- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki: JOPO
“Kadhia ya Kikurdi na Utafutaji wa Suluhisho”
Katika msururu wa amali zilizopewa anwani: "Kadhia ya Kikurdi na Utafutaji wa Suluhisho", ambazo zilianza kwa toleo la Juni la Jarida la Koklu Degisim, ziliendelea na jopo lililofanyika jijini Istanbul. Jopo hilo, ambalo lilifanyika katika afisi ya Koklu Degisim Istanbul, lilihudhuriwa na Mahmut Kar, Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Uturuki, na Musa Bayoğlu, mwandishi wa Koklu Degisim, ama wageni wa studio, aliyekuwa mbunge wa Diyarbakir Altan Tan, mwandishi wa habari-mwandishi na naibu mwenyekiti wa Mazlum-der Kenan Alpay, wakili Nesip Yıldırım, kwa upande mwengine alishiriki mtandaoni.
Katika jopo hilo lililoendeshwa na mwakilishi wa Koklu Degisim Istanbul Muhammed Emin Yıldırım, Musa Bayoğlu alianza kwanza. Akitunuku hotuba yake kwa Sheikh Said wakati wa maadhimisho ya miaka 96 ya kuuawa kwake shahidi, Musa Bayoğlu alisema kwamba Sheikh Said, kama msomi wa kuigwa, hakunyamaza juu ya kuondolewa kwa Dini ya Mwenyezi Mungu na alijitoa uhai wake kuitetea Khilafah.
Baada ya hotuba ya Musa Bayoğlu, Mahmut Kar, Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Uturuki, aliingia sakafuni. Mahmut Kar alitoa mada iliyopewa anwani, "Sababu ya Kadhia ya Kikurdi", alielezea kwa mpangilio jinsi kadhia ya Kikurdi ilivyotokea. Mahmut Kar alisema kuwa sababu ya kwanza ya tatizo hilo ni kutenganishwa kwa Uislamu na maisha, sababu ya pili ni misimamo ya kitaifa ya utawala wa Kemal, na sababu ya tatu ilikuwa mahusiano machafu na dola za kikoloni za magharibi.
Baada ya uwasilishaji wa Mahmut Kar, naibu mwenyekiti wa Mazlum-der Nesip Yıldırım alishiriki katika kipindi hicho kupitia mtandaoni. Akijibu swali: "Je! Kadhia ya Kikurdi na suala la ugaidi ni sawa au ni vitu tofauti?", Nesip Yıldırım alisema kuwa kadhia ya Kikurdi ni suala gumu ambalo lilianza na kuondolewa kwa Khilafah na linaendelea leo kwa mwelekeo wake wa kijamii, kithaqafa na kisiasa, na kwamba PKK iliongeza kina cha tatizo hili kwa kugeukia ugaidi na ghasia.
Baada ya Nesip Yıldırım kumaliza hotuba yake, mwanahabari-mwandishi Kenan Alpay alijiunga na kipindi hicho akiwa mtandaoni. Akisisitiza kuwa haiwezekani kutatua kadhia ya Kikurdi kwa lugha ya utaifa, Kenan Alpay alisema kuwa suluhisho lipo katika udugu wa Kiislamu, katika ufahamu wa Ummah, na kwamba Waislamu nchini Uturuki wanapaswa kushauriana juu ya kadhia hii.
Baada ya tathmini iliyofanywa na Kenan Alpay, mbunge wa zamani wa Diyarbakır Altan Tan alikuwa mzungumzaji wa mwisho kuungana na kipindi hicho akiwa mtandaoni. Altan Tan, ambaye alisema kuwa Uturuki inapaswa kusuluhisha kadhia ya Kikurdi na mienendo yake yenyewe ya ndani (ya nyumbani), alisema kuwa hatua za serikali na upinzani ambazo huwaona Wakurdi kama bohari ya kura ni za kimatata, kwamba Chama cha Kidemokrasia na Watu (HDP) kinapaswa kukubaliana na Uturuki kwa suluhisho, na kwamba vita vitaleta maafa tu pekee kwa eneo zima alisema.
Baada ya Altan Tan kumaliza hotuba yake, Mahmut Kar, Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uturuki, alitoa mada kwa anwani "Hatua za Kuchukuliwa kwa Suluhisho la Mwisho la Kadhia ya Kikurdi" katika raundi ya pili. Baada ya tathmini ya Mahmut Kar, Musa Bayoğlu alitoa mada yake ya pili kwa anwani: "Suluhisho la Uislamu kwa Kadhia ya Kikurdi." Baada ya hotuba ya Musa Bayoğlu, kipindi hicho kilihitimishwa.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah ya Uturuki
https://hizb-uttahrir.info/sw/index.php/dawah/uturuki/1729.html#sigProId582cbaf260