Ijumaa, 08 Dhu al-Hijjah 1445 | 2024/06/14
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Siasa za Nasaba na Shakhsiya ya Mtu Kamwe Haziwezi Kuleta Mabadiliko ya Kweli

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 18 Mei 2023, Mwenyekiti wa Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI), Imran Khan, alilaani shambulizi kwenye mitambo ya jeshi. Alisema muungano tawala wa PDM ulitaka kuiondoa PTI kutoka kwa siasa za kuu kupitia kuligombanisha jeshi na chama cha upinzani.

Huku mamlaka zikiimarisha ukandamizaji dhidi ya PTI, kufuatia ghasia zilizotokea tarehe 9 Mei, waziri mkuu huyo wa zamani alisema chama chake "hakina mzozo" na idara hiyo ya jeshi.

Maoni:

Bara dogo la India linakumbwa na siasa za shakhsiya ya mtu na za nasaba. Zinazozuia watu kuangalia fikra, sera, sheria, katiba na mifumo kwa uwazi. Hii ndio hali kuhusiana na wafuasi wa watawala na upinzani.

Tangu kubanduliwa kwake katika afisi ya Waziri Mkuu wa Pakistan mnamo Aprili 2022, Imran Khan na wafuasi wake wamechukulia kukamatwa kwake kama mstari mwekundu. Inamaanisha tu kwamba hakuna kitu kilicho muhimu zaidi kuliko Imran Khan. Hii inaonyesha kuwa utiifu wa wafuasi wa chama hicho unafungamana na kiongozi wa chama, badala ya fikra.

Hata hivyo, Imran Khan na wafuasi wa chama chake walikuwa wakilaani tabia kama hiyo ndani ya upinzani wao. Walikuwa wakiwashutumu wafuasi wa Altaf Hussain, kiongozi wa Vuguvugu la Muttahida Qaumi (MQM), chama chenye makao yake makuu Karachi. Pia walishutumu nasaba ya Bhutto ndani ya chama cha Pakistan People's Party na nasaba ya Sharif ndani ya chama cha Pakistan Muslim League- Nawaz.

Siasa zilizojengwa juu ya nasaba na shakhsiya ya mtu hufanya vigezo vya zuri au baya, kauli na matendo ya kiongozi wa chama. Imeharibu vibaya siasa za Pakistan na Ulimwengu mzima wa Kiislamu. Badala ya kutafuta maslahi ya watu na Uislamu, siasa imekuwa ni utumiaji wa wanaharakati wa vyama kwa maslahi binafsi ya viongozi wao. Siasa hii ndiyo imezuia; utabikishaji wa kina wa Uislamu, ukombozi wa Kashmir na Palestina, ulinzi wa heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na ustawi wa kiuchumi.

Kuna kiongozi mmoja na shakhsiya moja tu kwa Waislamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Pindi Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alipoondoka duniani, Maswahaba (ra) walitikisika. Hata hivyo, Khalifa wa kwanza wa Waislamu, Abu Bakr as-Siddiq (ra) alisema:

 أَمَّا بَعْدُ مَنْ كَانَ مِنْكُمْ يَعْبُدُ مُحَمَّدًا ﷺ فَإِنَّ مُحَمَّدًا قَدْ مَاتَ، وَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ يَعْبُدُ اللَّهَ فَإِنَّ اللَّهَ حَىٌّ لاَ يَمُوتُ، قَالَ اللَّهُ:

[‏وَمَا مُحَمَّدٌ إِلاَّ رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِنْ قَبْلِهِ الرُّسُلُ]

“Ama baada ya swala na salamu, yeyote miongoni mwenu aliyekuwa anamuabudu Muhammad (saw), basi Muhammad ameshakufa, na yeyote miongoni mwenu aliyekuwa anamuabudu Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu yuko Hai hafi milele. Mwenyezi Mungu amesema, “Na Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwisha pita kabla yake Mitume.” (Surah Aali Imran 3.144).” (Bukhari). Baada ya hapo, waliimarisha azma yao na kuthibitisha kujitolea kwao kwa Uislamu, na dola yake, Khilafah Rashida.

Waislamu wa Pakistan lazima waachane na siasa za nasaba na shakhsiya ya mtu. Ni lazima wakumbatie siasa zenye msingi wa Dini ya Uislamu na kufanya kazi ya kusimamisha dola itakayotabikisha Uislamu, Khilafah kwa Njia ya Utume. Hizb ut Tahrir ndiyo iliyotayarisha rasimu ya katiba na maktaba ya vitabu, inayofafanua hukmu za Shariah kuhusiana na sera, sheria na katiba. Hivyo basi Waislamu na waachane na siasa za kisekula za nasaba na shakhsiya ya mtu. Wafanye kazi na Hizb ut Tahrir kusimamisha tena hukmu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Shahzad Sheikh
Naibu Msemaji wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu