- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Misikiti Nchini Turkmenistan Imesalia Kufungwa
Habari:
Kama sehemu ya hatua za kuzuia dhidi ya kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza, misikiti ya nchi hiyo itabaki imefungwa hadi tarehe 1 Januari 2021, iliripoti Turkmenportal kwa mujibu wa Muftiate wa Turkmenistan.
Hatua hizi zilichukuliwa kulingana na uamuzi wa Tume ya Mambo Yasiyo ya Kawaida ya Turkmenistan kwa ajili ya Mapambano dhidi ya Magonjwa kutoka tarehe 26 Agosti 2020. Turkmenportal iliripoti mapema kwamba Rais wa Turkmenistan Gurbanguly Berdimuhammedov yeye mwenyewe alitia saini amri juu ya muundo wa Tume hiyo ya Mambo Yasiyo ya Kawaida ya Turkmenistan ili Kupambana na Kuenea kwa Magonjwa, ambayo itazuia kuenea kwa maambukizi kote nchini.
Maoni:
Kumbuka kwamba kwa msingi wa agizo la Muftiate wa Turkmenistan na kulingana na "Mpango wa Kujitayarisha kwa Turkmenistan ili Kukabili Janga la virusi vya Korona na Kuchukua Hatua za Kujibu kwa Haraka", misikiti yote nchini Turkmenistan ilifungwa kutoka Julai 13 hadi Julai 31, na baada ya hapo hatua hizi ziliongezwa muda hadi Desemba 1.
Wakati huo huo, taasisi zingine zote nchini - masoko, taasisi, shule, nk zinafanya kazi kama kawaida. Ni vyema kutaja pia kuwa hadi leo mamlaka za Turkmen hazijatambua ukweli kwamba kuna watu wameambukizwa na virusi vya Korona nchini.
Ikumbukwe kwamba Turkmenistan sio nchi pekee katika eneo hilo ambapo chini ya kisingizio cha kupambana na kuenea kwa virusi vya Korona, misikiti bado imefungwa, wakati taasisi zingine zote za umma zikibaki zimenguliwa. Kwa mfano, nchini Tajikistan taasisi zote, pamoja na shule, vyuo vikuu na masoko, hufanya kazi kama kawaida, wakati misikiti kote nchini bado imefungwa.
Vitendo hivi vya mamlaka za nchi za Asia ya Kati ni ishara nyingine tu ya lengo kuu la sera zao za kigeni - vita dhidi ya Uislamu na kuzuia mwamko wa Kiislamu katika eneo hilo, kwa sababu ni kwa lengo hili pekee serikali hizi za kidhalimu ziliasisiwa katika eneo hili na zinasalia kulindwa na Urusi na Amerika.
Kila hatua ya serikali hizi inaelekezwa kwa lengo lao kuu, na, kwa kawaida, pindi kisingizio rahisi cha kufunga misikiti kama janga la virusi vya Korona kilipoonekana, hawakusita kukitumia. Lakini, hatua hizi zote dhidi ya Uislamu hazizuii kwa vyovyote mwamko wa Kiislamu katika eneo hilo, badala yake, zinajaza kikombe cha uvumilivu wa watu kuleta mlipuko wa kisiasa, ambao mapema au baadaye utatokea kwa sababu ya uchovu wa idadi ya watu kutokana na madhalimu wa kisekula, ambao wamekuwa wakiwatesa kwa karibu miongo mitatu.
Bila shaka, wakati wa uasi-sheria kwa madhalimu utamalizika hivi karibuni, kama vile utakavyomaliza utawala wao wa kidhalimu wa kikafiri na uhalifu dhidi ya waumini. Mwenyezi Mungu Mtukufu asema:
]يُرِيدُونَ أَن يُطْفِئُوا نُورَ اللَّهِ بِأَفْوَاهِهِمْ وَيَأْبَى اللَّهُ إِلَّا أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ]
“Wanataka kuizima Nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao, na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.” [TMQ 9:32].
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammad Mansour