Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wakati wa Enzi ya Watawala Waovu, Matukufu ya Uislamu Yanakiukwa
(Imetafsiriwa)

Habari:

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Mevlüt Çavuşoğlu, alisema kuwa kuitwa kwa balozi wa Uswidi jijini Ankara mnamo tarehe 22 Januari 2023, kulijiri kama kulaani dhidi ya kuchomwa moto kwa Qur'an Tukufu mbele ya jengo la ubalozi wa Uturuki jijini Stockholm. Çavuşoğlu ameongeza kuwa, balozi wa Uturuki jijini Stockholm alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uswidi, Tobias Billström, na kumfahamisha kuhusu kutoridhika kwa Uturuki, na kukataa kwa serikali ya Uswidi kuwaruhusu waandamanaji kuchoma Qur'aniTukufu mbele ya jengo la ubalozi wa Uturuki.

Alieleza kuwa kuchoma Qur’an Tukufu na uadui kwa Uislamu na Waislamu hakuingii ndani ya uhuru wa kibinafsi. Serikali za Magharibi haziruhusu uchomaji wa vitabu vitakatifu vya dini nyenginezo. Ama Waislamu na matukufu yao, haraka wanahalalisha hilo kwa uhuru wa kujieleza. Çavuşoğlu alidokeza kuwa hakuna maandishi katika katiba ya Uswidi, wala ndani ya sheria za Muungano wa Ulaya, yanayoonyesha kuwa kuchoma Qur'an Tukufu iko chini ya uhuru wa kujieleza. Aliendelea, “Licha ya maonyo yetu yote, mamlaka za Uswidi zilitoa ruhusa ya kuchomwa Quran Tukufu, na hii inachukuliwa kuwa ni uhalifu dhidi ya Uislamu na Waislamu kote duniani.”

Pia ameashiria kuwa jamii ya Waturuki jijini Stockholm itaandaa maandamano mbele ya jengo la ubalozi wa Uturuki, na kuashiria haja ya serikali ya Uswidi kuchukua hatua zinazohitajika ili kuzuia kutokea tena kwa uhalifu kama huo.

Maoni:

Katika zama za Erdogan na Çavuşoğlu, Qur’an Tukufu imekuwa ikichomwa moto mara kwa mara, huku matusi dhidi ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) na Uislamu yakiongezeka. Hata hivyo, tunasikia tu maandamano na lawama kutoka kwa watawala hawa! Je, munadhani hili ndilo jibu sahihi kwa vitendo hivyo?! Lau Suleiman Mtukufu angekuwa hai, majibu yangekuwaje? Kama Mu'awiyah bin Abi Sufyan angekuwa hai, majibu yangekuwaje? Kama Omar bin Abdul Aziz angekuwa hai, majibu yangekuwaje? Kama al-Hajjaj angekuwa hai, majibu yangekuwaje?

Wakati wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), Yahudi mmoja alimshambulia mwanamke Muislamu, na jibu lilikuwa ni kufukuzwa kwa Mayahudi wa Banu Qaynuqa’ kutoka Madina. Wakati wa Al-Mu'tasim, mwanamke Muislamu alivamiwa, hivyo Amuriyya ilitekwa. Wakati wa Hajjaj, wanawake wa Kiislamu walivamiwa, na baadhi yao walitekwa, hivyo Sindh na Hind zilifunguliwa.

Ama zama za watawala hawa wa sasa, waovu, Palestina ilipotea, na watawala hawa wakakimbilia kusawazisha mahusiano na Mayahudi, huku mauaji ya kishahidi ya Waislamu yakiwa ni jambo la kawaida, bila aibu. Kila siku, Mayahudi wanawaua shahidi vijana wa Kiislamu, huku hakuna mtawala yeyote  anayenyosha kidole, sio hata kwa kiwango cha maneno ya kukashifu, kulaani na kupinga.

Wakati wa Suleiman Mtukufu, Suleiman alituma mjumbe kwa Mfalme wa Hungary, na Mfalme wa Hungary akamuua mjumbe wake. Suleiman Mtukufu aliongoza jeshi kibinafsi na kuifungua Belgrade, mji mkuu wa Hungary, katika mojawapo ya vita vikali zaidi katika historia, Vita vya Mohács.

Ama wakati wa Muawiyah bin Abi Sufyan, wakati jeshi la Waislamu lilipokuwa likiizingira Konstantinopoli, Abu Ayyub al-Ansari aliomba azikwe karibu na ukuta wa Konstantinopoli, na kwa hakika alizikwa kwenye sehemu ya karibu zaidi ya ukuta. Kaisari wa Rumi alijulishwa juu ya hilo, hivyo akatangaza kwa Muawiyah kwamba atalifukua kaburi na kuitoa ile maiti kwa ajili ya mbwa. Basi Mu'awiyah akamtangazia Kaisari wa Rumi, "أقسم بالله لو أن يدا امتدت إلى القبر لما تركت نصرانيا في بلاد المسلمين إلا قتلته، وما تركت كنيسة إلا هدمتها"   “Naapa kwa Mwenyezi Mungu, lau mkono utarefushwa kwenye kaburi sitamwacha Mkristo hata mmoja katika nchi za Kiislamu bila ya kumuua, na sitaacha kanisa hata moja, bila ya kulibomoa.” Kisha Kaisari wa Warumi akaamuru watu wake walilinde kaburi wao wenyewe, kwa kuogopa kwamba mmoja wa watu wa Kirumi anaweza kulifukua kaburi hilo!

Hivi ndivyo ardhi muitiko wenye mtingisho wa dunia lazima uwe, sio kwa maandamano, bali kwa majeshi yanayowatiisha maadui!

Kwa kumalizia, tunasema kuwa Khilafah ni ngao ya Uislamu na Waislamu. Wakati Khilafah ilipovunjwa, watu waovu zaidi waliushambulia Uislamu na Waislamu. Lau watawala wa kikafiri wangejua kwamba kuna mtawala katika Ardhi za Kiislamu anayekamata haki kwa mikono yake mwenyewe, wangeiweka Qur’an Tukufu juu ya sahani ya dhahabu, na kuiinua juu ya vichwa vyao...

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Salim – Ardhi Iliyobarikiwa (Palestina)

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu