- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Pindi Tembo Weupe Wanapopigana, Nyasi Ndizo Ziumiazo
(Imetafsiriwa)
Habari:
GENEVA (22 Septemba 2022) - Wataalamu wa Umoja wa Mataifa leo wamelaani vikali kifo cha Mahsa Amini mwenye umri wa miaka 22, ambaye alifariki akiwa chini ya ulinzi wa polisi baada ya kukamatwa kwa madai ya kushindwa kuzingatia sheria kali za Iran kuhusu mavazi ya wanawake kwa kuvaa “hijab visivyo”. (Chanzo: ohchr.org)
Maoni:
Iran inakabiliwa na baadhi ya machafuko mabaya zaidi kuwahi kutokea katika miaka mingi huku maandamano yakizuka kuhusu kifo cha mwanamke mwenye umri wa miaka 22 chini ya ulinzi wa polisi wa maadili wa serikali hiyo. Kifo cha Masha Amini chini ya ulinzi wa Polisi, ni shimo jengine katika taswira iliyochanika inayoonyeshwa kwa Uislamu na Shariah na nchi za Magharibi. Kwa kuzingatia taswira hii dhaifu inayoendelea kuporomoka na kuwaponda Waislamu kimwili, kisaikolojia na kiroho kana kwamba Kiislamu ni dalili ya ujinga. Kulingana na makadirio kuna Waislamu bilioni 1.9 ulimwenguni na kuna karibu nchi 50 zenye Waislamu wengi. Nyingi kati ya nchi hizo zinadai kuwa na Uislamu kama dini ya Dola yao na zote zinakubalina wao kwa wao kama dola za Kiislamu huku zikifuata toleo la Uislamu unaofafanuliwa na mwanadamu.
Matukio kama haya yameangaziwa sana na nchi za Magharibi na kuonyeshwa kama matokeo ya moja kwa moja ya sheria za Kiislamu, ingawa hali hiyo hiyo au mbaya zaidi imetokea kwa wanawake wa Kiislamu katika nchi za magharibi lakini katika kesi hizo kitu pekee kinachoweza kuhusishwa na Uislamu ni dini ya wahasiriwa. Ili kupambana na kashfa hii, wanaodhulumiwa wanapaswa kunyanyuka kifikra juu ya kiwango cha dhalimu na kukataa toleo lililozuliwa la mifumo ya Kiislamu. Jambo la kushangaza ni kwamba mtuhumiwa na mwathiriwa wote wanadai kutoka katika imani moja na wanatenda ipasavyo kulingana na madai yao wenyewe. Hii inaonyesha kwamba kuna imani ya tatu ambayo wote wawili wanaitekeleza na hiyo ni imani ya "mwenye nguvu mpishe" au "nitafanya, nikiweza". Pande zote mbili zinaamini kutawaliwa kwa hiari ya mwanadamu, na upande wenye nguvu zaidi ndio unaoshinda. Vivyo hivyo ndivyo hali ilivyo katika utawala wa Kiislamu nchini Iran ambapo ujamaa, utaifa na uliberali vyote vimecheza dori muhimu katika mapinduzi ya 1979. Hata hivyo baadaye iliitwa "Uislamu" kwa msisitizo mkubwa kwamba hili hatimaye likawa kivumishi chake pekee.
Muislamu anaamini Utukufu wa Mwenyezi Mungu (swt) na katika kunyenyekea na kumtii Yeye kikamilifu. Hajapewa haki ya kuchagua na kuchagua kutoka kwa amri zilizotolewa au kupendekeza kutoka kwa akili yake mwenyewe. Kujisalimisha huku kunakotakiwa hakuwezekani bila ya kutabikisha Mifumo ya Kiislamu katika sura zake safi kabisa, na katika hali ya sasa inayofanya kazi kwa ajili ya kusimamisha Dola itakayosimamia mambo ya watu wake na pia watu wanaosubutu kulichafua jina la Uislamu. Sheria za Mwenyezi Mungu (swt) zinatekelezeka kwa jinsia zote mbili, lakini kwa njia tofauti. Mkanganyiko ulisababishwa na akili ya mwanadamu na kupatilizwa na wale ambao wangeweza kunufaika nao, kwa hivyo kufanana kubadilishwa kuwa sawa. Kuporomoka na kuvunjwa kwa Dola ya Kiislamu kumeweka kila mtu katika hali ya kung’ang’ana kuishi. Waislamu waliotawanyika wakawa hawana usalama, na mapendekezo na ushauri ambao haukutoka kwenye Uislamu ulianza kuingia ndani.
Wanawake walihisi kunyimwa na kudhulumiwa na kuwaona wanawake wa Kimagharibi wakipigania haki zao za kimsingi, na mazingira ya kijamii yaliyowekwa yaliwapa chaguo hili la kupigania kitu ambacho kamwe hawakukipigania hapo awali. Waliheshimiwa na kutunzwa vyema na hata ikitokea dhulma yoyote walikuwa na majaji wa kuwafikia wakijua hilo na kupigania usawa uliocheleweshwa na kuwapotosha wanawake kutoka kwenye jambo hilo na Magharibi inatumia kila fursa iwezekanayo kuendelea kuwapotosha.
Suluhisho liko chini ya kivuli cha Khilafah, ambapo uadilifu ni wa kiwahyi na sio tu kwa ajili ya adhabu bali pia kwa ajili ya ulinzi. Uislamu unamlinda mwanamke kwa njia ya heshima kiasi kwamba hata likitokea suala kama hili atakuwa na mwanamume ambaye Mwenyezi Mungu amemuwajibisha kwa ajili yake mwenye kusimama mbele yake na ataulizwa kwa sababu yoyote inayowezekana kuanzia kwenye wendawazimu hadi ujinga.
Kamwe katika historia ya utawala wa Kiislamu mfumo wake wa haki haujawahi kumtesa au kumdhulumu mwanamke ili kumfanya afuate sheria. Mateso na unyanyasaji huu umekuwa na bado ni mtindo wa makafiri. Kuanzia kwa Hadhrat Sumayyah hadi kwa dada yetu mpendwa Aafia Siddiqui, kila walipoweka makucha yao kwa wanawake, waliteseka. Sasa ni wakati wa kusimama, kuchukua msimamo na kukataa kudanganywa. Mwenyezi Mungu (swt) ni الْمُقْسِطُ Al-Muqsit (Mwadilifu) na ametupa mpango kamili wa utekelezaji, unaoanza na kusimamishwa kwa dola ya Kiislamu na kabla ya hapo juhudi za kusimamishwa kwake. Hadi wakati huo watu watabaki kama nyasi zinazoumia pindi tembo wanapiganapo.
(وَأَنَّ هَذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ وَلا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَنْ سَبِيلِهِ ذَلِكُمْ وَصَّاكُمْ بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ)
“Na kwa hakika hii ndiyo Njia yangu Iliyo Nyooka. Basi ifuateni, wala msifuate njia nyingine, zikakutengeni na Njia yake. Haya amekuusieni ili mpate kuchamngu.” [Al-An’am: 153]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan