaidi ya 50 kuzama na kutelekezwa na waendeshaji wake. Maelfu ya Warohingya hujaribu safari hatari ya bahari kwenda Malaysia au Indonesia kila mwaka. Wanatoroka sera za mauaji ya kikabila.

Maoni:

Kinyume na maoni ya wengi, ukandamizaji wa ndugu na dada zetu katika jimbo la Burma sio jambo la hivi karibuni. Mateso ya Waislamu wa Rohingya huko Myanmar yalianzia kutokea angalau miaka ya sabiini. Tangu wakati huo, watu wa Rohingya wamekuwa wakiteswa mara kwa mara na serikali na wazalendo wa Kibudha. Ukiukaji muovu wa wanawake na kifo kwa moto ambapo vijiji vyote vimechomwa hadi majivu imekuwa kawaida ya vizazi vya Waislamu nchini Myanmar. Uhalisia unaochukiza ni kwamba wanapojaribu kutoroka, wanakabiliwa na hatari kubwa katika bahari zisizokuwa salama na kisha maumivu zaidi kutoka kwa ubaguzi wa serikali wa nchi jirani. Hawakaribishwa kama inavyopaswa kuwa katika sunnah ya Mtume (saw), ambaye alitunza kikundi chochote kinachotafuta hifadhi. Badala yake, wanaadhibiwa na kuwekwa katika kambi za wakimbizi zilizojaa kama zile zilizo nchini Bangladesh.

[وَاعْبُدُوا اللَّهَ وَلَا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا وَبِذِي الْقُرْبَىٰ وَالْيَتَامَى وَالْمَسَاكِينِ وَالْجَارِ ذِي الْقُرْبَى وَالْجَارِ الْجُنُبِ وَالصَّاحِبِ بِالْجَنْبِ وَابْنِ السَّبِيلِ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ مَنْ كَانَ مُخْتَالًا فَخُورًا]

“Muabuduni Mwenyezi Mungu wala msimshirikishe na chochote. Na wafanyieni wema wazazi wawili na jamaa na mayatima na masikini na jirani wa karibu na jirani wa mbali, na rafiki wa ubavuni na mpita njia, na walio milikiwa na mikono yenu ya kulia. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri” [4:36]

Wale waliokufa wiki hii ni pamoja na wanawake 13 na wanaume 10; Waislamu wote wa Rohingya watasimama mbele ya Mwenyezi Mungu (saw) siku ya kiyama na watauliza haki zao kutoka kwa viongozi wa Waislamu ambao walipuuza mateso yao. Enyi Ummah wa Mohammad (saw)! Msiwe kimya dhidi ya kuwahasibu wale walio na jukumu la kuregesha mamlaka ya Uislamu ulimwenguni, msije mkafufuliwa pamoja na waovu!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Imrana Mohammad
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu