Jumatano, 14 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Tarehe ya Makataa ya Kushindwa Kulipa Deni ya Marekani Yakaribia kwa Kasi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 12 Mei, Waziri wa Hazina wa Marekani Janet Yellen aliandika: 'Endapo Bunge la Congress halitaongeza kiwango cha deni, tutakabiliwa na janga la kiuchumi na kifedha. Ni muhimu sana tuhakikishe kuwa hili linafanyika." Yellen ni mwanauchumi mwenye uzoefu ambaye hapo awali alikuwa mwenyekiti wa 15 wa Hizina ya Marekani. Alirudia onyo lake mnamo Mei 15: "Pamoja na habari ya ziada inayopatikana sasa, ninaandika ili kutambua kwamba bado tunakadiria kuwa Hazina haitaweza tena kukidhi majukumu yote ya serikali ikiwa Congress haijachukua hatua ya kuinua au kusimamisha kikomo cha deni mapema Juni, na ikiwezekana mapema Juni 1."

Maoni:

Kila baada ya miaka michache maonyesho ya kisanii ya ukomo wa deni la Marekani hutikisa uchumi wa dunia uliojengwa juu ya riba. Bajeti ya Marekani na kiasi cha pesa ambacho Marekani inaweza kukopa huamuliwa na Bunge la Congress pekee, na kadiri Marekani inavyokopa pesa nyingi zaidi kuliko inazozalisha kila mwaka deni huzidi kupanda na kuingia kwenye kikomo kilichoamuliwa na Bunge la Congress, ambacho pia huitwa kiwango cha juu cha deni. Kiwango hicho cha juu kimefikiwa na serikali inaishiwa na pesa lakini haiwezi kukopa tena hadi Wanademokrasia na Wanajamhuri wakubali kuongeza kikomo. Kwa vile utawala uko mikononi mwa Democrat, Warepublican wanakataa kukubaliana hadi matakwa yao wenyewe yatimizwe. Kwa hiyo, ikileta mgogoro huku tishio la serikali ya Marekani kukiuka wajibu wake wa kifedha likizidi kukaribia.

Mgogoro huu unatikisa imani ya wakopeshaji wa kimataifa, na hivyo basi gharama ya kukopa ya Marekani kupanda hata kabla ya Marekani kushindwa kulipa deni lake. Inaweza kutokea, na hivyo kutoa mikopo kwa Marekani inakuwa hatari zaidi. Waziri wa Hazina Yellen alidokeza hili katika barua yake kwa Congress: "Kusubiri hadi dakika ya mwisho kusimamisha au kuongeza kikomo cha deni kunaweza kusababisha madhara makubwa kwa biashara na imani ya watumiaji, kuongeza gharama za ukopaji za muda mfupi kwa walipa ushuru, na kuathiri vibaya kiwango cha mkopo cha Marekani ... Kwa kweli, tayari tumeona gharama za kukopa za Hazina zikiongezeka kwa kiasi kikubwa kwa dhamana zinazotimu muda wake mapema mwezi Juni,” aliandika.

Afisi ya Bajeti ya Bunge la Congress ilionya kwamba ikiwa kikomo cha deni kitabaki bila kubadilika, "kuna hatari kubwa kwamba wakati fulani katika wiki mbili za kwanza za Juni, serikali haitaweza tena kulipia majukumu yake yote" na kuongeza kuwa malipo ya madeni ya serikali hiyo ya shirikisho "yatasalia kutokuwa na uhakika mwezi mzima wa Mei, hata kama Hazina hatimaye itaishiwa na fedha mapema Juni." Hivyo Wamarekani wa kawaida wanapata hasara, kwani watalazimika kulipia zaidi chakula na mahitaji mengine ya kimsingi huku wanasiasa wakipigania maslahi finyo.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdullah Robin

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu