Ongezeko la Takwimu Sio Jipya Bali Halina Budi kwa Zabuni za Kifedha Kabla ya Kongamano la Wafadhili la Brussels kwa Ajili ya Syria
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Vita katili nchi Syria dhidi ya raia vimeingia mwaka wake wa tisa mnamo Machi 15. Zaidi ya watu nusu milioni wamekufa, kwa mujibu wa ripoti za kimataifa, na shirika la Uangalizi wa Haki za Kibinadamu la Syria limenakili vifo 19800 vya watoto tangu 2011. Inakisiwa watoto milioni 8.6 wanahitaji msaada wa dharura, na sasa zaidi ya watoto milioni 6 hawana makao au wanaishi kama wakimbizi, na baadhi ya milioni 2.5 yao hawendi shule. Zaidi ya watoto milioni 3 wako katika hatari ya mabomu ya ardhini, huku takriban asilimia 40 ya wale waliouwawa na mabomu ya ardhini wakiwa ni watoto.