- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kesi ya Mauaji ya Daniel Pearl ni Mfano Wazi wa Jinsi Watawala wa Pakistan Wanafuata kwa Upofu Matakwa ya Amerika
Habari:
Katika "Taarifa yake kupitia Kaimu Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jeffrey A. Rosen juu ya Mashtaka ya Pakistan yanayohusiana na Utekaji nyara na Mauaji ya Daniel Pearl" Bwana Rosen alitoa taarifa ifuatayo mnamo tarehe 29 Disemba 2020, "Tunaelewa kuwa mamlaka za Pakistan zinachukua hatua kuhakikisha kuwa Omar Sheikh anasalia kizuizini wakati Rufaa ya Mahakama ya Upeo inayotaka kuregesha kifungo chake ikiendelea. Maamuzi tofauti ya mahakama yanayobadilisha hukumu yake na kuagiza aachiliwe huru ni dharau kwa waathiriwa wa ugaidi kila mahali. Tunabaki wenye shukrani kwa hatua za serikali ya Pakistan kukata rufaa kwa maamuzi kama haya ili kuhakikisha kwamba yeye na washtakiwa wenzake wanawajibishwa. Ikiwa, hata hivyo, juhudi hizo hazitafanikiwa, Amerika iko tayari kumzuilia Omar Sheikh ili kushtakiwa hapa. Hatuwezi kumruhusu kukwepa haki kwa dori yake katika kutekwa nyara na kuuwawa kwa Daniel Pearl."
Maoni:
Omar Sheikh alikamatwa mnamo 2002 akihusishwa na mauaji ya mwandishi wa habari wa Amerika jijini Karachi na alishtakiwa kuhusiana na kuhusika katika mauaji hayo. Omar alizuiliwa gerezani kwa miaka kumi na nane iliyopita. Alipewa hukumu ya kifo kutoka kwa Mahakama ya Kupambana na Ugaidi, ambayo ilifutwa na Mahakama Kuu ya Sindh. SHC ilimpa miaka saba gerezani kama adhabu kwa dori yake, mnamo Aprili 2020. Kwa sababu ya kufungwa kwake kabla ya uamuzi huu wa rufaa, muda wa adhabu ya Omar ulionekana kuwa umetumika. Kwa hivyo chini ya sheria ya Pakistan kuachiliwa kwake kulikuwa maarufu. Lakini, ili kumridhisha bwana wake wa kikoloni, serikali ya Bajwa-Imran ilimzuilia Omar chini ya Sheria ya Udumishaji Utangamano wa Umma (MPO). Pia iliwasilisha rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama Kuu ya Sindh katika Mahakama ya Upeo ya Pakistan. Mnamo Disemba 2020, mahakama kuu ya Sindh ilitangaza kuzuiliwa kwa Omar Sheikh, chini ya MPO, kinyume cha sheria. Iliamuru aachiliwe huru mara moja. Lakini, Omar bado hajaachiliwa, kwa sababu ya utiifu wa serikali kwa Amerika.
Katika nidhamu hii ya mahakama ya wakoloni, iliyoachwa nyuma na Raj wa Uingereza kama pigo la kugawanya watu, haki ni mtumwa wa watu wenye nguvu. Hukumu mwanana hutolewa kutoka mahakamani na wenye nguvu, wakati watu wakiamriwa kuheshimu na kutii sheria. Ikiwa wenye nguvu hawatatoa uamuzi mwanana, wanaipuuza tu. Wanaweza hata kuivunja mahakama hiyo, kama ilivyotokea katika kesi ya uhaini ya Pervez Musharraf. Mahakama ya wakoloni ilimwachilia huru muuaji wa Wapakistani wawili, Raymond Davis, mara moja akamkimbiza Amerika. Lakini, imezuia kuachiliwa kwa Mpakistani, ambaye amri zake za kutolewa zimetolewa na korti. Kwa maana hii, kesi hiyo inafanana na ile ya Naveed Butt, ambaye anasalia kupotezwa kwa lazima licha ya mamlaka ya kisheria kutoa agizo la kumtoa mnamo Januari 2018. Na kuna kesi nyengine nyingi zinazofanana na hizi.
Hakika Khilafah kwa Njia ya Utume itatukomboa kutoka kwa utumwa huu mbaya wa wakoloni. Nidhamu ya mahakama ya Khilafah itaamua mambo kwa msingi wa Quran na Sunnah pekee. Ndani ya Khilafah, watawala hawataiogopa Amerika na kuzingatia maagizo yake, badala yake, watamuogopa Mwenyezi Mungu (swt) Pekee na kuhakikisha kutii amri Zake, na kando na nyengine zote. Ndani ya Khilafah, raia hawatalazimika kuvumilia kupotezwa kwa lazima au kuwekwa kuzuizini kwa matakwa ya Amerika. Ndani ya Khilafah, watu hawatalazimika kuhama kutoka nguzo hadi nguzo ili kupata haki, wakitumia miaka au miongo mingi. InshaAllah katika Khilafah inayokuja, watawala watawapenda raia wao na raia watawapenda watawala wao. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,
«خِيَارُ أَئِمَّتِكُمُ الَّذِينَ تُحِبُّونَهُمْ وَيُحِبُّونَكُمْ وَيُصَلُّونَ عَلَيْكُمْ وَتُصَلُّونَ عَلَيْهِمْ وَشِرَارُ أَئِمَّتِكُمُ الَّذِينَ تُبْغِضُونَهُمْ وَيُبْغِضُونَكُمْ وَتَلْعَنُونَهُمْ وَيَلْعَنُونَكُمْ»
“Bora wa viongozi wenu ni wale ambao mnawapenda na wanakupendeni na wanakuombeeni na mnawaombea. Na waovu wa viongozi wenu ni wale ambao mnawachukia na wanakuchukieni na mnawalaani na wanawalaani.” (Muslim).
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Asghar Ahmed – Pakistan