- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi ya Ukombozi: “Na Saidianeni katika Wema na UchaMungu wala Msisaidiane katika Uovu na Uadui”
Matembezi ya 65 yalianzia mbele ya Msikiti wa Al-Fath katika mji mkuu wa Tunis, baada ya swala ya Ijumaa, mnamo tarehe 3 Januari 2025 yalioandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia kuwanusurur watu wa Palestina na Al-Aqsa iliyo mateka, na kichwa chake kilikuwa “Na Saidianeni katika Wema na UchaMungu wala Msisaidiane katika Uovu na Uadui!” na matambezi haya yaliyohudhuriwa na umati mkubwa wa watu yalizunguka katika barabara kuu za mji mkuu zinazoelekea Barabara ya Al-Thawra, ambapo wahudhuriaji walibeba mabango, bango moja likitanguliza kichwa cha matembezi, huku bango kuu likiwa limeandikwa: “Enyi Enyi majeshi katika nchi za Waislamu, je haijatosha siku 450 hadi musonge kwa ajili ya kuinusuru Palestina” na bango la tatu likiwa na takwimu za majeruhi na mashahidi wa Gaza, na wakati wa matembezi hayo wahudhuriaji waliimba kauli mbiu zilizowahutubia watu jumla na majeshi, miongoni mwazo ni “Ewe askari, amka, kuinusuru Gaza ni faradhi juu yako”, “Ewe Mzayuni, sikiliza, sikiliza Khilafah yetu iliyoondoka itarudi”, “Enyi Maafisa wa jeshi... Mwenyezi Mungu ndiye bwana wenu, bwana bora, na msaidizi bora zaidi”, “Kutoka Tunisia hadi Ash-Asham maagano yetu ni Dola ya Kiislamu”, “Kutoka Tunisia hadi Palestina, Umma ni moja, sio Umma mbili”.
Matembezi hayo yalihitimishwa kwa kalima iliyotolewa na mmoja wa mashababu wa Hizb ut Tahrir iliyoangazia mzingiro wa Jenin katika eneo la Ukingo wa Magharibi na kwamba yanayojiri katika kambi ya Jenin yanapelekea fitna ambazo zitateketeza kila kitu katika njia yake na kuanzisha vita vya umwagaji damu ambavyo vitapelekea, Mwenyezi Mungu apishe mbali, kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. Vita hivi vitasaidia tu mpango wa wavamizi wanaotaka kuwaona watu wa Palestina wanamwagana damu wao kwa wao, na hivyo Hizb ut Tahrir inathibitisha kupitia matembezi yake mfululizo kwamba Umma wa Kiislamu hautazuiliwi na mipaka na hautajagawanywa na mipaka ya Sykes-Picot! Damu yake, heshima yake, na dini yake ni kitu kimoja, sawa na mwili mmoja ikiwa sehemu yake moja itashitakia maumivu, mwili mzima hujibu kwa kukosa usingizi na homa!
Tunamuomba Mwenyezi Mungu awafanyie sahali watu wa Jenin na Gaza na aharakishe ushindi wao kutoka kwa wenye nguvu, wachamungu, watu wenye nguvu na uwezo, maafisa na wanajeshi, ili waweze kuinua bendera ya Uislamu na kusimamisha utawala wa Uislamu, Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia
Ijumaa, 03 Rajab Tukufu 1446 H sawia na 03 Januari 2025 M
- Sehemu ya Amali ya Matembezi –
https://hizb-uttahrir.info/sw/index.php/dawah/tunisia/4468.html#sigProId254605d1e0
- Alama Ishara za Amali -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia