Bangladesh Yazidi Kutumbukia ndani ya Mtego wa Indo-Pasifiki Uliotegwa na Marekani Mkoloni Mwenye Kiburi
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Ripoti ya hivi punde ya Pentagon ilisema kwamba viongozi wa kijeshi wa Marekani wameanza kufanya maandalizi ya kulinda maslahi ya Marekani katika eneo la Indo-Pacifiki. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Marekani inafanya mazoezi ya kijeshi na kubadilishana mipango na nchi mbalimbali za eneo la Indo-Pacifiki kwa malengo maalum. Makamanda wa Komandi ya Indo-Pacifiki ya Marekani walisisitiza kuongezeka kwa ushirikiano katika eneo lote.