- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Halaqa ya Mjadala Mjini Yalova Kutafuta Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi
Ndani ya wigo wa msururu wa makongamano, semina na halaqa zilizoandaliwa na Hizb ut-Tahrir / Wilayah Uturuki chini ya kichwa "Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi", na sanjari na mnasaba wa kumbukumbuka ya miaka 101 Hijria ya kuvunjwa Dola ya Khilafah mnamo tarehe 28 Rajab Muharram 1342 H, Hizb ilikutana na wawakilishi wa vyama vya kisiasa, mashirika yasiyo ya kiserikali, wawakilishi wa vyombo vya habari vya ndani na walezi katika mji wa Yalova katika jimbo la Bursa.
Wazungumzaji katika mkutano huo walikuwa ni maustadh; Ali Tenjar, Musa Beyoglu, Mahmud Kar, Mehmet Emin Yildirim.
Katika mkutano huu, ilisisitizwa udharura wa kuwekwa masuluhisho na hukmu za Uislamu katika kila nyanja kwenye ajenda, na kwamba Uislamu una masuluhisho ya kina na ya asili katika utawala, uchumi, elimu na nyanja za kijamii, na kwamba ni lazima yabainishwe katika kila jambo.
Mkutano wetu ulimalizika kwa hamu na msisitizo juu ya udharura wa kuwekwa mikutano hii ya mashauriano na masuluhisho mara kwa mara katika maeneo yote.
Kwa Mengi zaidi Bonyeza Hapa
Jumapili, 19 Rajab Al-Muharram 1443 H sawia na 20 Februari 2022 M
https://hizb-uttahrir.info/sw/index.php/dawah/uturuki/2179.html#sigProIdf585fa5a49
Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki
Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki