Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari na Maoni
Afrika Yataabika Kutokana na Ukoloni Umagharibi na Yahitaji Khilafah Kukombolewa

Habari:

Nigeria, ni taifa lenya uchumi mkubwa na watu wengi Afrika limeipita India na hivi sasa ndilo lenya idadi kubwa ya watu walio katika umasikini wa kupindukia duniani! Kenya, ni taifa lenye uchumi mkubwa na ambalo ni kituo cha biashara Afrika Mashariki na Kati, ina takribani watu milioni 1.2 wamo hatarini kufa njaa kutokana na ukame. Na jumla zaidi ya Wakenya takribani milioni 14.7 hawana chakula kwa msimu huu wa kiangazi unaoendelea. Kwa ujumla nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi ndani ya Afrika ziko katika usambaratifu mkubwa!

Maoni:

Mataifa yaliyotajwa ni mfano tu wa hali ilivyo Afrika kutokana na muendelezo wa utekelezaji wa sera za kisekula za kirasilimali ambazo bara hili na uongozi wake umezirithi kutoka kwa mabwana Wamagharibi. Wakoloni ndio ambao walitekeleza uhalifu wa kupindukia kwa wanadamu kwa njia ya utumwa wa kiakili kwa Waafrika kama ilivyosimulia na Hendrik F. Verwoerd, "Hakuna nafasi kwa Muafrika katika jamii ya Kizungu isipokuwa ngazi ya ufanyikazi aina fulani. Mpaka sasa, Muafrika tumemfunga katika nidhamu ya masomo/shule inayomuweka mbali na jamii yake na kumpotosha kwa kumuonyesha kuwa kuna matumaini ndani ya jamii ya Kizungu ambapo haruhusiwi kufaulu." Uhalifu mwengine ni wa utumwa wa kiwiliwili kwa watu wa Afrika na uporaji wa rasilimali zao kama ilivyosimuliwa na Sir Andries Stockkenstrom, "Suali la kuiba ardhi za wenyeji sio kwamba ni sawa au ni makosa kupora ardhi zao, kuwaua na kuwaangamiza Wahottentot, Makafiri…suali rahisi ni je ITALIPA? Lakini ikiwa Bibilia na umishenari utakuwa kikwazo katika njia hii iliyo na faida mara elfu moja…Lau kwa kifupi, hazitoweza kupigia debe kazi ya uporaji mali…basi mtutu wa bunduki utatumika na kuwa ndio njia ya usambazaji wa hadhara yetu ili kufikia malengo." Zaidi ya hayo, mwanafilosofia wa Kiingereza,Betrand Russell, aliandika kuhusu historia ya maangamivu ya ukoloni na kuandika kuwa, "Kila kijiji kiliamrishwa na utawala kukusanya na kupeleka kiasi fulani cha raba –kiwango ambacho wanaume watakachoweza kuleta na kutelekeza kazi za kusimamia maisha yao. Lau watafeli kupeleka kiwango kinacho stahiki, wanawake wao walichukuliwa na kuwekwa kama mateka…katika majumba ya wafanyikazi wa serikali ya kikoloni. Lau mbinu hiyo ikifeli…wanajeshi hutumwa katika vijiji ili kuwatisha, na ikibidi hata kuwaua baadhi ya wanaume…waliagizwa kupeleka mkono wa kulia uliokatwa kutoka kwa muhanga wa Kiafrika kwa mujibu wa kila risasi iliyotumika."

Majanga hayo yalifanywa na Wamagharibi wakoloni wakiongozwa na Uingereza, Ufaransa na washirika wao pale walipokuwa ndio dola kubwa duniani zenye usemi. Amerika ilipoibuka kidedea baada ya Vita vya Pili vya Dunia ilikuwa kinara wa ulimwengu na ilisonga mbele na kuanza kunyang'anyira pande la makoloni kwa kushindana na Ulaya! Hivyo basi, Amerika kupitia vibaraka wao watiifu Waafrika viongozi wakakuza wimbi la uasi barani kwa kisingizio cha kutaka uhuru kutoka kwa ukoloni wa Ulaya! Natija yake ni kwamba Ulaya ili patiliza uasi huo na kuutumia kwa maslahi yao na kubakisha hali halisi kwa sura ya kutoa uhuru bandia wa bendera lakini ikabakisha muundo jumla wa serikali ukiwa na watawala vibaraka wakoloni kuendelea kuhudumia maslahi yao! Kwa hivyo, Amerika ikasonga mbele na kubuni chaguzi za kidemokrasia ili kuweza kuwaondosha vibaraka wa Ulaya mamlakani na kuweka watawala vibaraka wa Marekani na ikiwezekana kufanya mapinduzi! Sera hii ya kuzozania Afrika baina ya Ulaya na Amerika inaendelea hadi leo! Ruwaza yao kuhusu Afrika ni moja nayo ni kuitawala, kuipora na kuwafanya watu wake watumwa kama wafanyikazi kwa malipo duni! Tofauti pekee ni kuwa Amerika na washirika wake hivi sasa wanaendeleza vita vya wazi na vya kiulimwengu dhidi ya Uislamu na Waislamu kupitia eti 'vita dhidi misimamo mikali na ugaidi.' Lengo likiwa ni kuukashifu Uislamu na Waislamu kama mfumo mbadala kwa mfumo wao wa kisekula wa kirasilimali ambao umeleta majanga duniani kote kiasi kwamba hata kipofu anaweza kuona ufisadi unaoendelezwa katika kila nyanja ya maisha! Kuongezea ni kuwa mwishowe ni kutia wasiwasi na mchanganyiko kwa wanadamu hususan Waislamu ili wasiutazame Uislamu kama mfumo badala ulio na uwezo wa kutatua matatizo yanayo wakumba hivi sasa duniani kote.

Hali ya sasa ya Afrika ni sawa na ilivyo duniani kote hususan Mashariki ya Kati ambayo ili shuhudia kugawanywa kwa iliyokuwa Dola Moja ya Serikali ya Kiislamu ya Khilafah na kuwa vijidola 54 vikiongozwa na watawala watumwa wa wakoloni ambao daima hutafuta muongozo kutoka Washington, London na Paris! Kugawanywa huko kulikamilika 3 Machi 1924M ambapo Khilafah ilivunjwa! Suluhisho pekee lipo katika kuwaondosha watawala vibaraka wakoloni pamoja na mfumo wao wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake. Hilo lawezekana kupitia kukumbatia mwito wa ulinganizi wa Khilafah kwa njia ya Utume ambao umetapakaa duniani na unaopigiwa debe na Hizb ut Tahrir. Ni kupitia Khilafah pekee ndipo masekula warasilimali pamoja na sera zao watafurushwa na kuachana na uporaji wa Afrika, Mashariki ya Kati n.k kupitia utekelezwaji wa sera na sheria zao ovu. Khilafah itahakikisha kupatikana kwa utulivu, maendeleo na ufanisi wa kweli kupitia utekelezwaji wa Shari'ah (Qur'an na Sunnah) kwa ukamilifu ikiongozwa na kiongozi Khalifah ambaye anatafuta Pepo ya juu kwa kujifunga na utafutaji wa radhi za Mwenyezi Mungu (swt)

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Hizb ut Tahrir na
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:34

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu