Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Semina katika Mji wa Hatay iliolenga Kutafuta Suluhisho la Kiislamu la Mgogoro wa Kiuchumi

Ndani ya mwendelezo wa mfululizo wa makongamano na semina zilizoandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki chini ya kichwa "Suluhisho la Kiislamu kwa Mgogoro wa Kiuchumi", wawakilishi wa vyama vya kisiasa, mashirika yasiyo ya kiserikali, wawakilishi wa vyombo vya habari vya ndani na walezi walikusanyika mjini Hatay (Antakya).

Mazungumzo hayo yaliyoanza kwa hotuba ya ufunguzi wa Ustadh Ahmed Saba, yaliendelea kwa kuwasilishwa na Ustadh Musa Beyoglu, baada ya uwasilishaji, awamu ya maswali na majibu ilianza na baadhi ya washiriki walitoa mchango mkubwa kwa maswali yao na wengine kwa maoni yao. Maustadh Hakki Eren, Abdullah Imamoglu, Musa Beyoglu na Mehmet Hanafi Yaghmur wote walijibu maswali yaliyoulizwa.

Mtazamo wa pamoja wa wote waliohudhuria mkutano huo ulikuwa kwamba suluhisho na hukmu za Uislamu katika kila nyanja ziwekwe kwenye ajenda, na ikasisitizwa kwamba Uislamu una masuluhisho ya kina na ya kweli katika usimamizi, uchumi, elimu na nyanja za kijamii na kwamba yanapaswa kuonyeshwa katika kila jukwaa.

Mjumuiko wetu ulimalizika kwa hamu na msisitizo juu ya udharura wa kufanywa mikutano hii ya mashauriano na masuluhisho mara kwa mara katika maeneo yote.

Kwa Mengi zaidi Bonyeza Hapa

Jumapili, 27 Jumada al-Akhir 1443 H sawia na 30 Januari 2022 M

Kwa Maelezo Zaidi Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Ukurasa wa Twitter wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Akaunti ya Instagram ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Chaneli ya YouTube ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki

Tovuti ya Jarida la Kokludegisim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu