Jarida la Al-Waie: Vichwa Vikuu vya Habari vya Toleo (467)
- Imepeperushwa katika Jarida la Al-Waie
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Jarida la Al-Waie: Vichwa Vikuu vya Habari vya Toleo (467)
Jarida la Al-Waie: Vichwa Vikuu vya Habari vya Toleo (467)
Macho ya Waislamu kwa jumla, na waandishi wa habari, wachambuzi, waangalizi, na wale wanaohusika hasa, yanaelekea Ikulu ya White House, na kwenye matokeo ya mikutano ya Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi, Benjamin Netanyahu. Je, Trump atamshinikiza Netanyahu kukubali kwa upole kusitisha vita vyake dhidi ya Gaza?
Ujumbe kutoka Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Lebanon, unaojumuisha Dkt Muhammad Jaber na Mhandisi Saleh Salam, kama sehemu ya kampeni ya kuwatembelea wabunge, walimtembelea Mbunge Dkt. Imad Al-Hout jijini Beirut kwa takriban saa moja.
Mwenyezi Mungu (swt) alipowapa watu wa ash-Sham baraka za kumwangusha dhalimu mhalifu wa Syria, asubuhi ya tarehe 8 Disemba 2024, licha ya mipango na njama kubwa zilizopangwa na ulimwengu wote wa Magharibi, ukiongozwa na Marekani, ili kuyabatilisha mapinduzi na kuyazuia yasifikie lengo lake, ulikuwa ni utashi, azma, na Iman ya watu ash-Sham, kwa zana zao hafifu na za kawaida, ambapo hatimaye walishinda dhidi ya jumuiya ya kimataifa.