Jumatano, 09 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir:

Kampeni ya Kitengo cha Wanawake ya Ramadhan “Ramadhan ni Mwezi wa Ushindi”

Karibu Ramadhan, mwezi wa ushindi, mwezi wa bishara njema, mwezi wa kujadidishwa imani na kutakasa nyoyo, mwezi wa utiifu na kushindana katika mambo mema. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu aliyetufikisha Ramadhan, mwezi huu mtukufu ambao tunahisi ndani yake maana ya rehema na umoja baina ya Waislamu. Karibu, Ramadhan.

Je, Ramadhan ni mwezi wa ushindi kwa Waislamu wa Gaza, mwezi wa ushindi kwa Waislamu wa Palestina?

Ushindi kwa wale wote walio imara na kushikamana na ahadi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na bishara njema ya Mtume wake (saw), katika nchi za Syria, Sudan, Myanmar, Kashmir, Turkestan Mashariki, India na duniani kote.

Katika kipindi cha miaka mia moja iliyopita, Umma wa Kiislamu umepoteza maisha na mali zisizohesabika, umekumbwa na maafa, umeshuhudia vita vya kikatili, na kuzuiwa kutekeleza ibada zake za kidini, zikiwemo saumu, swala na mavazi ya Kiislamu.

Lakini haukujisalimisha au kushindwa kwa sababu Umma huu lazima uwe na ushindi. Ndio maana unawaona makafiri wanakimbilia kwenye chinjachinja na mauaji ya halaiki na hata kutaka kufutwa kwa mwezi wa Ramadhan kwa sababu wanauogopa, kwa sababu ni mwezi ambao Waislamu wako karibu na Mola wao, wakiitamani zaidi Pepo na neema zake, na kukumbusha zaidi historia, ufunguzi na ushindi walioupata mujahidina. Majaribio yote haya ya uoga ya makafiri yanathibitisha kuwa Ramadhan ni mwezi wa ushindi kwa Waislamu.

Kwa hivyo, lengo letu katika mwezi huu mtukufu lazima liwe kuunganisha safu za Waislamu, na sisi sote tuna imani na hakika kwamba ushindi unakuja, ulimwengu wote utashuhudia, na makafiri watapata fedheha ya kushindwa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Sisi katika Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir, tunakualikeni kuungana nasi katika kuunganisha maana ya ushindi na ujumbe wake na kueneza bishara njema yake sambamba na mwezi wa Ramadhan, mwezi wa ushindi, ushindi unakuja pasi na budi, na hakika Mwenyezi Mungu Mtukufu atatunusuru ikiwa tutamnusuru Yeye na kutembea kwenye njia ya haki ambayo kwayo wahyi ulishuka.


﴿وَأُخْرَى تُحِبُّونَهَا نَصْرٌ مِّنَ اللهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ﴾

“Na kinginecho mkipendacho, nacho ni nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini!” [As-Saff: 13]

Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari

ya Hizb ut Tahrir

Jumatatu, 01 Ramadhan 1445 H sawia na 11 Machi 2024 M

- Alama Ishara za Kampeni -

#رمضان_شهر_النصر

#RamadanMonthOfVictory

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu