Onyesho la Mshikamano nchini Malaysia huku Hali mjini Gaza Ikizidi kuwa Mbaya
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hali mjini Gaza inazidi kuwa mbaya. Umbile haramu la Kiyahudi linaendelea na mashambulizi yake, na kusababisha idadi ya vifo ambayo sasa imefikia 37,000, na zaidi ya 82,000 kujeruhiwa. Inajulikana sana kuwa hakuna maeneo salama kabisa yaliyosalia kwa wakaazi wa Gaza kutafuta kimbilio kutokana na mashambulizi ya umbile hilo haramu la Kiyahudi. Takriban Waislamu wote wa Gaza sasa wanalazimika kuyahama makaazi yao, wakitafuta hifadhi hadi kusini mwa Rafah, karibu na mpaka wa Misri.