Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Shaka ya Magharibi ina Madhara Mabaya

(Imetafsiriwa)

Habari:

Ongezeko la vijana wanaojihusisha na makundi ya Nazi mamboleo na itikadi kali za mrengo wa kulia “ni la kutisha sana”, afisa mmoja wa upelelezi wa kukabiliana na ugaidi amesema. Naibu Msimamizi Gareth Rees alisema polisi hawawezi tena "kuendelea kuwakamata watu hili haliwezi kutatua” suala hilo.

“Kuna watu ambao ni wachanga sana, wanaovutia sana, na walio katika mazingira magumu sana ambao wanavutwa katika eneo la wasiwasi sana ambalo haliathiri tu ustawi wao, lakini pia hatimaye linawasilisha tishio kwa watu wengine.”

Dkt. Lella Nouri, mtaalamu mkuu wa chama cha mrengo wa kulia, alisema “kutokuwa na uhakika kunazaa itikadi kali”. Dkt. Nouri, mhadhiri mkuu wa masuala ya uhalifu katika Chuo Kikuu cha Swansea, alisema mkanganyiko na ukosefu wa habari kuhusu Covid ulicheza mikononi mwa watu wa mrengo wa kulia na ilikuwa ni chombo chenye nguvu cha kusukuma ujumbe wao. (Chanzo: BBC)

Maoni:

Sasa tunaishi katika ulimwengu wa baada ya enzi ya ukweli, ambapo vyombo vya habari na wanasiasa wanakuza fikra ya baada ya enzi ya usasa. Maswali ya lazima ya umma juu ya kitambulisho na kukataa ukweli ulio wazi inamaanisha kwamba viwango vya akhlaqi vilivyokuwa vikibadilika polepole katika nchi za Magharibi, sasa vinabadilika haraka sana, hivi kwamba ni rahisi kuona jinsi vijana wanavyoshindwa na hisia kwamba hakuna ukweli wowote. Kukata tamaa kama huko hakukubaliani na maumbile yetu ya kibinadamu, kwa hivyo ima kutamwangamiza mtu na kumlazimisha kutafuta msingi thabiti zaidi wa imani na maadili yake. Hakuna lolote kati ya haya linalopelekea kwenye furaha katika nchi za Magharibi, hasa kwa vile utoroshaji wa mali unazidi kuwa nje ya uwezo wa watu wengi.

Kinachozidisha mgogoro huu wa kina wa maadili na kitambulisho ni ukweli kwamba fikra ya Kiislamu kwa hakika haipo kwenye mazungumzo ya umma. Kipote cha wakoloni kwa muda mrefu kimekuwa kikiogopa kuibuka kwa Uislamu kama mfumo ambao utawang’oa vibaraka wao wa kikoloni kwenye viti vyao vya utawala na kupambana na utawala wa Magharibi wa ulimwengu. Sera zao za makusudi na za hila za kuuchafua Uislamu na Waislamu kwa hakika zimewatia hatiani Waislamu wanaouwasilisha Uislamu kama mfumo mbadala wa maisha ya wanadamu.

Uislamu kwa hakika ndio mfumo pekee wa kweli ambayo imethibitishwa kiakili na kuafikiana na umbile la mwanadamu. Maswali kama hayo ya kitambulisho na maadili yanapaswa kuregeshwa kwa Mwenyezi Mungu Muumba wa wanadamu wote.

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا)

“Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi. Na mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Mwenyezi Mungu na Mtume, ikiwa mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Hayo ndiyo bora zaidi na ndiyo yenye mwisho mwema.” [An-Nisaa, 4:59]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu