Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Qatar ni nchi ya Kisekula na Kamwe Haitapiga Marufuku Unywaji Pombe katika Kombe lake la Dunia
(Imetafsiriwa)

Habari:

Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) lilitangaza kuwa vinywaji vyenye vileo havitauzwa katika viwanja vinane vitakavyoandaa mechi za Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar.

Vinywaji vya vileo vilipaswa kuandaliwa “katika maeneo yaliyotengwa ndani ya viwanja vya michezo,” ingawa uuzaji wao unadhibitiwa vikali katika dola hiyo ya Ghuba ya Kiislamu.

Wale ambao watakuwa katika maeneo ya watu muhimu sana (VIP) ya viwanja kwenye mashindano hayo bado wataweza kununua vileo. (BBC, 11/18/2022)

Maoni:

Qatar ilikuwa, kabla ya Kombe la Dunia, na bado ingali, nchi inayoruhusu uuzaji na ununuzi wa pombe na kuna baa 'za kupendeza', kulingana na maelezo ya wageni wao, kama ambavyo kuna vilabu vingi vya usiku katika mji mkuu na katika miji ya Qatar, mithili ya nchi nyenginezo za kisekula. Kama vile wanavyoruhusu sharubati, wanaruhusu mvinyo, na kama vile wanavyoruhusu kujengwa kwa misikiti, pia wanaruhusu ujenzi wa makanisa na mahekalu kwa ajili ya makafiri.

Kwa hakika, Qatar haikupiga marufuku pombe katika Kombe la Dunia, kama inavyosemekana, na watetezi wake na wapambe wake wanavyoinadi. Jaime Byrom, rais wa MATCH Hospitality, mfadhili wa Kombe la Dunia, alisema, “Vileo vitapatikana kwa mashabiki katika viwanja vya michezo kulingana na ununuzi wa vifurushi vya gharama kubwa. Lakini uamuzi bado haujatolewa juu ya upatikanaji wake katika viwanja kwa wenye tikiti za kawaida.”

Kwa upande mwingine, tuchukulie kuwa Qatar ilipiga marufuku pombe katika viwanja vyake, basi kwa nini wapambe hawa wanalipima hili kinafiki?! Baadhi ya nchi hapo awali zilipiga marufuku pombe katika viwanja vyao ili kulinda usalama, si kwa kujali dini au kwa sababu pombe ni haramu, la sivyo kusingekuwa na baa na mivinyo kuenea katika mitaa yao. Kipande cha habari kilichapishwa miaka iliyopita kikisema, "Ili kuhakikisha usalama wa Kombe la Dunia la 2018 katika kandanda kuanzia Juni 14 hadi Julai 15 kwenye ardhi yake, mamlaka za Urusi hazikusita kuchukua hatua kali: kuanzia kupiga marufuku pombe hadi uchomaji nyama, marufuku ambayo inabadilisha maisha ya Warusi. Uuzaji wa vileo na kila aina ya chupa za glasi zitapigwa marufuku jijini Moscow na miji mingine mkesha na siku ya mechi, katika maeneo maalum ambayo yanajumuisha maeneo ya karibu ya viwanja vya michezo na viwanja vya mazoezi, maeneo ya mashabiki na maeneo mengine makuu, kama vile vituo na mabustani." Moscow, nchi hiyo ya makafiri, hapo awali ilipiga marufuku pombe katika viwanja vyake vya michezo, basi uko wapi ukutufu na ustaarabu wa Qatar kupiga marufuku pombe kwenye viwanja vyake vya michezo?!

Inasikitisha kusikia baadhi ya Waislamu wakiishukuru Qatar kwa kitendo hiki, na kwa kuwakaribisha madaiee (wabeba dawah) ya Uislamu katika ardhi zake. Hata hivyo, ni lazima tuwakumbushe Waislamu kwamba Qatar pia imewakaribisha makuhani wa Kiyahudi na kuwapangia chakula, nyumba na ibada zao, na ilielezwa katika Gazeti la Al-Shorouk: “Mamlaka za juu za Qatar ziliwahakikishia mashabiki wa soka wa Kiyahudi kwamba hawatafanyiwa shinikizo lolote au vitisho vyovyote, wakati wa maandalizi ya mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2022. Qatar imejitolea kutoa mahekalu ya ibada kwa mashabiki wa soka wa Kiyahudi, pamoja na chakula kama ilivyoainishwa katika sheria zao, ili kujenga madaraja ya ushirikiano na udugu kati ya Mayahudi na Nchi za Ghuba.

Hapa, enyi Waislamu, sura ya kweli ya Qatar inadhihirishwa kupitia kuhalalisha mahusiano na Mayahudi maadui wa Uislamu na Waislamu. Hii ndiyo Qatar ya kisekula inayotumia fedha, uwezo na neema za Waislamu kuwaridhisha maadui wa Mwenyezi Mungu (swt) na maadui wa Uislamu. Kwa hivyo, hii inatosha kwenu kuishutumu Qatar na watawala vinaraka, kwani wote ni ndugu katika khiyana dhidi yenu na Dini yenu.

Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

(لَقَدِ ابْتَغَوُاْ الْفِتْنَةَ مِن قَبْلُ وَقَلَّبُواْ لَكَ الأُمُورَ حَتَّى جَاء الْحَقُّ وَظَهَرَ أَمْرُ الله وَهُمْ كَارِهُونَ)

 “Tangu zamani walitaka kukutilieni fitna, na wakakupindulia mambo juu chini, mpaka ikaja Haki na ikadhihirika amri ya Mwenyezi Mungu, na wao wamechukia.” [Surah At-Tawba 9:48]. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

(إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُواْ يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّواْ عَن سَبِيلِ الله فَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ وَالَّذِينَ كَفَرُواْ إِلَى جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ)

“Hakika wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa, kisha yatakuwa juu yao majuto, na kisha watashindwa. Na wale walio kufuru watakusanywa kwenye Jahannam.” [Surah Al-Anfal 8:36].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fatima Mahmoud

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu