Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Miaka 100 Bila Khilafah: Ummah Unaendelea Kuzama Katika Mizozo ya Kikabila

Habari:

         Jamii za Garre na Murule kutoka Kaunti ya Mandera nchini Kenya zimekuwa zikipigana kwa miaka kuhusiana na mipaka, malisho na maji pamoja na rasilimali nyingine muhimu. Jamii hizo zinazo zozana zililetwa pamoja na Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Ushirikiano (NCIC) na maafisa kutoka serikali za Kitaifa na Kaunti. NCIC iliunda kamati ya upatanishi ili kuleta amani chini ya mwenyekiti Sheikh Umal. Mnamo Jumatatu, 8 Februari 2021 pande hizo mbili zilitia saini makubaliano ya amani yaliyokuwa na idadi ya maamuzi. Miongoni mwa maamuzi hayo ni kuweka faini ya ngamia 350 kwa watakao vunja makubaliano hayo. Kwa kuongezea, malipo ya Sh60,000 ($600) kwa wale watakao patikana na makosa ya ubakaji. (Vyombo vya habari Kenya).

Maoni:

Mzozo baina ya jamii mbili hizi umekuwepo kwa muda mrefu na umekuwa ukizidi kutokana na kung’ang’ania uongozi wa kisiasa mashinani. Haya ni makubaliano ya pili ya amani baada ya kwanza yaliyotiwa saini mnamo 2005 pasi na kufaulu. Pande zinazopigana ni sehemu ya Ummah wa Waislamu uliotapakaa duniani kote na kufisidika na ugonjwa wa ‘usekula.’ Maradhi hayo yamepenya katika fikra, fahamu na vitendo vya Ummah. Kiasi kwamba umebeba utambulisho wa kisekula na kujitolea kwake!

Hatimaye, wamejifunga na mfumo wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake kusimamia mambo yao. Hata hivyo, wametosheka na kuwa Waislamu ambao wanatenda baadhi ya ibada za kiroho!  Kwa upande mwingine, wakizikwepa aya za Mwenyezi Mungu (swt) aliposema:وَمَن لَّمۡ يَحۡڪُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُوْلَـٰٓٮِٕكَ هُمُ ٱلظَّـٰلِمُونَ “Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhalimu.” [Al-Ma’idah: 45].وَمَن لَّمۡ يَحۡڪُم بِمَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ فَأُوْلَـٰٓٮِٕكَ هُمُ ٱلۡفَـٰسِقُونَ “Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu basi hao ndio wapotofu.” [Al-Ma’idah: 47]. Kwa kuongezea, Rasulullah (saw) ameharamisha mizozo aina hiyo aliposema: «لَيْسَ مِنَّا مَنْ دَعَا إِلَى عَصَبِيَّةٍ، وَلَيْسَ مِنَّا مَنْ قَاتَلَ عَلَى عَصَبِيَّةٍ، وَلَيْسَ مِنَّا مَنْ مَاتَ عَلَى عَصَبِيَّةٍ» “Sio katika sisi yule anayelingania ‘Uasabiyyah, sio katika sisi yule anayepigana kwa ajili ya ‘Uasabiyyah, na sio katika sisi yule anayekufa kwa sababu ya ‘Uasabiyyah.” [Sunan Abu Daud].

Aya na hadith hizo ziko wazi kuwa Sharia’h ya Kiislamu ndio muongozo msingi pekee. Hivyo basi, makubaliano haya mapya si lolote bali ni hewa moto ambayo itapotea punde tu wino utakapogusa karatasi! Kwani masuala msingi hayaja suluhishwa ambayo ni ukandamizaji wa kimfumo kutokana na nidhamu za kisekula zinazo watawala na kuwa chanzo cha mizozo hiyo. Na ndio maana vyombo vya habari vikuu vikatekwa na faini ya kosa la ubakaji! Na kuwapelekea ‘watetezi wa wanawake’ kuzusha gumzo katika mitandao ya kijamii kwa kukashifu hilo badala ya kujadili kuhusu mchakato fisadi na mbaya usiokuwa wa Kiislamu.

Naam, maamuzi yao yako sawa kwa kuwa yapo ndani ya uhuru wa kidemokrasia kuweka maamuzi aina hiyo! Lakini, wamekosea kwa kuzingatia Shari’ah ya Kiislamu. Suala la ubakaji ni kitendo cha kumvunjia heshima mwanamke.  Zipo rai mbili kuhusiana na adhabu yake baada ya kupatikana ushahidi: kwanza- sawa na kosa la uzinifu. Lau mtendaji ameoa basi anapigwa mawe hadi kufa. Lau hajaoa basi anapigwa mboko mia na kufurushwa nje ya mji kwa mwaka mmoja. Pili- lau mtendaji ametumia silaha kutenda kitendo hicho basi ima anauliwa au anasulubiwa au anakatwa mikono na miguu kwa kupishana au anafurushwa nje ya mji. Moja kati ya rai hizo zinaweza kuchukuliwa pamoja na mtendaji kumpa mwanamke malipo ‘mahari’ au la.  [Muwatta Malik] na [Al-Ma’idah: 33]. Kufanyiwa kazi kwa moja kati ya rai hizo kunategemea kuwepo kwa nidhamu ya Khilafah ambayo haipo leo. Kwa hiyo, tunatakiwa kujumuisha juhudi zetu ili kurudisha maisha ya Kiislamu kwa kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Ni Khilafah pekee ndio inayoweza kulinda damu, mali na heshima za watu pasina kuzingatia jinsia na dini zao. Kutawaliwa na ukafiri kunatuletea idhilali hapa duniani na Akhera.

#أقيموا_الخلافة               #خلافت_کو_قائم_کرو

#ReturnTheKhilafah          #YenidenHilafet          #TurudisheniKhilafah

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro Ali

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu