Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Ubelgiji: Warsha ya Kisiasa:

“Ummah Bora umeletwa Wanadamu”

Kama sehemu ya amali za kiulimwengu zilizo zinduliwa na Hizb ut Tahrir katika kumbukumbu ya Hijria (Rajab 28, Muharram) ya kuangamizwa kwa dola ya Kiislamu (Dola ya Khilafah) kuwakumbusha Waislamu namna wakoloni walivyo koloni uvujwaji wa dola yao (khilafah) iliyo asisiwa na Mtume (saw) na Maswahabah zake, Hizb ut Tahrir / Ubelgiji iliandaa warsha ya kisiasa mjini Liège kwa anwani,

“Ummah Bora ulioletwa kwa Wanadamu”

Warsha ilianza kwa kusomwa Aya za Qur’an Tukufu katika ukumbi uliojaa wageni waheshimiwa, kisha kufuatiwa na hotuba ya ndugu Muhammad Yassin, “Hitajio la Utu katika Ufunuo” na vipi ummah unaamini ufunuo huu na kuweza kuongoza kwa mwamko sahihi.

Mada ya pili iliwasilishwa na mgeni kutoka Uturuki, Shaikh Abdullah Imam Oglu, “Namna ya kuukomboa Ummah wa Kiislamu kutoka katika Ukoloni na kuurudisha kuwa ummah bora.” Alisisitiza juu ya umuhimu wa kufanyakazi kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu kupitia kuasisi Khilafah na namna ambavyo hili litaregesha fahari yetu na kuinua hadhi yetu. Alihitimisha mazungumzo yake kwa mifano katika historia ya Khilafah.

Jumapili 01, Sha’aban 1440 H  -  07, Aprili 2019 M

Naibu wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ulaya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu