Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Utawala Dhalimu wa Dolari ya Marekani Wasababisha Uharibifu kwa Sarafu ya Malaysia

(Imetafsiriwa)

Habari:

Leo (26 Septemba 2022), thamani ya Ringgit ya Malaysia (RM) imeshuka hadi kiwango cha chini kabisa kuwahi kurekodiwa tangu mgogoro wa kifedha wa 1997 ambapo kiwango cha ubadilishaji cha USD 1 sasa ni sawa na RM4.60. Kushuka kwa thamani ya RM kulitokea wakati wawekezaji wengi walipogeukia sarafu salama kutokana na kutokuwa na uhakika wa mtazamo wa kiuchumi duniani. Wanauchumi walilaumu nafasi ya kuimarika kwa dolari ya Marekani ikilinganishwa na sarafu za nchi nyingi juu ya upandishaji mkali wa viwango vya riba wa Marekani ili kuvutia fedha za kuimarisha dolari. Kutokana na mahitaji yanayoendelea ya USD, wawekezaji hawaioni ringgit kama sarafu ya ushindani na RM itaendelea kuwa katika mwelekeo dhaifu hadi hatua zitakapotangazwa za kukuuza uchumi. Licha ya kushuka kwa thamani ya ringgit, Waziri wa Fedha, Tengku Datuk Seri Zafrul Tengku Abdul Aziz, alionekana akitetea nafasi hiyo kwa kusema kuwa thamani ndogo ya ringgit itaongeza mahuruji ya nchi.

Maoni:

Ingawa kuanguka kwa ringgit kunaonekana kuwa kuzuri kwa wauzaji mahuruji wa ndani, Wamalaysia wengi watavumilia mzigo athari hasi. Kushuka kwa thamani ya Ringgit ya Malaysia (RM) kuna matokeo kadhaa, miongoni mwayo:

1) Gharama ya juu ya bidhaa zinazoagizwa kutoka nje - Malaysia inapaswa kulipa zaidi kwa maduhuli kutokana na kushuka kwa kiwango cha ubadilishaji wa RM.

2) Bei ya bidhaa kwa jumla itapanda - Kwa sababu ya gharama kubwa ya maduhuli, bei ya bidhaa muhimu pia itapanda na Malaysia inaagiza, ikiwemo vyakula.

3) Mfumko wa bei - Mzigo wa bei za juu unaonekana zaidi na kundi la kipato cha chini. Baya zaidi mapato hayaongezeki wala kuongezeka sana ikilinganishwa na kupanda kwa bei ya bidhaa muhimu.

4) Nguvu ya ununuzi ya Wamalaysia ng'ambo inapungua - Wale wanaotegemea mapato ya ndani kutumia ng’ambo watalazimika kutumia pesa zaidi wakati wa kutumia ng’ambo.

Ni wazi, Wamalaysia wana mengi zaidi ya kupoteza kuliko faida kutokana na kudhoofika kwa RM. Je, ni ipi sababu ya kudhoofika huku? Tangu kuzuka kwa vita vya Ukraine na Urusi Februari mwaka jana, Rais Biden wa Marekani aliweka vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Urusi. Marekani inafanya kampeni kwa nchi duniani kote kuitenga Urusi kiuchumi. Kwa kuwa Urusi ndiyo inayoongoza duniani kwa uzalishaji wa petroli na gesi asilia na Ukraine ni mojawapo ya wazalishaji wakuu wa ngano na mbolea, vikwazo hivyo vinaathiri usambazaji wa mafuta, gesi asilia na chakula. Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo (FAO) linaripoti kwamba Fahirisi ya Bei ya Chakula duniani (FPI) ilikuwa wastani wa pointi 159.3 mwezi Machi 2022, ikiwa ni pointi 17.9 (12.6%) kutoka Februari. Kwa kweli hii inaathiri Amerika vilevile na pamoja na kifurushi cha kichocheo cha dolari trilioni 4 baada ya janga la Covid, na mfumko wa bei ulipanda hadi karibu 9%. Ili kupunguza mfumko wa bei kwa haraka, Marekani ilipandisha viwango vya riba kwa dolari ya Marekani kwa ukali. Hili nalo lilisababisha wawekezaji kote ulimwenguni kuhangaika kubadilisha fedha zao kuwa dolari na kupata faida kubwa kutokana na mapato ya riba. Mahitaji makubwa ya USD yamesababisha sarafu zingine zikiwemo ringgit kutelekezwa.

Mahitaji makubwa ya pesa zisizo na thamani ya dhati za USD zisizoegemezwa kwa bidhaa kama vile dhahabu na fedha yamezidisha thamani ya sarafu kupita kiasi. Thamani ya pesa zisizo na thamani ya dhati hupimwa na uhusiano kati ya usambazaji na mahitaji ya pesa na uthabiti wa serikali inayozitoa, sio kulingana na thamani yake ya asili. Ikiwa mahitaji yanaongezeka, thamani ya pesa hupanda na inaweza kutathminiwa kupita kiasi (overvalued). Kwa upande mwingine, ikiwa kuna mzunguko mwingi, thamani ya pesa huanguka hadi mahali ambapo inaweza kuwa haina maana (hyperinflation). Kwa kuwa Marekani ilipandisha viwango vya riba, mahitaji makubwa ya USD yalisababisha thamani ya USD kuongezeka, huku mahitaji ya RM yakipungua na thamani ya ringgit ya Malaysia pia kupungua. Hili ndilo tatizo la viwango vya kubadilisha fedha kwa fedha zisizo na thamani ya dhati - sarafu kuu itadhoofisha sarafu zengine na kusababisha dhulma ya biashara ya kimataifa.

Uislamu uliweka dhahabu na fedha kama kiwango cha sarafu. Kipimo cha thamani ya bidhaa, huduma na kawi yote inaegemezwa juu ya kiwango cha dhahabu na fedha. Aina zote za shughuli za kiuchumi na kibiashara zinafanywa kwa kiwango hiki. Mfumo huu unahakikisha kuwa kiwango cha ubadilishaji wa sarafu kati ya nchi kimedhibitiwa. Kiwango maalum cha ubadilishaji wa fedha kitashajiisha ongezeko la biashara ya kimataifa kwa sababu wafanyibiashara hawaogopi kushindana. Tatizo la kutegemea sarafu kuu (sarafu madhubuti) linaweza kuondolewa na usawa katika biashara ya kimataifa unaweza kupatikana. Hadi sasa, nchi zengine ikiwemo Urusi na China hazijaweza kuondoa utawala wa dhulma wa USD katika uchumi wa dunia. Ni kwa kusimamishwa Khilafah pekee, ndio mfumo wa sarafu wa Kiislamu unaoegemezwa juu ya dhahabu na fedha utatabikishwa na kukomesha utawala wa USD, Insha’ Allah.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Mohammad – Malaysia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu