Rajab Mwezi ambao watu wa Yemen waliukubali Uislamu na ndani ya mwezi huo huo Khilafah Ilivunjwa
- Imepeperushwa katika Yemen
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Tarehe Ishirini na nane Rajab yapita kila mwaka kwa Ummah wa Kiislamu ikileta ndani yake machungu ya kumbukumbu ya kuvunjwa Khilafah mwaka wa 1342 Hijria sawia na 3 Mach 1924 Miladi. Mwaka huu 1440 Hijria, tunakaribia mwisho wa karne moja bila kua chini ya kivuli cha Khilafah (wala sio siku tatu na usiku wake), wakati wa kuchagua Khalifah na kumpa bay’ah kuhukumu kwa kitabu cha Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume wetu Muhammad (saw).