Jumatatu, 04 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/07
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:

Matembezi “Musiitelekeze Rafah kama Mulivyoitelekeza Gaza!”

Matembezi ya 31 mfululizo, tangu kuanza kwa vita vya Kimbunga cha Al-Aqsa, yalianza mbele ya Msikiti wa Al-Fatah katika mji mkuu wa Tunis, ambayo yaliitishwa na Hizb ut-Tahrir/Wilayah Tunisia, kwa watu wa Al-Zaytouna, na kichwa chake kilikuwa“Musiitelekeze Rafah kama Mulivyoitelekeza Gaza!” na kama matembezi yaliyotangulia yalihudhuriwa na umati mkubwa wa watu, ambapo walizunguka katika barabara za mji mkuu kuelekea Barabara ya Al-Thawra, waliinua mabango ambapo bango kuu liliandikwa kichwa cha matembezi hayo, na mengine yalikuwa na takwimu za mashahidi na waliojeruhiwa wakati ambapo umati ulipiga takbira "Allahu Akbar" na kutamka kauli mbiu, ambazo muhimu zaidi zilikuwa “Tunakuitikia tunakuitikia tunakuitikia ewe Rafah”, “Rafah inawalingania Wamisri Mpindueni Al-Sisi Aliyelaaniwa”, “Rafah inawalingania Waislamu iko wapi Ghera, iko wapi dini”, “Rafah inawalingania Wamisri Fuzuni kwa Pepo ya Naim”, “Enyi majeshi, kuweni kwa ajili yake... umbile limekwisha ”…

Matembezi hayo yalihitimishwa kwa kalima iliyotolewa na mmoja wa mashababu wa hizb mbele ya ukumbi wa manispaa katika barabara ya Al-Thawra, ambapo alizungumzia kuhusu kuzingirwa kwa ndugu zetu wa Rafah na mauaji ya kutisha yanayofanywa na umbile hilo chafu dhidi yao yakiwemo kupuuzwa na kusalitiwa na watawala wa Waislamu hususan Al-Sisi mhalifu ambapo kupitia kwayo aliwataka watu wenye nguvu na wanyoofu katika majeshi ya Waislamu kuwapindua watawala hao na kusimamisha Khilafah Rashida ili umma na ulimwengu mzima uondolewe jinai za umbile la Kiyahudi linalokalia kwa mabavu na Makruseda wenye chuki wa Kimagharibi na ulimwengu ufurahie uadilifu wa Uislamu mtukufu.

Hivyo basi, Hizb ut-Tahrir katika Wilayah ya Tunisia inaendeleza nusra yake kwa Gaza, kwani imeshaandaa matembezi 31 tangu kuanza kwa cheche za Kimbunga cha Al-Aqsa, na ina shauku kubwa ya kuukusanya umma na majeshi yake ili waweze kusimamisha Dola ya Kiislamu ambayo Mwenyezi Mungu amewafaradhishia, hivyo kuwaokoa wanadamu wote kutokana na dhulma na uhalifu wa Mayahudi na Makruseda wenye chuki wa Kimagharibi.

Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia

Ijumaa, 09 Dhu al-Qa’adah 1445 H sawia na17 Mei 2024 M

- Sehemu ya Amali ya Matembezi –

- Alama Ishara za Amali -

#طوفان_الأقصى

#الجيوش_إلى_الأقصى

#الأقصى_يستصرخ_الجيوش

#AksaTufanı

#OrdularAksaya

#ArmiesToAqsa

#AqsaCallsArmies

Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu